Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Nimeshindwa kuelewa mamlaka husika hawajaona haya lakini na hawa wasanii kwanini wanafanya hivi, lengo lao hasa ni nini kutoa nyimbo za namna hii huku wakijua wahanga wakubwa ni watoto na vijana wadogo!??

Wasanii wengi ni mawakala wa shetani...

Huitaji mtu mwenye akili kama wewe kuweza kujua kampeni zao, sababu katika nyimbo zao huwa wanafanya vitu vinavyoonekana kama vya kawaida tu kumbe nia yake ni kuelekeza akili za watu wasio na ufahamu kuona mambo wanayofanya ni ya kawaida tu
 
Hapa nakataa nilichokiona ni burudani Tena wote walimu na wanafunzi wanainjoy mziki. Kwani kucheza mziki nakuburudika ni kosa!? Kama siyo mziki unafikri ni kipi kingewaburudisha hao wanafunzi kiasi hicho!? Na kwani huo mziki unakitu Gani au maneno yapi yakusema yaharibu watoto!? Kwangu ni "BIG NO" wameonewa walimu nilitegemea wapongezwe kwa ubunifu wakupiga mziki watoto wanapenda
Wewe nawe ni baba? Yaani hapakuwa na mziki mwingine zaidi ya huo? Kucheza mziki ni sawa lakini wimbo gani? Una maudhui gani kwa hadhira? Yaani wewe maneno ya mpenzi wangu akina namkatika kiuno iko sawa hiyo? Utakuwa mbaba mwenye kasoro!
 
Kabisa kwenye hili wameonewa kiukweli
Huyu Zuchu juzi kati amealikwa na CCM haohao akatumbuize Geita.


Disco tena la wazi kwenye sherehe ni kawaida
Na huo wimbo upo kwenye peak,watoto wanacheza sana..nimekumbuka juzi hapa nyumbani palikuwa na birthday watoto wanacheza hatari..sembuse shule?

Huyo waziri Yeye alisoma Burundi?
Kama alisoma shule za mfagio na kidumu , hicho juu hapo ni kitu cha kawaida sana.

Nchi Ina mahitaji mengi,
Kero mashuleni ni nyingi,
Shule hazina walimu wa kutosha,miundombinu mibovu
Vitabu havitoshi
Matatizo ni mengi..wameacha kutafuta hayo,wamejitoa fahamu wanakwenda kuingilia furaha ya watoto na walimu.
 
Wewe nawe ni baba? Yaani hapakuwa na mziki mwingine zaidi ya huo? Kucheza mziki ni sawa lakini wimbo gani? Una maudhui gani kwa hadhira? Yaani wewe maneno ya mpenzi wangu akina namkatika kiuno iko sawa hiyo? Utakuwa mbaba mwenye kasoro!
mkuu acha makasiriko, acha watoto waenjoy kwa muda
 
Niweke wazi tu bwana waziri kakurupuka kwa sababu hizo nyimbo almost watoto wote wa uswahilini wanaimba ubeti wa1Hadi wa Mwisho[emoji23] kumdemote mwalimu ni uonezi waziri ulitaka hapo waimbe tazama ramani?!!acha unafiki Mzee wangu na usitumie vibaya cheo chako haya maisha Yana kupanda na kushuka
Well said. Ukitazama kwenye video yaani ni watoto wote wanaufahamu wimbo na wanauimba mwanzo mwisho. Kama ni kulinda maadili kwa hawa watoto basi serikali ingeanzia kwenye kuhakikisha kwamba nyimbo zisizo na maadili hazipenyi kwenye media na popote kwingine. Pia mtu au taasisi iliyokwenda kufanya jambo lake shuleni walipaswa kujua au kuambiwa na uongozi/mamlaka iliyowapa kibali cha kufanya shughuli yao hapo shuleni kwamba hawapaswi kupiga nyimbo yoyote isiyo na maadili mbele ya watoto. Na kwa mtazamo wangu hata hao walimu wakuu wanaotakiwa kuvuliwa vyeo vyao angalau basi wangepewa onyo tu na siyo kuwavua vyeo baada ya kuteleza kwenye tukio hilo. Ni mara ngapi hata hao mawaziri wameharibu mambo lakini hadi leo bado wapo ofisini?
 
Wana kosa gani? Hivi unadhani mtumishi wa umma anafukuzwa kazi kama unavyomfukuza mbwa wako hapo nyumbani kwako?
Huyo waziri ni empty set, hao watoto wanauimba huo wimbo wamejifunzia mtaani walikotoka, sidhani kama hao walimu ndiyo wamewafundisha, kama hiyo nyimbo haina maadili basi waziri ashirikiane na mamlaka husika kupiga vita nyimbo zote zisizo na maadili kupigwa kwenye public, kwenye mabasi kama ilivyo kwa pombe kuuzwa bar vivyohivyo miziki ya hovyo ipigwe maeneo walipo watu wa hovyo tu
 
Tuache kuhalalisha ujinga nyie huo wimbo mtaruhusu watoto wenu waimbe nyumbani?? Ni wimbo wenye maadili?? Maneno ya "namkatia uno hani wangu" ndio mnasema hayahamasishi ngono?? Mnataka watoto wayaimbe hayo halafu baadaye mje mseme kizazi hiki kimeharibika?? Wengi mnasema et kama wimbo ulikuwa mbaya kwanini Basata wasifungie yaani kwahiyo Basata wakiruhusu mbaya wewe utaruhusu wanao wasikilize kwa sababu Basata wameruhusu?

