Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Hata mimi kuna braza kwa mama mkubwa nae ana mwili kama huo,anapenda shikamoo balaa,sasa sisi tunamchukulia poa,ila anaitaka kwa nguvu zote

Haya maisha bwana wengine hawataki shikamoo na wengine wanaitaka basi ni shida tu kwakweli
 
😂😂😂
 
Aisee,sio poa kabisa hii sslamu
 
Nitakuwa nimerithi expert wangu,kwa kawaida mara nyingi kidevu ndio huanza kupata mvi
 
Kipind nimetoka toka tu chuo nimanza kazi, mkurugenz wangu ambaye ndio mwenye kampuni alikua amenizid umri wa miaka 10 na siku pekee aliopata shkamoo yangu ni siku naingia kwenye interview. Baada ya hapo mpaka naondoka kazin sikiwah mpa shkamoo.

Ukiachana tu na wewe kuona uzito kuamkia, hata watu wazima ukitazama kwa makini utakuja kugundua kuwa hawapendelei sana kuamkiwa na vijana kuanzia rika flani , labda awe mzee may be
 
Sio kweli ,wanasalimia kwa kichaga , huko kwa wa Iraq karatu na babati ukivaa ukapendeza halafu sio mtu wa huko ndio unasalimiwa shkamoo na marika yote.
Kule kwa wairaq na hasa kwa wafugaji wote wanajua Shikamoo ni salamu ya Mwalimu na mtu mtu mgeni. Hivyo ukiwa mwalimu utakuwa unapokea Shikamoo za wanafunzi wa wazazi wao. Pia ukiwa siyi mtu wa kabila lao utakuwa shikamoo kwa sana.
 
Kule kwa wairaq na hasa kwa wafugaji wote wanajua Shikamoo ni salamu ya Mwalimu na mtu mtu mgeni. Hivyo ukiwa mwalimu utakuwa unapokea Shikamoo za wanafunzi wa wazazi wao. Pia ukiwa siyi mtu wa kabila lao utakuwa shikamoo kwa sana.
Yeah wewe unawajua vizuri mno
 
Na umri huo unasalimia watu shikamoo ili iweje? Aah wee mi nilishaacha labda wale wazee kabisa
Ukiwa mkubwa halafu ukose pesa , then upitwe na kitoto ambacho juzi juzi tu ulikiona kina jipupulia bila salamu ,ndio utajua mziki wake unakuaje.
 
Hii salamu maadam mtu ni mkubwa kwako unatakiwa uitoe

Sisi nyumbani tulilazimishwa kuamkiana,huyo mdogo wangu wa kike alikuwa hani amkii,mama ndio akamwambia ebu mwamkie kaka yako,mwanzoni alikuwa anacheka akiniamkia ila now ameshazoea

Dada yangu nae nilikuwa simwamkii,kupitia shinikizo la bimkubwa basi namuamkia

Sisi wenyewe wala hatukujali ila bimkuwa ndio akashika bango
 
walimu tunasalimiwa mpaka na babu na bibi zetu shikamoo mwalimu unajshtukia ila unaitikia tu🤠🤠
 
Ukiwa mkubwa halafu ukose pesa , then upitwe na kitoto ambacho juzi juzi tu ulikiona kina jipupulia bila salamu ,ndio utajua mziki wake unakuaje.
🤣🤣🤣 hilo nalo neno!
Watoto watusalime tu kwakweli. Ila kwa sisi watu wazima kusalimiana shikamoo shikamoo mmmh ni issue!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…