Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali
Michango isitishwe sasa
Maana kwenye vimedia uchwara
Naona watangazaji washaanza...
Kuwaomba watu watoe hela

Ova
Isitishwe>????? Wewe usitoe na hatuamini tu! hii ahadi ilitolewa wakati Tundu alipomininiwa gololi 38 matokeo yake??
 
Wanasiasa na fursa za kutafuta popularity.

Hapo hapo MNH kutakuwa na wagonjwa makapuku kwelikweli wanashindwa kufanya dialysis kwa kukosa tu fedha but no one will care,lakini kwa mtu maarufu huyu ambaye kashaanza kuomba michango kwa umma serikali inasema italipia full,so michango i-stop.
Michango iendelee mkuu!; kwani ilichangwa Kwa sababu Jay ni mtu maarufu au Kwa sababu ni binadamu au ilichangwa Kwa malengo yaliyojificha na Sasa watu wamekasirika kuwa malengo yao yamekwama?

Michango iendelee na wapewe hao wengine uliowaita makapuku. !!
 
Watanzania walivyo wapumbavu watashangilia na kuruka ruka huku wakibinua makalio kana kwamba waziri ametatua changamoto ya afya kitaifa.

Jiulize wewe, mtoto au mzazi au ndugu yako akiumwa atapata hiyo favour?au ni wale waliokula keki ya taifa wanaipata hiyo neema peke yao?

Tunahitaji kupaza sauti juu ya bima ya afya kwa kila raia wa Nchi hii. Ni heri tutumie fedha kuhudumia afya ya za wananchi wetu huku wakiwa wanapita kwenye barabara zenye foleni kuliko kuwapitisha kwenye flyover wakiwa ndani ya jeneza.
wewe ni nani hadi ututukane watu zaidi ya milioni 50 ni wapumbavu ?
 
Hiyo sio nongwa. Tatizo sio yeye kusaidiwa. Asaidiwe privately.

Ni discrimination kutumia pesa ya umma kumsaidia mtu mmoja ilhali watu wengine walio katika situation kama yake wakiachwa kujipigania wenyewe!
hili lipo toka enzi na enzi, hata kwa Mungu hakuna usawa,hata Yesu aliwahaidi pepo wale jamaa aliosurubiwa nao, utauliza kwanini wale aliwakubalia kuwa nao katika ufalme wa mbinguni huku akiacha wengine wajipiganie wao ?
hata Mungu alimsifu Ayubu,je watu wengine wangelalamika kwanini hajawasifu ?
 
Ummy,

Kwanza kabisa umefanya jambo la maana sana kughramikia matibabu ya Prof lakini labda tu nikwambie umeyasema hayo ktk wakati usio sahihi hata kidogo.

Profesa hana shida kiuchumi hivyo acheni kabisa kuingiza siasa ktk masuala ya msingi. Kuna watu wengi hasa kule Ikungi, Lyankoma, Simiyu wanahitaji matibabu na hawana usaidizi eti leo mnakuja hapa kutuambia kwamba mmeona mgharamikie kupunguza ugumu wa maisha kwa Profesa. Narudia acheni kucheza na maisha ya watanzania kisiasa.

Kama kumsaidia, anzeni kusaidia watu wasio na uwezo na wana magonjwa makubwa makubwa ila hawa wenye uwezo na profle mkitaka kufanya fanyeni kimya kimya. CCM mnakwama sana acheni siasa ktk masha ya watanzania.

Nimemaliza, naamini ujumbe utaupata dk hii hii.
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuanzia sasa Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule Profesa J anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi hapo atakaporuhusiwa kurudi nyumbani.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipofika Muhimbili leo kumjulia hali Msanii huyo.



Pia soma:
Tumuombee sana Profesa J
Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu
Pongezi nyingi Kwa serikali.. wametumia busara nyingi hapa
 
GEDC0286.jpg

Wawakilishi wa nchi kama hawa hawasaidiwi
 
Ummy anatafuta kiki kisiasa kwa kutumia mgonjwa ambae haitaj msaada wake. Alichofanya hakiswii kama angetaka kutoa msaada angeenda mwaisela uko na ocean load kuna wagonjwa hawajiwez hawana ata ndugu angewasaidia kimy kmya
 
Nchi ya laana yani kiongozi badala ya kupanga strategy ya kusaidia wengi wasiojiweza yeye anakimbilia kusaidia mtu maarufu ili apate kiki kisiasa. Hawa viongozi wetu wana uwezo mdogo sana wa kufikiri
 
Umeambiwa bure au kusaidiwa kama Prof J?? hakuna watu wanasaidiwa na serikali kwenye matibabu??
Bado upo usingizini, wangekua wanasaidiwa wangeshindwaje kulipia matibabu hadi maiti inadaiwa?
Mara nyingi tu maiti zinazuiliwa hapo Muhimbili sababu ya Deni. Acha upumbavu
 
Ummy kasema serikali itagharimia, siyo yeye.
na unavyokuwa unazungumzia wizara ya afya boss ni yeye,hivyo hayo kayasema kwa hisia zake kupitia mgongo wa serikali maana pesa yeye hana inatoka kwetu kwenda kumhudumia tajiri anaejiweza ni ujinga na upumbavu
 
Wewe uko wapi ?
Mbona wanatibiwa ! Na kama Hana Elfu kumi si akamuone hata Diwani wake wa CCM au Mtendaji ili aseme kuwa hawezi kulipa?

Ukumbuke kuwa Matibabu ya Jay. bila kumsaidia ujue atafilisika kabisa.

Matibabu madogo madogo watu wanapewa dawa na serikali Kwa kiwango kidogo Cha magonjwa madogo. Lakini magonjwa makubwa hasa magonjwa yanayotokana na tabia za kimaisha hua Matibabu yake ni ghali sana. Na Kwa Karne hii magonjwa yasiyoambukizwa / yanayotokana na hali ya kimaisha yanawakuta watu wengi sana.

Ndio maana hata Mabeberu hawajajitokeza Afrika kufadhili Matibabu ya magonjwa yatokanayo na tabia za kimaisha mana yanagharama kubwa sana.
Wewe mtu upo Tanzania hii kweli? Mtu mwenye shida ya matibabu akamuone diwani atasaidiwa?
Upo humuhumu Tanzania au?
Ni kweli hujui Kuna watu wengi wanakufa kwa kushindwa kumudu gharama?
 
Watu wa chini watafanya kimya Kwa MTU mkubwa kama profesa lazima watangaze Ili watu wajue coz ni sehemu ya siasa. After all hawajafanya vibaya
 
Huyo Umi unamlaumu bure tu, anatumwa, ni kama anayefukuza Wamasai analaumiwa Mkuu wa Wilaya au Polisi lkn wanashindwa kuelewa kwamba aliyefukuza Wamasai ni Raisi wenu Samia na siyo Mkuu wa Wilaya.

Hivyo Umi katumwa afanye alivyofanya, mna Kiongozi asiyejali chochote kuhusu maisha yenu isipokuwa power, atafanya chochote kwa ajili ya power !
 
Umeongea jambo la msingi sana.Inasikitisha sana kuona vijijini masikini wanakufa kwa kukosa msaada wakati huo watu wenye uwezo wakineemeka
 
Back
Top Bottom