Unadhani kwanini Tanzania hii, safu ya matajiri imetawaliwa na waajemi?

That’s my mom😩
Hakupi mia mbovu!
Anakwambia mimi nilipambana nikapata kwahiyo na wewe tafuta chako😆
 
That’s my mom😩
Hakupi mia mbovu!
Anakwambia mimi nilipambana nikapata kwahiyo na wewe tafuta chako😆
Cold hearted mom. Hanaga shida ya kutaka kusaidiwa?
 
Mkuu,nimemaanisha kwamba wao wanasomesha watoto wao shule na vyuo vizuri ili baadae waje kuendeleza vitu vya familia wakiwa na maarifa zaidi ya kuinua biashara za wazazi wao pale walipozikuta. Niliowatolea mfano wote wamesomeshwa nje ,wakapata elimu iliyosaidia kuinua biashara za wazazi wao kuzipeleka mbele zaidi ya zilipokuwa.
Je sisi matajiri wetu wanawapa watoto wao elimu bora ili waje waendeleze pale wazazi wao walipoishia? Siongelei kijana anaetoka familia maskini ambaye yeye ndio anaanza,shida yetu sisi ni kuwa utajiri hauvuki kwenda kizazi kijacho,kila kizazi kinaanza from zero,wao baba akianza from zero,mwanae haanzii from zero.
 
Subiria urithi hapo! Ana mawazo ya kibepari au masharti 😀
Ni mkoloni tu hakuna nini wala nini, pia wasukuma wana ile mwanamke ataolewa kwahiyo yuko busy na madogo ni wa kiume tupu!
 
Huwezi amini mama yangu huwa ananiambia hivi, eti ukitesekea unafanikiwa, Mungu anakuona!
 
Dahh umenikumbusha kuna mabasi yamepakiwa mpaka yameharibika pale Mwanza, walimuua mmiliki sasa hawataki yafanye kazi mpaka wagawane, kama wangelikuwa na akili timamu unakubali ata bus moja tu mengine waachie unataka kuniambia asingerudisha pesa nyingi kutokana na hiyo biashara? Ila tamaa ndio inatangulizwa kuliko akili!
 
Tusisahau, wanatumia sana rushwa pia.

Huyo Myemeni alitoa bilioni kumi mchana kweupe Mlimani City kuchangia kampeni ya Samia. Chochote anachotaka sasa hv anapata. Ukikataa kuondoa kodi ambayo hakubaliani nayo unaondoka wewe TRA. Samia alimfuta kazi kamishna wa TRA ambae alikataa rushwa iliyoletwa ofisini. Anakwamisha madili ya watu. Mnakumbuka ???

Hawa Wa Asia wanamiliki serikali pia.
 
Kwamba tuwapeleke watoto wetu ist? Unajua kama chekechea tu ada ni 30m?
 
Mbona wengi wanapelekwa shule za international na wanasoma nje pia!
 
Private interest! Ambayo kwa lugha ya kawaida ni selfishnes. Ni vigum sana jambo moja liendeshwe na watu wengi kwa common interest Afrika. Ngum mnooo, mm pia shuhuda wa hili. Bora tukose wote kuliko tufanye kwa faida ya wote
 
 
Mifumo Mibovu ya NCHI ,
Badala ya kutafuta…. Sisi tunapiga mudomo

Hatupendani, hatuaminiani, tunapiga sana njumu na majungu. Na mbaya zaidi tuko busy kufurahia maanguko yetu

We need to change
 
Bakhresa anakopeshwa Sana na world bank, ni rahisi kwa haya mashirika makubwa kukukopesha kama Una Shea faida yako na wananchi. Like world bank hawawezi kukukopesha then Ile hela ukawekeze kwenye hisa ama ukanunue Vodacom na Tigo ufaidike wewe, ila watakupa hela kama biashara yako inaweza toa maelfu kwenye umasikini na vifananiavyo.

Mfano biashara ya Bakhresa ya Ice cream wakati inaanza ilikua ni pasu kwa pasu MTU akiuza ice cream 500 anachukua 250 na Bakhresa 250, ukienda omba mkopo wa baiskeli na distribution logistics nyengine kama madeli ni rahisi kupata sababu moja kwa moja inamgusa masikini wa Chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…