Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Kwani hao watoto wamejifunza huo wimbo shuleni?

Huo wimbo wamejifunzia wakiwa kwao kwa wazazi wao na huko mitaani, ndio maana wanajua kuuimba wote na kuucheza kama Zuchu. Wawashushe vyeo na wazazi wa hao watoto

Walimu wakuu wameonewa

Nje ya mada: Ila wakuu Zuchu anajua aisee hii ngoma nimekaa nimeisikiliza vizuri ina vibe
 
Nina wasiwasi na maamuzi ya prof.. kashinikizwaa bila ku think twice..ahah hapana prof tunamjua ye ni great thinker..natumaini angepata muda wa kutafakari angepuuza..cz alichokifanya ni kuziba tundu la panya kwa mkate.. kama kweli alinaanisha basi karuka process za kutatua tatizo.. Ambazo wao wametufundisha kwenye research. Asante kwa taarifa pia nawakumbu Elimu ya msingi mwsho darasa la sita kuanzia 2027.
 
Mmh najaribu kutafakari na kuona kosa la walimu mpaka kuvuliwa nyadhifa zao sioni.

Tujiulize haya!

1.Je kosa ni kurekodiwa na kuwekwa katika social media au

2. Mziki kupigwa maeneo ya shule na watoto kucheza.

3. Je ingekuwa siku ya mahafali ya Darasa la saba na wimbo huo ukapigwa na wanafunzi wakaucheza je mwalimu angevuliwa nyadhifa yake?

Kiukweli tunakemea mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu lakini mpaka wimbo umepita basata walichuja wapi na kuona utatumika kwaajili ya wakubwa tu na watoto hawata sikiza wimbo huo?

Watoto wanavyoimba inaonesha wanaujua wimbo tangu awali, this means kwamba kwa siku hiyo tu mwalimu mkuu hajasababisha mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi.

Kumvua cheo mwalimu mkuu ni Kuiambia BASATA kuwa walikosea kuruhusu wimbo huo.
Kwa maoni yangu mwalimu mkuu hana makosa ya kumvua cheo chake.

Yani Kiukweli mawaziri hukurupuka sana katika maamuzi, sijui ni poor kantiri ndo maana na mindset zetu zipo kama hali yetu ya uchumi.

Honeeey.
umeambiwa aina ya wimbo, utumie akili na wewe
 
Siongei mengi... Ni kweli!?? Wamefukuzwa kazi!?? Anyone...!!

View attachment 2801918
Bro uko mkoa gani kwanza yaani unatuletea ushamba wa hali ya angalia nchi za wenzetu mifumo yao ya elimu time kubwa watoto wanacheza lkn wako very bright sasa na sisi tutumieni mifumo hiyo hiyo sio mikwaju tu kila wakati lazima serikali ibadilishe mifumo tuwalee watoto wetu kutokana na mazingara ya sasa .
 
Tunadhibit
Mwanangu juzi ananiimbia hizo nyimbo,nikamwuliza umesikia wapi?manake nyumbani hazipigwi na Kuna channel tumeblock,akanambia anatupigiaga dreva tukienda shule[emoji1787]nikamwambia lol nitaongea na mwalimu,akanambia , hapana usimtaje[emoji1787][emoji23]akamwonea huruma kibarua chake mzee yule
Nikamwambia,ok usiwe unazisikiliza si nzuri,akajibu sawa mama,tukamaliza[emoji120]
Huwezi kuepukaa, hata akikosa kwa Gari ya shule, je akiwa mtaan na watoto wenzie.?
 
Halafu kwenye kampeni za CCM ni nyimbo hizo hizo zitatumika kukusanya watu, yaani vitu vingine vinachekesha kweli walimu wanateseka sana nchi hii mara wachapwe, wakimbizwe kama watoto, wafanywe masanamu km hivi nao wameinama tu kama makondoo
Pia hao hao Walimu watatumika kuishindisha sisiemu[emoji1][emoji1]
 
Visharobaro vyabaadae vinaburudika na vi pisi Kali vyao...[emoji23]
Maisha kama mahanjumati fulani hivi yana kabla ya kupikwa na baada ya kupikwa!
Hapa nakataa nilichokiona ni burudani Tena wote walimu na wanafunzi wanainjoy mziki. Kwani kucheza mziki na kuburudika ni kosa!? Kama siyo mziki unafikri ni kipi kingewaburudisha hao wanafunzi kiasi hicho!?

Na kwani huo mziki una kitu Gani au maneno yapi ya kusema ya haribu watoto!? Kwangu ni "BIG NO" wameonewa walimu, nilitegemea wapongezwe kwa ubunifu wa kupiga mziki watoto wanapenda.
Mkuu ni Muziki siyo mziki
 
Halafu kwenye kampeni za CCM ni nyimbo hizo hizo zitatumika kukusanya watu, yaani vitu vingine vinachekesha kweli walimu wanateseka sana nchi hii mara wachapwe, wakimbizwe kama watoto, wafanywe masanamu km hivi nao wameinama tu kama makondoo
Sas watafanyajeee? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Visharobaro vyabaadae vinaburudika na vi pisi Kali vyao...[emoji23]
Maisha kama mahanjumati fulani hivi yana kabla ya kupikwa na baada ya kupikwa!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hawajafukwa Kazi Isipokuwa Walimu Wakuu Maagizo Toka Kwa Waziri Husika
Kasema Watolewe Vyeo Vya Ualimu Mkuu, Kwa Hilo Jambo
Profesa Mkenda naye ni Kilaza tu. Sasa hao wanafunzi kucheza huo wimbo wa Zuchu - Honey wana kosa gani!!

Na kama huo wimbo hauna maadili, ni kwa nini haujafungiwa na Basata? Au nyimbo zinazofungiwa ni zile za akina Ney wa Mitego pekee, kwa sababu zinaikosoa serikali yake ya ccm?
 
Back
Top Bottom