Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

hiyo ni salamu za enzi zile za kitumwa salamu hii ilianzishwa na warabu dhidi ya watanganyika ,shikamoo maana yake niko chini ya miguu yako e bwana angu ,marhaba maana yake endelea kuwa chini yangu eeh mtumwa wangu....hii salamu ni kielelezo cha utumwa.
 
Na pia inatumika kama ngao kwa wanawake kuwakata ngebe 'wazee vijana'.

Unakuta mko makamo sawa, akihisi unataka kutoa ya rohoni basi anakuzungushia lishikamoo kuuubwa ili ujibahave!

Ukijibu salamu hiyo kuja kuzinduka kuanza kupanga mistari ya kuweza kumuwin, tayari huyo kishafika zake mbali!

Kumbe dawa ukipigwa shikamoo na mtu unayemtamani, jikohoze kujifanya haujamsikia.

Akikuandamisha nalo mara mbili mara tatu, mchane... 'kuniamkia shikamoo mkubwa mwenzangu unataka kuninyima nini', ili naye aone haya ahangaike cha kukujibu.

Maana sasa tunadhalilishana!
Imekuwa shikamoo si shikamoo, huku mtu kakukazia macho usoni kukutathimini, inahuu?

Na kweli pendekezo la mdau lipite ipatikane salamu isiyobagua makamo kama ilivyo kwa wasukuma na salamu yao ya, 'ng'wadilah'.
 
Hata wazee ambao huwa naswali nao ni assalaam alikum kwa kwenda mbele na ni dua pia safi kabisa
 
Ukiwa na pesa we tajirii oh hata usipo sema shikamoo wazee watakupa na kushangiliwa kwa maneno matamu na utaamkiwa tu hadi na hawa wazee hataa kama mdogo huna mvii ndiyo ujue pesa mwanaharamuπŸ˜…
πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nimeipenda hiiπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hata wazee ambao huwa naswali nao ni assalaam alikum kwa kwenda mbele na ni dua pia safi kabisa
Hao hawana Shida maana ndio salamu yetu hiyo akhy Kwanza "nakushikamoo " haina fadhila zozote sema tu kuna baadhi hawaridhiki mpaka uweke hiyo juu ya salamu nyingine
 
Dada yangu namzidi miaka 5 tukikutana Ananishikamoo kiheshima, dogo anayefuata namzidi 8yrs yeye ni wa mambo vipi.
Madada waliobaki napokea shikamoo.
Kimbembe kumpa shikamoo mama mdogo ninayemzidi umri miaka 15 hivi
 
Ahaaa !! Mimi mke wangu ananisalimia shikamoo Ila tukikutana live hanipi shikamoo shikamoo yake inaishia katika simu
Dah hii nayo ya mke kumsalimia mume inakuwaje?

Kwa upande wangu naona kama sio poa yani
 
Noted expert wangu
 
Hahaha hii inanikuta mimi kuna mda nawasalimia wadogo zangu kabisa siku hizi watu wanakua haraka sana hasa wanawake hahahaha kuna profesa mmoja nikimuamkia shikamoo haitikii na madam flani ivi alikua mwalimu wangu wa kozi hahah
Shikamoo ina boa sana expert wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…