Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali
Unapaswa utumie ubongo vizuri.
Prof Jay yupo Tz Muhimbili na kufika hapo kafuata hatua zote.
Lissu alienda Dodoma hospital na alitibiwa vizuri tu, serikali ikashauri ahamishiwe Muhimbili kwa matibabu zaidi, Kama kawaida hoyahoya wa chadema wakakataa wakamkimbiza Nairobi, na wakampeleka tena ubelgiji.
Sasa hapo utailaumu serikali?
Mfano hata huyi Prof jay angeenda kutibiwa Marekani unafikiri serikali ingekuwa na mpango nae?
Soma vizuri ukiona nilipo laumu unitag.
 
hii sio sawa, anatibiwa kama nani..

gharama za wagonjwa wengine hapo muhimbili wasio na mbele wala nyuma nazo Serikali itazibeba? tuwe serious kidogo.

Hao wengine serekali haiwezi kupata kick. Ule mpango wa bima ya afya kwa kila mwananchi umeishia wapi? Au bi utapeli as usual?
 
Gharama za matibabu ya Mh. Lissu mtatoa ama hamtoai?

Haya yapo kisheria wala si hisani yenu nyie wana Lumumba.
 
Pamoja na kuwa mbunge wa upinzani hakuwa mtu wa mihemko kama kina rema kina msingwa, alifanya anachoona kina maslahi kwa taifa ndio maaana Leo hii Kila mtu unaona anasupport Kila kitu kinachosemwa kuhusu kupigania afya yake.

Siasa si uadui
 
Pamoja na kuwa mbunge wa upinzani hakuwa mtu wa mihemko kama kina rema kina msingwa, alifanya anachoona kina maslahi kwa taifa ndio maaana Leo hii Kila mtu unaona anasupport Kila kitu kinachosemwa kuhusu kupigania afya yake.

Siasa si uadui
Chadema wala familia ya J haikushindwa kumtibu mtu wao , Kujichomeka kwa serikali ili ipate huruma ya wananchi kusikupumbaze .

Tumenyamaza kwa sababu maalum
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuanzia sasa Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule Profesa J anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi hapo atakaporuhusiwa kurudi nyumbani.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipofika Muhimbili leo kumjulia hali Msanii huyo.



Pia soma:
Tumuombee sana Profesa J
Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu
Kamanda mnyenyekevu sana akiwa bungeni aliongea kwa busara na hekima muda wote, upone haraka comrade
 
Hii baada ya Chadema kutangaza kuwa wamekusanya milioni 15 kwa ajili ya tiba yake? Ninawashauri wasiziguse kwa kuzingatia yakiyompata mbunge wao mwingine ambae Ummy aliahidi kuwa serikali itagharamia matibabu yake kokote duniani.

Amandla...
 
Ni muda wa wasanii chipukuzi kujua kuwekeza.

Kwamba Haule ameshindwa kuwekeza kwenyw afya?

Ameshindwa hata Silver plan ya bima achilia gold plan.

Hadi napata ukakasi nini kinachomsumbia hadi serikali iingie kati kulipia matibabu yake.
 
Mara nyingi kwa Research yangu wagonjwa mahututi ambao selikali iliwahi kuingilia kati na kuwatibu kwa gharama za selikali Waliishia kufa.. Bora tu wangeachwa watu Wachange..
 
Jambo lililo jema zaidi ni kutowasahau na Watanzania wengine wasio na majina/ maarufu.

Au wao sawa tu wakiachwa wajigharamie matibabu yao wenyewe?
Kila mmoja ashinde mechi zake, waambie ba wao wapambane wawe maarufu.
 
Prof. Jay ni tone tu kwa mamilioni wanaohitaji msaada wa matibabu angalau ya panado, serikali isijifiche kwenye kichaka cha kugharimia matibabu ya mbunge mstaafu badala ya kuboresha huduma za afya na kuzifanya kuwa nafuu kwa wote.......haingii akilini hospitali ya muhimbili kutoza bei kubwa za matibabu na vipimo huku tukijua kwamba ni hospitali ya umma ambapo vifaa na wataalamu wanalipwa na serikali kwa kodi za wananchi.
 
Watanzania walivyo wapumbavu watashangilia na kuruka ruka huku wakibinua makalio kana kwamba waziri ametatua changamoto ya afya kitaifa.

Jiulize wewe, mtoto au mzazi au ndugu yako akiumwa atapata hiyo favour?au ni wale waliokula keki ya taifa wanaipata hiyo neema peke yao?

Tunahitaji kupaza sauti juu ya bima ya afya kwa kila raia wa Nchi hii. Ni heri tutumie fedha kuhudumia afya ya za wananchi wetu huku wakiwa wanapita kwenye barabara zenye foleni kuliko kuwapitisha kwenye flyover wakiwa ndani ya jeneza.
ujumbe mzito sana huu
 
Back
Top Bottom