Michango isitishwe sasa
Maana kwenye vimedia uchwara
Naona watangazaji washaanza...
Kuwaomba watu watoe hela

Ova
Isitishwe>????? Wewe usitoe na hatuamini tu! hii ahadi ilitolewa wakati Tundu alipomininiwa gololi 38 matokeo yake??
 
Michango iendelee mkuu!; kwani ilichangwa Kwa sababu Jay ni mtu maarufu au Kwa sababu ni binadamu au ilichangwa Kwa malengo yaliyojificha na Sasa watu wamekasirika kuwa malengo yao yamekwama?

Michango iendelee na wapewe hao wengine uliowaita makapuku. !!
 
wewe ni nani hadi ututukane watu zaidi ya milioni 50 ni wapumbavu ?
 
Hiyo sio nongwa. Tatizo sio yeye kusaidiwa. Asaidiwe privately.

Ni discrimination kutumia pesa ya umma kumsaidia mtu mmoja ilhali watu wengine walio katika situation kama yake wakiachwa kujipigania wenyewe!
hili lipo toka enzi na enzi, hata kwa Mungu hakuna usawa,hata Yesu aliwahaidi pepo wale jamaa aliosurubiwa nao, utauliza kwanini wale aliwakubalia kuwa nao katika ufalme wa mbinguni huku akiacha wengine wajipiganie wao ?
hata Mungu alimsifu Ayubu,je watu wengine wangelalamika kwanini hajawasifu ?
 
Ummy,

Kwanza kabisa umefanya jambo la maana sana kughramikia matibabu ya Prof lakini labda tu nikwambie umeyasema hayo ktk wakati usio sahihi hata kidogo.

Profesa hana shida kiuchumi hivyo acheni kabisa kuingiza siasa ktk masuala ya msingi. Kuna watu wengi hasa kule Ikungi, Lyankoma, Simiyu wanahitaji matibabu na hawana usaidizi eti leo mnakuja hapa kutuambia kwamba mmeona mgharamikie kupunguza ugumu wa maisha kwa Profesa. Narudia acheni kucheza na maisha ya watanzania kisiasa.

Kama kumsaidia, anzeni kusaidia watu wasio na uwezo na wana magonjwa makubwa makubwa ila hawa wenye uwezo na profle mkitaka kufanya fanyeni kimya kimya. CCM mnakwama sana acheni siasa ktk masha ya watanzania.

Nimemaliza, naamini ujumbe utaupata dk hii hii.
 
Pongezi nyingi Kwa serikali.. wametumia busara nyingi hapa
 
Ummy anatafuta kiki kisiasa kwa kutumia mgonjwa ambae haitaj msaada wake. Alichofanya hakiswii kama angetaka kutoa msaada angeenda mwaisela uko na ocean load kuna wagonjwa hawajiwez hawana ata ndugu angewasaidia kimy kmya
 
Nchi ya laana yani kiongozi badala ya kupanga strategy ya kusaidia wengi wasiojiweza yeye anakimbilia kusaidia mtu maarufu ili apate kiki kisiasa. Hawa viongozi wetu wana uwezo mdogo sana wa kufikiri
 
Umeambiwa bure au kusaidiwa kama Prof J?? hakuna watu wanasaidiwa na serikali kwenye matibabu??
Bado upo usingizini, wangekua wanasaidiwa wangeshindwaje kulipia matibabu hadi maiti inadaiwa?
Mara nyingi tu maiti zinazuiliwa hapo Muhimbili sababu ya Deni. Acha upumbavu
 
Ummy kasema serikali itagharimia, siyo yeye.
na unavyokuwa unazungumzia wizara ya afya boss ni yeye,hivyo hayo kayasema kwa hisia zake kupitia mgongo wa serikali maana pesa yeye hana inatoka kwetu kwenda kumhudumia tajiri anaejiweza ni ujinga na upumbavu
 
Wewe mtu upo Tanzania hii kweli? Mtu mwenye shida ya matibabu akamuone diwani atasaidiwa?
Upo humuhumu Tanzania au?
Ni kweli hujui Kuna watu wengi wanakufa kwa kushindwa kumudu gharama?
 
Watu wa chini watafanya kimya Kwa MTU mkubwa kama profesa lazima watangaze Ili watu wajue coz ni sehemu ya siasa. After all hawajafanya vibaya
 
Huyo Umi unamlaumu bure tu, anatumwa, ni kama anayefukuza Wamasai analaumiwa Mkuu wa Wilaya au Polisi lkn wanashindwa kuelewa kwamba aliyefukuza Wamasai ni Raisi wenu Samia na siyo Mkuu wa Wilaya.

Hivyo Umi katumwa afanye alivyofanya, mna Kiongozi asiyejali chochote kuhusu maisha yenu isipokuwa power, atafanya chochote kwa ajili ya power !
 
Umeongea jambo la msingi sana.Inasikitisha sana kuona vijijini masikini wanakufa kwa kukosa msaada wakati huo watu wenye uwezo wakineemeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…