UTEUZI: Amos Makalla ahamishiwa Mwanza, Chalamila apelekwa Dar
Hivi hamuwazi vitu vingine zaidi ya huu umaskini?!!!!!! Inaboa mno sometimes.
failed state,kwamba tusifu utendaji uliotukuka? au amehamishwa kwa sababu ya uchapakazi bora? badilika zama za watz mapunguani zilipita tunajua mbivu na mbichi.
N.B:Inaboa mnoo kuona taifa linawatu machawa kama wewe!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:

1. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

2. Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

3. Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

4. Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.

AAEB0FC1-3EE6-45A4-A0FB-B04D4F069033.jpeg

KUHUSU MAKALLA

Makalla alishawahi kushika nafasi ya katibu wa uchumi na fedha wa CCM na aliwahi kukaimu nafasi ya katibu wa umoja wa vijana wa CCM ( UVCCM).

Pia. Amewahi kuwa mbunge wa Mvomero kwa vipindi tofauti na mara ya mwisho alikuwa mbunge mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Makalla pia, amewahi kuwa naibu waziri wa habari enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kisha kuhamishiwa Mkoa wa Mbeya kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Katavi.

Mei 14, 2019 Hayati John Magufuli alitengua uteuzi wake akiwa mkoani Katavi.

Mei 15, 2021, Rais Samia alimteua Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam

Pia, soma: Rais Samia, tuondolee huyu RC Amos Makalla mkoa wa Dar es Salaam

KUHUSU CHALAMILA

Chalamila aliteuliwa Rais Samia kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mei 15, 2021 akitokea Mbeya alikodumu kwa takribani miaka minne tangu Julai 29, 2018 alipoteuliwa na Hayati Dk John Magufuli.

Baadaye uteuzi wake wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ulitenguliwa na raia Samia na kukaa nje kwa siku 412 hadi Julai 28, 2022 alipoteuliwa tena na rais Samia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Kabla ya hapo Chalamila alikuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, wadhifa alioupata Desemba 5, 2017 baada ya kushinda katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Kabla ya kuibukia katika siasa, Chalamila alikuwa mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Tumaini mkoani Iringa na amewahi kuwa mwalimu katika shule mbalimbali.
Clearly, My Mother is fumbling around!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:

1. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

2. Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

3. Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

4. Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.
View attachment 2623197

KUHUSU MAKALLA

Makalla alishawahi kushika nafasi ya katibu wa uchumi na fedha wa CCM na aliwahi kukaimu nafasi ya katibu wa umoja wa vijana wa CCM ( UVCCM).

Pia. Amewahi kuwa mbunge wa Mvomero kwa vipindi tofauti na mara ya mwisho alikuwa mbunge mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Makalla pia, amewahi kuwa naibu waziri wa habari enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kisha kuhamishiwa Mkoa wa Mbeya kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Katavi.

Mei 14, 2019 Hayati John Magufuli alitengua uteuzi wake akiwa mkoani Katavi.

Mei 15, 2021, Rais Samia alimteua Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam.

Amos Makalla amehamishwa Dar wakati mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo ukiendelea.

Pia, soma: Rais Samia, tuondolee huyu RC Amos Makalla mkoa wa Dar es Salaam

KUHUSU CHALAMILA

Chalamila aliteuliwa Rais Samia kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mei 15, 2021 akitokea Mbeya alikodumu kwa takribani miaka minne tangu Julai 29, 2018 alipoteuliwa na Hayati Dk John Magufuli.

Baadaye uteuzi wake wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ulitenguliwa na raia Samia na kukaa nje kwa siku 412 hadi Julai 28, 2022 alipoteuliwa tena na rais Samia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Kabla ya hapo Chalamila alikuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, wadhifa alioupata Desemba 5, 2017 baada ya kushinda katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Kabla ya kuibukia katika siasa, Chalamila alikuwa mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Tumaini mkoani Iringa na amewahi kuwa mwalimu katika shule mbalimbali.
ivi huyu si ndio alisema bebeni mabango hata ya mat***toasi njooni nayo au, halafu akantenguliwa sasa sijui alirudishwa kwanini
 
Makalla tulijua Dar haimtoshi, baada ya kushindwa kutatua changamoto ya wafanya biashara na TRA.
Kawekewa msuli mixa upaja kaufyata mkia, bi mkubwa kaona huyu ngoja tumtafutie pengine hapa hapawezi panahitaji mtu mtu kweli mtu na Nusu si maskhala na Dar tukigoma tumegoma, kafanya sub faster anatoka Makalla anaingia Chalamila Ila aangalie tu Dar Ina mengi na yeye asije akachomolewa mda si mrefu
 
failed state,kwamba tusifu utendaji uliotukuka? au amehamishwa kwa sababu ya uchapakazi bora? badilika zama za watz mapunguani zilipita tunajua mbivu na mbichi.
N.B:Inaboa mnoo kuona taifa linawatu machawa kama wewe!
Kwani mi nimesifia nn ndugu hadi uniite chawa?!!!!! Sijasema lolote kama hayo mabadiliko yako sawa au hayako sawa. Nilikuwa nashangaa tu, katika mengi ambayo ungeweza kutolea maoni uamuzi huo (kusifia au kuponda) iweje unawaza habari ya watu kufaidi keki ya taifa tu?!!!! Ungeweza kutuambia unafikiri nani anafaa hapo dar n.k
 
Chalmila alienda Kagera Kwa mikwara, jambo la kwanza ilikuwa kuwananga Wahaya mwanzo mwisho...akajinasibu sana kuunyosha mkoa akahaidi mambo kibao, ila mpaka Sasa sijui ametoka amefanikisha mangapi...Mungu amtangulie Huko aendako.
 
Chalamila kaja DSM tuinjoi mbwembwe zake
Ndiyo maana mimi huwa nasema Tanzania itazidi kudidimia. Huyu ni mtu mzima hajui kuwa uongozi bora ni muhimu kwenye maisha yake. Anaona mbwembwe ndiyo muhimu tena kabisa anasema tu-enjoy! Ni elimu yetu inazalisha mindset za aina hii? Siku utakapojitambua kuwa hukutaka ku-enjoy mbwembwe za viongozi bali kuwa serious na kuwasimamia wawajibike utakuwa umeshachelewa.
 
Back
Top Bottom