Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali
Za kuchangia mawakili wamtoe mtu, mahabusu zinapatikana,
Lakini za kuchanga matibabu apate mtu, watu wa chama mashati washikana,
Chama cha mgonjwa cha "watu", ukitaja mgonjwa mwapishana,
Heko Mheshimiwa Ummy Mwalimu, utu wa mtu kuupambania.
Umeandika lugha gani
 
Maamuzi haya yana agenda ya siri nyuma ya pazia, ni namna fulani ya kuinanga Chadema.
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?
Shangaa mkuu!

Pr J alikuwa msanii anaeingiza hela kutokana na umaarufu wake!
Akaenda bungeni ambako kwa miaka 5 amevuna zaidi ya nusu bilioni,
Leo hii anachangiwa matibabu na selikali ambapo wala si mtumishi wa selikali,

Sijui mtz wa kule sitimbi atatibiwaje?
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuanzia sasa Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule Profesa J anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi hapo atakaporuhusiwa kurudi nyumbani.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipofika Muhimbili leo kumjulia hali Msanii huyo. #MillardAyoUPDATES
 
Hapa ukiweka tu siasa unaharibu hata maana ya Msaada...

Prof J ni my favorite rapper of All time... Nawaombeni tumuache apone kwanza ndio tuendeleze siasa...

Tumuombee Prof Jay apone mapema
 
Bahati ya mtu msiilalie mlango wazi. Wengi mmemnanga sana kisa kuomba achangiwe haya Mungu si Athumani Rais kaamua asaidiwe mbona watu wengi tu wanasaidiwa na sio watumishi wa serikali??

Yani ishu ni Prof Jay tu Wala sio utanzania wake? Whether alikuwa na hela lakini kwa sasa hana za matibabu so tumuache afe?

Ombeni bahati wandugu, hata shule tunasoma wote Ila omba bahati ya kupata kazi nzuri. Tumesoma na hadi wengine ni mawaziri Ila Sasa ndio iwe bahati akukumbuke tu.

Ombeni bahati na kutibiwa sio kwamba ndio atapona msilalamike Ila nae no mtanzania ana haki kwa bahati aliyonayo.
 
Mkuu jamaa nayeye si anamajukumu kadhaa,, kwani ukipata kiinua mgongo ndio hela itakaa tu..

Gharama za matibabu yake ni kubwa sana.
Watu Wana wivu sana dah. Kwa hiyo asitibiwe kisa alikuwa mbunge wa awamu moja ?

Watanzania hawana shukrani ndio maana huwa nawashauri watu wakati mwingine heri uwe CCM tu maana kijana amewapigania sana jimboni Ila leo watu wanamsema vibaya.

Alikataa offer ya kusaliti chadema in return agombee Mikumi Ila kwa ticket ya CCM akakataa. Leo kila mtu anamtusi hivi akipona atabaki kwa watu wasio na shukrani??

Ombea usipatwe na vitu viwili duniani, umasikini na wivu.
 
Back
Top Bottom