Pre GE2025 Upendo Peneza aeleza sababu za kuondoka kwake CHADEMA

Pre GE2025 Upendo Peneza aeleza sababu za kuondoka kwake CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Amesema kuhusu pesa walizokuwa wanachangishwa wao kama wabunge, hawafahamu zimetumika kufanya Nini. Na ni kweli hizi pesa zimekuwa zikitolewa porojo. Huyu Upendo kwakuwa ana hasira ataongea mengi ya hasira, lakini humo ndani tutapata ukweli.
Matumizi ya pesa za Chadema zinakaguliwa na CAG, kama kuna sintofahamu anawataka watoe maelezo. Amezungumzia michango ya 400000 kwa kila mbunge kwa ajili ya familia ya Marehemu Mawazon ambazo anadai hazikufikishwa. Shida ni kuwa amechelewa mno kutoa tuhma hizi ( hata kwenye mahojiano kazipenyeza mwishoni).

Amandla....
 
Kisiasa, Upendi amedata mapema sana.

Au pengine alikuwa hana kitu kuanzia mwanzoni zaidi ya mvuto wa ile sura ya kitusi na coaching za marehemu Alphonce Mawazo
 
Upendo amewalaumu Chadema kwa kutopigania kesi ya wakina Halima. Anasahau kuwa chama chake ndicho kinachowakingia kifua.
Amezungumzia Mbowe kuwakaribisha wakina Halima kwenye shughuli ya Kanisa Moshi. Amesema hiyo ni ishara ya mtu asiyekuwa na msimamo thabiti. Amesahau kuwa Mbowe alikaa ndani lakini alipotoka alienda kunywa chai na Mkuu wa Dola. Amezungumzia magumu aliyopitia katika uchaguzi uliopita bila kuwataja waliomsababishia maumivu yake.
Upendo ana personal ambitions zake ( sio dhambi) na anataka kupitia njia za waliomtangulia kwa kukichafua chama chake cha zamani. Anasikitisha sana.

Amandla...
 
Upendo amewalaumu Chadema kwa kutopigania wakina Halima. Anasahau kuwa chama chake ndicho kinachowakingia kifua.
Amezungumzia Mbowe kuwakaribisha wakina Halima kwenye shughuli ya Kanisa Moshi. Amesema hiyo ni ishara ya mtu asiyekuwa na msimamo thabiti. Amesahau kuwa Mbowe alikaa ndani lakini alipotoka alienda kunywa chai na Mkuu wa Dola. Amezungumzia magumu aliyopitia katika uchaguzi uliopita bila kuwataja waliomsababishia maumivu yake.
Upendo ana personal ambitions zake ( sio dhambi) na anataka kupitia njia za waliomtangulia kwa kukichafua chama chake cha zamani. Anasikitisha sana.

Amandla...
kila anaye toka cdm wamama huwa wanatoa machungu mengi waliyopitia inawezekana mbowe anawafanyia mabaya sana hawa kina mama
 
Wewe jamaa umelishwa bangi ya wapi. Yaani mtu akiongea kitu kuhusu mtu usiyemkubali basi automatically kinakuwa cha kweli. Inawezekana na wewe ndio wale wale wa Da Mange kasema.
Mkuu zingatia neno baadhi ya asemayo. Hakuna popote ninaposema akiongea chochote automatically kinakuwa kweli. Nina utambuzi wa kutosha, naweza kukisia ukweli unaosemwa uko kwa kiwango gani, na yapi ni maneno ya kusaka cheo.

Kama ni huyo Mbowe sijaanza kusema leo hastahili kuendelea tena kuwa mwenyekiti wa cdm bada ya Upendo kuongea, bali nilianza kusema hivyo mara tu baada ya ujio wa Lowassa ndani ya cdm, na kupewa nafasi adhimu ya kugombea urais kwa njia ya vodafasta.
 
Kwamba inawezekanaje akina Mdee wamsifie sana mwenyekiti wao kuhusu wao kuwepo bungeni? Cha kushangaza Hadi Mbowe ameonekana na Mdee wakigonga cheers kwenye sherehe fulani. Isitoshe Mbowe kafikia mahali pa kuwaalika akina Mdee kwenye harambee ya kanisa huko kwao Machame. Pia namna kesi ya kina Mdee inavyoendeshwa huko mahakamani ni kama cdm haiko serious na kesi hiyo.
Kwani siasa Ni vita au Uadui?
 