Tukubaliane kuwa wimbo hauna maadili kwa watoto, na walimu tumewapa dhamana ya kusimamia maadili ya watoto wawapo shuleni wakiwa nje ya shule ni jukumu la wazazi, sasa mtu anaposema kwenye kampeni za CCM hizo nyimbo zinapigwa hawapigiwi watoto bali watu wazima, na hatuwezi halalisha eti kwa sababu zinapigwa kwenywe kampen za CCM sijui chadema.

Sisi wazazi ndio tunaweza wapa changamoto hao BASATA na WASANII kwa suala zima la nyimbo za maadili, lazima tukubaliane kuwa wasanii miaka hivi karibuni wamekuwa wapumbavu wanaimba Mambo ya ngono tu na wao ndio wanaohamasisha hata ngono kinyume na maumbile, usishangae siku za usoni wakaanza kuusifia ushoga tutashangilia tena
 
Huyu Zuchu juzi kati amealikwa na CCM haohao akatumbuize Geita.


Disco tena la wazi kwenye sherehe ni kawaida
Na huo wimbo upo kwenye peak,watoto wanacheza sana..nimekumbuka juzi hapa nyumbani palikuwa na birthday watoto wanacheza hatari..sembuse shule?

Huyo waziri Yeye alisoma Burundi?
Kama alisoma shule za mfagio na kidumu , hicho juu hapo ni kitu cha kawaida sana.

Nchi Ina mahitaji mengi,
Kero mashuleni ni nyingi,
Shule hazina walimu wa kutosha,miundombinu mibovu
Vitabu havitoshi
Matatizo ni mengi..wameacha kutafuta hayo,wamejitoa fahamu wanakwenda kuingilia furaha ya watoto na walimu.
Halafu wanaita press eti tushuhudie kuwavua walimu wakuu vyeo hii nchi tumerogwa walahi
 
Haya mavi-ongozi ya Tanzania yana akili za kiminyama minyama tu.Kazi kuonea vidagaa tu .
 
Mmh najaribu kutafakari na kuona kosa la walimu mpaka kuvuliwa nyadhifa zao sioni.

Tujiulize haya!

1.Je kosa ni kurekodiwa na kuwekwa katika social media au

2. Mziki kupigwa maeneo ya shule na watoto kucheza.

3. Je ingekuwa siku ya mahafali ya Darasa la saba na wimbo huo ukapigwa na wanafunzi wakaucheza je mwalimu angevuliwa nyadhifa yake?

Kiukweli tunakemea mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu lakini mpaka wimbo umepita basata walichuja wapi na kuona utatumika kwaajili ya wakubwa tu na watoto hawata sikiza wimbo huo?

Watoto wanavyoimba inaonesha wanaujua wimbo tangu awali, this means kwamba kwa siku hiyo tu mwalimu mkuu hajasababisha mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi.

Kumvua cheo mwalimu mkuu ni Kuiambia BASATA kuwa walikosea kuruhusu wimbo huo.
Kwa maoni yangu mwalimu mkuu hana makosa ya kumvua cheo chake.

Yani Kiukweli mawaziri hukurupuka sana katika maamuzi, sijui ni poor kantiri ndo maana na mindset zetu zipo kama hali yetu ya uchumi.

Honeeey.
Kama huoni kosa basi huna akili
 
Free walimu wakuu

Aisee
Akapambane Basata kufunga wimbo
Siyo kuwasumbua Walimu


Huyo mkenda yeye alisoma Primary Ulaya?
Kama amesoma Tz asijifyatue akili.
Hilo tukio ni kitu cha kawaida.
kabisa mkuu, sijui kwa nn anataka kuwanyima watoto haki yao ya msingi ya kucheza na kufurahi na walimu wao.
 
Na kwa mtazamo wangu hata hao walimu wakuu wanaotakiwa kuvuliwa vyeo vyao angalau basi wangepewa onyo tu na siyo kuwavua vyeo baada ya kuteleza kwenye tukio hilo. Ni mara ngapi hata hao mawaziri wameharibu mambo lakini hadi leo bado wapo ofisini?
👍✔️
 
Halafu wanaita press eti tushuhudie kuwavua walimu wakuu vyeo hii nchi tumerogwa walahi
Hivi ni nani huyo kaifanya hii furaha ya watoto kuwa tukio la kiharifu?

Hii nchi Kuna namna viongozi wetu wanarukwa na akili.
Sijui ndo kiwewe cha uongozi.


Wakatekeleze mambo ya msingi.
Miaka 60 ya uhuru ,shule bado watoto wanakaa chini
Ila yapo yanaitana kujadili nyimbo ya Zuchu.

Pumbavu sana,wakajadili na Basata
Ama wamwite Zuchu mwenyewe.
 
Wanasiasa ni watu wapumbav sana maamuzi ya kukurupuka kujipendekeza na uchawa tu vichwa vyao vinawaza kusifiwa na kujikomba komba kwa mamlaka hivyo anatafutwa mnyonge na mnyonge siku zote ni mwalimu,

Waanzie majumbani wawavue vyeo wazazi na walezi hizo nyimbo hazipigwi wala kusikilizwa shuleni ila wanafunzi wanazijua
Mavi kabisa haoo wao wanafanya makosa chungu nzima ,kazi kuonea vidagaa .Mavi kabisa huyo Waziri.
 
Wasanii wa Tanzania siku hizi hakuna kitu na sio kama zamana ambapo msanii alikuwa kioo cha jamii .
Mziki ulikuwa wa zamani siku hizi ni njaa tu zinawasumbua.
 
Being positive, hapo hakuna kosa. Ni burudani baada ya kazi, sasa kwani wakicheza ngoma zetu za asili hawakati viuno?
Hawa mawaziri wajiepushe na kauli za kukurupuka.
 
Back
Top Bottom