Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuanzia sasa Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule Profesa J anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi hapo atakaporuhusiwa kurudi nyumbani.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipofika Muhimbili leo kumjulia hali Msanii huyo.

1644587800108.png


Pia soma:
Tumuombee sana Profesa J
Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?

Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.
 
Mhh !!!!

Haya ni Majibu mepesi kwa Maswali Magumu..., Hakikisheni gharama za Matibabu ni rafiki kwa kila kiumbe na sio kutoa Charity everytime you see Fit..... (which most of the time you don't)

Hayupo pale kuchague nani alipe na nani asilipe bali kuhakikisha Healthcare is Reachable and Affordable for All....
 
Ila wanyonge wasiothaminika katika nchi wananyimwa fursa ya kuchukua na kwenda kuzika miili ya wapendwa wao pindi wanapofariki katika hospitali hizo hizo za umma licha ya kutamka hadharani kuwa hawana pesa za kulipa kutokana na umasikini wao.
🤔
 
Watanzania walivyo wapumbavu watashangilia na kuruka ruka huku wakibinua makalio kana kwamba waziri ametatua changamoto ya afya kitaifa.

Jiulize wewe, mtoto au mzazi au ndugu yako akiumwa atapata hiyo favour?au ni wale waliokula keki ya taifa wanaipata hiyo neema peke yao?

Tunahitaji kupaza sauti juu ya bima ya afya kwa kila raia wa Nchi hii. Ni heri tutumie fedha kuhudumia afya ya za wananchi wetu huku wakiwa wanapita kwenye barabara zenye foleni kuliko kuwapitisha kwenye flyover wakiwa ndani ya jeneza.
 
Habari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinasema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali itagharimia matibabu ya mwanamziki maarufu wa kizazi kipya ambaye pia alikuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule, a.k.a Prof. J aliyelazwa katika Hospitali hiyo. Hayo yameandikwa katika mtandao wa jamii wa Twitter.

Pongezi kwa serikali kwa kuwaenzi viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom