Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuanzia sasa Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule Profesa J anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi hapo atakaporuhusiwa kurudi nyumbani.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipofika Muhimbili leo kumjulia hali Msanii huyo.

Pia soma:
Tumuombee sana Profesa J
Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu

Huku ni kudhalilishana. Kama taifa tungekuwa na serikali ya kueleweka, huduma muhimu kama za afya na elimu ingekuwa bure kwa watu wote. Hatungekuwa na huu ujinga wa kudhalilishana nanma hii.
 
Nadhani gharama zinatakiwa kulipwa na NHIF kwa kuwa ulikwisha changia kwa miaka kadhaa iliyopita.
Huu uongo huwa unawasaidia nini? Bima inacover pale tu inapolipiwa
Ni sawa na umekata bima ya gari kwa miaka 10 alafu mwaka wa 11 hujakata alafu ukipata ajali unataka bima ikulipe kisa tu kwa miaka 10 ulikua unachangia?
Nchi Ina watu hii, suala dogo Kama hili tu watu hawaelewi na ndio tunatakaa sijui Tanzania ya viwanda
 
Wakati Kayafa alipokuwa anapita Mabarabarani na kugawa maburungutu ya fedha,je aligawa kwa Watanzania wote wenye shida?
 
Huu uongo huwa unawasaidia nini? Bima inacover pale tu inapolipiwa
Ni sawa na umekata bima ya gari kwa miaka 10 alafu mwaka wa 11 hujakata alafu ukipata ajali unataka bima ikulipe kisa tu kwa miaka 10 ulikua unachangia?
Nchi Ina watu hii, suala dogo Kama hili tu watu hawaelewi na ndio tunatakaa sijui Tanzania ya viwanda
Wee ng'ombe wastaafu wa serikali wanagharimiwa na NHIF hadi wafe!
 
Watanzania walivyo wapumbavu watashangilia na kuruka ruka huku wakibinua makalio kana kwamba waziri ametatua changamoto ya afya kitaifa.

Jiulize wewe, mtoto au mzazi au ndugu yako aliumwa atapata hiyo favour?au ni wale waliokula keki ya taifa wanaipata hiyo neema peke yao?

Tunahitaji kupaza sauti juu ya bima ya afya kwa kila raia wa Nchi hii. Ni heri tutumie fedha kuhudumia afya ya za wananchi wetu huku wakiwa wanapita kwenye barabara zenye foleni kuliko kuwapitisha kwenye flyover wakiwa ndani ya jeneza.
Kama lile limradi la Ringroad Dodoma liAnitia kichefuchefu kweli nikilinganisha na gharama za huduma za afya
 
Ni maamuzi mazuri ingawa italeta maswali kwa jamii nyingine, ila ni vizuri zaidi kuwepo na sera ya ujamaa katika kupata matibabu kwa watu wote.
 
Watanzania hatuna jema kwa kweli, kama hadi hili la Prof J kusaidiwa inakuwa nongwa?
Ukiishi kwenye jamii pana na akili yako ukaiweka huru utajua kwanini mdau ameandika hivyo,kuna siku niliingia pharmacy moja Kariakoo nikamkuta yupo jamaa ameingia mule kuomba dawa (sikumbuki zilikuwa za maradhi gani maana siyo Dr) ila yeye akizitaka kwa msaada na wakati huo ilionekana kinachomsumbua ndiyo kilikuwa kimekaza kuuma na hela mfukoni hana na mule ndani wote hawajui wafanyeje!

Hizo dawa zilikuwa zina-cost Tsh 7,000/= tu so fikiria ni wangapi wanateseka na maradhi ktk umaskini wao na wakuwaokoa hawana?issue siyo Jay kutibiwa na serikali the issue ni serikali kwa ujumla kuweka mazingira bora ili kila mtu ktk hangaiko lake apate pakujishikiza,kama akawa mkulima au mwanasiasa sijui msanii wote ni haki yao kupata tiba kwa unafuu wowote unaowezekana.
 
Shetani akizeeka hugeuka kuwa malaika. Yaani Ccm ile ile iliyo kataa kumtibu Lissu na kumfukuza bungeni bila mafao wameona nini kumtibu Prod Jey walio mpora ubunge?
Hawa jamaa ninwaigizaji kama wale wa futuhi..... Hatuja sahau mlivyo mvunja Mbowe mguu halafu mkasema alianguka bar.
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?

Nchi yetu ina shida sana. Wale wasiokuwa na majina wanakufa kwa kukosa matibabu na hakuna anayejali.

This is a guy who could have easily been able to enroll in a health insurance plan when was healthy, but he chose not to. It doesn’t make any sense that Tanzanian taxpayers now have to foot his medical bill. Ujinga mtupu!
 
SERIKALI INAYOONGOZWA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUGHARAMIA MATIBABU YA JOSEPH HAULE (PROF JAY)

Huu ni mwezi wa Upendo, kaka yetu na rafiki yetu Prof Jay amelala kitandani sasa akipigania uhai wake. Licha ya kuwa msanii wa Hip Hop aliyejengea sanaa ya muziki Bongo katika sekta zenye kuingiza kipato kwa Vijana wengi, lakini Prof Jay alikuwa mwanasiasa wa Upinzani hii haitoshi kumfanya awe adui kwenye mlengo tofauti wa kisiasa. Rais Samia ameonyesha upendo kwa kuiongoza serikali kugharamia matibabu ya Prof Jay.... Hakika Tanzania itajengwa na Vijana wenye upendo. #mamayukokazini

Screenshot_20220211-172602.jpg
 
Mtu alikuwa mbunge kwa miaka 5 hana uwekezaji wa kulipa gharama za matibabu!!!!! Pathetic. I remember they received gratuity in the region of 300m/= tax exempted. Inafikirisha
 
Watanzania walivyo wapumbavu watashangilia na kuruka ruka huku wakibinua makalio kana kwamba waziri ametatua changamoto ya afya kitaifa.

Jiulize wewe, mtoto au mzazi au ndugu yako aliumwa atapata hiyo favour?au ni wale waliokula keki ya taifa wanaipata hiyo neema peke yao?

Tunahitaji kupaza sauti juu ya bima ya afya kwa kila raia wa Nchi hii. Ni heri tutumie fedha kuhudumia afya ya za wananchi wetu huku wakiwa wanapita kwenye barabara zenye foleni kuliko kuwapitisha kwenye flyover wakiwa ndani ya jeneza.
Kwani wewe ni wa Taifa gani hadi useme watanzania ni wapumbavu. Kama ni mtanzania ujue unawakashifu ndugu zako wengi ikiwemo baba na mama yako. Shame on you.
 
Back
Top Bottom