Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?
Ni jambo jema lakini vipi maelfu wanaokufa wakikosa pesa za kutibu wapendwa wao hata kiasi kidogo tu.

Ni wakati muafaka Gvt kuanzisha universal medical insurance covers kwa wananchi wasio na uwezo sio kutoa msaada kwa wachache sana maarufu ambao wanaweza kuchangiwa hata na vikundi na watu walikaribu nao.
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuanzia sasa Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule Profesa J anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi hapo atakaporuhusiwa kurudi nyumbani...
Bima ni muhimu sana . Nilisikia anafanya dialysis ambayo ni expensive sana na ni matibabu yanaendelea mpaka upate figo nyingine. Hata kama una pesa kutumia Tsh 2M kwa matibabu kila mwezi ni pesa nyingi sana kama hauingizi pesa
 
Habari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinasema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali itagharimia matibabu ya mwanamziki maarufu wa kizazi kipya ambaye pia alikuwa Mbunge wa Mikumi Bw. Haule, a.k.a Prof. J aliyelazwa katika Hospitali hiyo. Hayo yameandikwa katika mtandao wa jamii wa Twitter.

Pongezi kwa serikali kwa kuwaenzi viongozi wetu.
Unafiki wa serikali ya CCM, mbona walishindwa kugharamia matibabu ya kisheria na kikatiba ya lissu walipojaribu kumuua akiwa bado mbunge!
 
Back
Top Bottom