Mmmmmh!Kuamini ni ukweli mwingi ni hadi kuwe na uthibitisho.Mpaka sasa naamini kweli anaongea na si anaongea ukweli.Uthibitisho?
Anasema kiasi Cha 5b+ walichokuwa wanachangishwa kwa ajili ya kusaidia wagombea kwenye uchaguzi wa 2020 hakikupelekwa kwa wagombea wa uchaguzi hiyo 2020. Na kama hizo hela zingekuwepo Bado, basi wakati chama kimegomea ruzuku zingetumika kuendesha chama. Hapa unahitaji udhibitisho gani?
 
kila anaye toka cdm wamama huwa wanatoa machungu mengi waliyopitia inawezekana mbowe anawafanyia mabaya sana hawa kina mama
Hajasema lolote kuhusu kufanyiwa ubaya na Mbowe. Anamtuhumu kuwa hayuko serious kwenye suala la wakina Halima. Pengine anataka kuamini kuwa kuna mahusiano kati yao maana amezungumzia sifa ambazo Halima alimmwagia wakati ana apishwa kuwa mbunge. Aidha, kumkaribisha kwenye sherehe baada ya Halima kusema maneno ya ovyo dhidi yake.

Amandla...
 
Anasema kiasi Cha 5b+ walichokuwa wanachangishwa kwa ajili ya kusaidia wagombea kwenye uchaguzi wa 2020 hakikupelekwa kwa wagombea wa uchaguzi hiyo 2020. Na kama hizo hela zingekuwepo Bado, basi wakati chama kimegomea ruzuku zingetumika kuendesha chama. Hapa unahitaji udhibitisho gani?
Aje na risiti ya salio anzia hadi ishia tuwe tunafanya mlinganyo sahili.
 
Anasema kiasi Cha 5b+ walichokuwa wanachangishwa kwa ajili ya kusaidia wagombea kwenye uchaguzi wa 2020 hakikupelekwa kwa wagombea wa uchaguzi hiyo 2020. Na kama hizo hela zingekuwepo Bado, basi wakati chama kimegomea ruzuku zingetumika kuendesha chama. Hapa unahitaji udhibitisho gani?
Lijualikali alisema ana ushahidi wa jinsi viongozi wa Chadema wanavyofuja mali za Chadema. Takukuru wakasema kuwa watafuatilia. Wangapi wamekamatwa kwa tuhuma hizo? Upendo amesema bila kutoa ushahidi. Na kaichomekea mwisho kabisa baada ya kuambiwa majibu yake hayatoshelezi.

Mkuu achana na Takukuru, hiyo sio taasisi unayoitegemea kufanya lolote la weledi
 
Dada anafunguka vibaya huko clouds FM kuhusu mambo ya cdm. Anamuanika Mbowe hadharani.

Hao wapo kwenye project ,kukikaribia uchaguzi ,kamati ya propaganda ya "sisiemu" inarecruit "makalai" aka ng'ombe wasio na mkia kwa ajili ya kuichafua CDM....Nashangaa hadi Marcosy nae ameingia kwenye mtego ,tatizo ukiwa na biashara ukawa mpinzani lazima watakufirisi nahisi Dr Marcosy kaogopa biashara yake ya Maji JIBU kufa.
 
Kuiponda cdm hadharani ni nguzo kuu ya kupata cheo ghafla ndani ya ccm. Na cheo kinasogea haraka sana iwapo Kuna ukweli Fulani utaongea ambao utaibeba ccm, au kuharibu haiba ya cdm.
Alichoongea Peneza ni upuuzi mtupu. Kwa mfano kasema kuwa alikuwa mdogo na CHADEMA walikuwa hawampi nafasi ya kwenda naye kwenye mikutano ya operesheni Sangara ila akawa anafosi hadi kwenda huko kwa kujilipia mwenyewe. Kimsingi unaona hapo CHADEMA hawakuwa na kosa kubebabana na binti mdogo kwenye harakati zao ambaye anatakiwa awe chini ya uangalizi wa wazazi. Peneza anadhihirisha tabia yake mbovu aliyokuwa nayo kwa muda mrefu. Mimi ni mwanaCCM damu ila Peneza hana maadili kabisa.
 
Back
Top Bottom