Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?
Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?
Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.
Nchi hii imebadilika sana.
Tangu watawala wa CCM wagawane Mali za umma na kujiwekea mishahara na mafao makubwa na kujilimbikizia Mali ,Watanzania wamekua na roho mbaya sana .
Watu wanaombeana na kutakiana mabaya tu Kwa sababu ya tofauti za kisiasa.
Shetani inaonekana amefanikiwa kuweka Ubalozi Tanzania.
Prof. Jay alitumikia Taifa hili Kwa uamunifu mkubwa .
Mama Samia Kwa Upendo wake na utu wake ameamua kufanya jambo jema tofauti na awamu zilizopita waliokua wanamtaja Mwenyezi Mungu midomoni mwao ila nafsini mwao walikua watu waovu wakubwa.
Kwa Mwislam yeyote matendo kama hayo ni Ibada na thawabu Kwa Mwenyezi Mungu.
Lakini Kwa wanaoweka Siasa mbele na umaarufu wa kishetani kwao ni kupinga tu .
Rais ana mafungu Mengi sana. Kwa wale Marais wenye Imani zisizokataza ukevi na ufuska anaweza akatumia tu mabilion ya pesa Kununua pombe Kali na za bei kubwa kutoka Ulaya ,huku akiwa anabadlisha nyumba ndogo.
Tanzania awamu ya SITA tumebahatika kumpata Rais mcha Mungu wa kweli.
Anayejua maana ya kumwogopa Mungu na kuwatumikia watu huku akijua kuna kuulizwa kesho ahera, lakini Cha ajabu Bado watu wanapinga mpaka matendo mema ya huruma.
Ama kweli wahenga walisema " Tenda mema uende zako usisubiri shukrani" . Na wengine wakasema " Shukrani ya Punda ni Mateke."
Watanzania Itatuchukua miaka mingi sana Kuja kupata Rais kama Mh. Samia Suluhu kupitia CCM ,Chama kilichojaa watu katili kimfumo na wanye kuweka mbele maslahi Kwa namna yoyote.
Tumempata Mama hasa tushukuru Mungu. Tungelimia meno. Mwenyezi Mungu ni mkubwa kutuletea Mh. Samia.
.Tuacha Roho Mbaya.