Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Na hao hao CCM watayakata mauno jukwaani ili wapewe kura

2015 walicheza mapanga ya TMK .

Si ajabu mwaka 2025 wakaja na zuchu..na hata kwenye ziara zake wanaenda naye ,si ndio hizo hizo nyimbo anazoimba?
Ila hapo wanawaona walimu wakosaji.


Hiyo nyimbo watoto wengi wanapenda,na usipowawekea wanaidai.
Wawaache walimu.
Kabisa kwenye hili wameonewa kiukweli
 
View attachment 2801642

Baada ya kipande cha video kinachowaonesha watoto wa shule za msingi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu ‘Honey’ wilayani Tunduma kusambaa mitandaoni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza walimu wakuu wawili wa shule hizo wavuliwe vyeo.

Amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu video hiyo ambapo pia amepiga marufuku wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka walimu kuwa wasimamizi wa maadili pindi wanafunzi wawapo shuleni.

“Tumeshatambua shule yenyewe iko Tunduma, kulikuwa na kikundi kimeenda kutoa msaada shuleni pale, baada ya kutoa msaada ule kikaweka na muziki halafu wanafunzi wakacheza, na maudhui ya muziki wenyewe kila mtu ameusikia sina haja ya kuurudia,” amesema Profesa Mkenda.

Ameongeza, “tumeongea na wadhibiti ubora wapeleke taarifa kule, mkurugenzi awaondoe walimu wakuu wa shule mbili; moja shule ya Tunduma na nyingine ambazo ni kama shule pacha, waondolewe madaraka ya ukuu wa shule watafutwe wakuu wengine wa shule. Tunafanya hivi ili kutuma ujumbe, walimu wakuu tusaidieni msiruhusu vitu kama hivi viingie mashuleni.”

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wote na wanaohudumia watoto kusimamia malezi na makuzi ya watoto.
Akili zetu tz tunazijua wenyewe,sasa kama nyimbo hazina maadili kwa nini wali zipitisha,huu wimbo na ule wa nay,upi hauna maadili.
 
Siongei mengi... Ni kweli!?? Wamefukuzwa kazi!?? Anyone.,..!!
View attachment 2801918
Aliyewasimamisha kazi atakuwa ni mpumbavu.

Huyu Zuchu si juzi kaalikwa Geita kwenye ziara za CCM akatumbuize!
Si ndio nyimbo hizo alikuwa anaimba?

Shule miziki kama hii kwenye sherehe ni kawaida..na ilianza Toka enzi za Mwalimu,la Saba wanapomaliza mitihani huwa kunaambatana na sherehe na miziki..
Labda kama huyo waziri na CCM wao walisoma Burundi.

Waache upumbavu.
Watoto mtaani wanacheza hii nyimbo sana maana imekaa kitoto .
Kama wapo serious basi wangeifungia ama waanze kuwaadhibu wote wanaoicheza..ambapo wataadhibu watoto wote sasa..hakuna mtoto hajui hiyo..tunajionea mtaani huku.
 
Waziri husika huyo ni nani!?

Hao Walimu wamefanya kosa gani!??

Ahhh!!!
Hivi Watanzania akili tumemkopesha nani siku hizi? Huo wimbo una maadili gani ya kumfundisha mtoto? Umeyasilikiliza vizuri hayo maneno yanayotamkwa kwenye huo wimbo? Tunatetea vitu vya kijingaa
 
this is purely insane, yaani imefika hatua waziri anawanyima watoto haki yao ya msingi ya kucheza na kufurahi?
Huyo Waziri angejua jinsi gani Walimu huku vijijini wanapambana na dropout ya wanafunzi..utoro...

Ilibidi hawa walimu awapongeze sana.
 
Back
Top Bottom