Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?
Chadema mmefungiwa mlango wa upigaji, mlianza kuchangisha muibe
 
Hii inaweza kuwa kama rushwa kwa wanasiasa na wabunge, hawa watu watashindwa kutetea maslahi ya wananchi wakiamini serikali will take care of them..

Ilipaswa kuwa fundisho ili watete kwa nguvu maslahi ya wananchi kwenye suala zima la Afya na Elimi wakitambua nao siku watafika kwenye hizo hospitali..
 
SERIKALI INAYOONGOZWA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUGHARAMIA MATIBABU YA JOSEPH HAULE (PROF JAY)

Huu ni mwezi wa Upendo, kaka yetu na rafiki yetu Prof Jay amelala kitandani sasa akipigania uhai wake. Licha ya kuwa msanii wa Hip Hop aliyejengea sanaa ya muziki Bongo katika sekta zenye kuingiza kipato kwa Vijana wengi, lakini Prof Jay alikuwa mwanasiasa wa Upinzani hii haitoshi kumfanya awe adui kwenye mlengo tofauti wa kisiasa. Rais Samia ameonyesha upendo kwa kuiongoza serikali kugharamia matibabu ya Prof Jay.... Hakika Tanzania itajengwa na Vijana wenye upendo. #mamayukokazini

View attachment 2116240
Lissu alipopigwa Risasi Rais Samia alikwenda kumtembelea hospital Nairobi, Prof Jay anaugua serikali inalipa Fadhila kwa kugharamia matibabu yake. Samia ana Upendo sana.
 
Mkuu , ukiugua figo , bima haisaidii
Na hapo ndipo shida ilipo kama nachangia Kila mwezi lakin nikipata ugonjwa mzito kama huu sisaidiwi hiyo bima ni ya nini?
Ya kutibu malaria? Nini tofauti Kati ya mtu mwenye bima na asiyenayo kama mambo yako hivi? Ni nini kinaangaliwa ili magonjwa mengine yaondolew kwenye bima? Nini mchango wa serikali kwenye kufanya huu mfuko ushindw kuhudumiwa wanachama?
 
SERIKALI INAYOONGOZWA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUGHARAMIA MATIBABU YA JOSEPH HAULE (PROF JAY)

Huu ni mwezi wa Upendo, kaka yetu na rafiki yetu Prof Jay amelala kitandani sasa akipigania uhai wake. Licha ya kuwa msanii wa Hip Hop aliyejengea sanaa ya muziki Bongo katika sekta zenye kuingiza kipato kwa Vijana wengi, lakini Prof Jay alikuwa mwanasiasa wa Upinzani hii haitoshi kumfanya awe adui kwenye mlengo tofauti wa kisiasa. Rais Samia ameonyesha upendo kwa kuiongoza serikali kugharamia matibabu ya Prof Jay.... Hakika Tanzania itajengwa na Vijana wenye upendo. #mamayukokazini

View attachment 2116240
Mambo mengi anafanya vizuri, isipokuwa kesi ya Mbowe na kakataa katiba mpya ya wananchi. Huku yeye akiwa makamo mwenyekiti wa bunge la katiba !!
 
SERIKALI INAYOONGOZWA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUGHARAMIA MATIBABU YA JOSEPH HAULE (PROF JAY)

Huu ni mwezi wa Upendo, kaka yetu na rafiki yetu Prof Jay amelala kitandani sasa akipigania uhai wake. Licha ya kuwa msanii wa Hip Hop aliyejengea sanaa ya muziki Bongo katika sekta zenye kuingiza kipato kwa Vijana wengi, lakini Prof Jay alikuwa mwanasiasa wa Upinzani hii haitoshi kumfanya awe adui kwenye mlengo tofauti wa kisiasa. Rais Samia ameonyesha upendo kwa kuiongoza serikali kugharamia matibabu ya Prof Jay.... Hakika Tanzania itajengwa na Vijana wenye upendo. #mamayukokazini

View attachment 2116240
Tuna taka kumuona Mbowe akiwa huru keshooooooo
 
‪Ni hatua nzuri sana. Ni jambo jema serikali sasa imeamua kuchukua jukumu la kuhudumia gharama za matibabu ya Professor Jay baada ya siku 19 za kujiuguza mwenyewe hadi atakaporuhusiwa kutoka. Kimsingi sielewi kwanini wakati wa Magufuli na Ndugai (Samia akiwa VP), Tundu Lissu alinyimwa matibabu halali, tena akiwa mbunge.
 
Ni maamuzi mazuri ingawa italeta maswali kwa jamii nyingine, ila ni vizuri zaidi kuwepo na sera ya ujamaa katika kupata matibabu kwa watu wote.

Kabisa,na hii inatakiwa iwe Haki ya msingi ya Raia.Haiwezekani Mtu awe ana Haki ya kuishi kisha akiumwa anaweza kufa kwa kushindwa kupata matibabu sababu ya gharama,na Maiti yake izuiwe kwenda kuzikwa kwa sababu ya deni hilo!
Matibabu yanapaswa kuwa kama huduma zingine zote muhimu anazopewa Mwananchi.Imewezekanaje Elimu kuwa bure,Maji na Umeme kwa gharama nafuu ishindikane kwenye Matibabu!
 
Za kuchangia mawakili wamtoe mtu, mahabusu zinapatikana,
Lakini za kuchanga matibabu apate mtu, watu wa chama mashati washikana,
Chama cha mgonjwa cha "watu", ukitaja mgonjwa mwapishana,
Heko Mheshimiwa Ummy Mwalimu, utu wa mtu kuupambania.
 
Kuna watu wamepanic jamaa kutibiwa na serikali
Mkuu hakuna mtu aliyepanik ila issue ni kwamba Kuna watanzania wengi wa Hali ya chini Wana matatizo kama haya ambao hawana msaada kabisa hivyo basi kama serikali imeweza kumsaidia Prof J maana yake inakiri kwamba sera yetu ya afya haiko vizuri kwani kwa wasio na wakuwasemea ni kufa tu.
 
Lissu alipopigwa Risasi Rais Samia alikwenda kumtembelea hospital Nairobi, Prof Jay anaugua serikali inalipa Fadhila kwa kugharamia matibabu yake. Samia ana Upendo sana.
Ni Mama yetu sote. Nampenda sana. Mungu ambariki sana.
 
Mtu alikuwa mbunge kwa miaka 5 hana uwekezaji wa kulipa gharama za matibabu!!!!! Pathetic. I remember they received gratuity in the region of 300m/= tax exempted. Inafikirisha
Mkuu ugonjwa wa muda mrefu hela zinaisha kabisa kumbuka hapo huenda ameanza kuugua muda tu akijitibu mwenyewe.
Suala hapa ni ima uwe mbung au kapuku fulani kuwe na utaratibu wa kuhakikisha mtu anachangia kidogo na serikali inaongeza ili siku akiugua awese kupata matibabu.
 
Back
Top Bottom