Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dangote alivyoanza oparesheni simenti alikua anauza elfu 7 kwa mfuko, hiyo ilikuwa ni Dar mwaka 2016, ila makampuni yaliyokuwepo tayari yakashinikiza kuwa bei ipande na kuwa elfu 11 kama wanavyouza wao, ikabidi Dangote afuate nyayo zao.Mmh! Hata kwenye gesi ya Mtwara tuliambiwa sasa Mtwara itakuwa kama NewYork na umeme utakuwa bure kama mwanga wa jua.
Wakati kiwanda cha Dangote kinajengwa, tuliambiwa bei ya sementi itapungua na kuwa sh elfu 5.
Lakini Sasa yako wapi??
Dada acha ujinga. Unafikiri wale Tec waliongea kwa ajili yao? Hujui kwamba hata watoto wa kuendeleza majina yao hawapo? Sio kwa vile either raisi ni di i yako ndo anawazia mema watu au kwa vile ni dini tofauti basi anatuwazia mabaya. Nilimpinga Magu kwa baadhi ya sera zake na si kwa sababu ni mkristo mwenzangu. Naona wewe umeweka dini mbele kama kibatari cha kumuunga mkono mtu.TEC mashavu yamewashuka kwakununa, nyuzo zao leo utafikiri soksi zilizojaa tope. Zimewashuka shuu.
Acha tuHii siku nilikuwa nnaingoja kwa hamu na shauku kubwa sana.
Waende wakajinyonge tu hamna namna! Mama Samia hoyee!!Tec wamefura kwa hasira
Hawa member wa "Rainbow society" wana shida kweli.Mdude na Mwakibusi wapo live 🤣
NDIO maana wakamrudisha Makonda Ili aweze kupiga kelele vizuriKwa ujumla na kipekee kabisa, Rais Samia ameshukuru watanzania wote waliotoa maoni kwani linapokuja jambo jipya ni lazima watu wawe na maoni tofauti.
Roma ikisema imekwisha....hebu andika huu msemo kea kilatiniCha msingi mama yako amesikiliza maoni ya wannchi na TEC kama kutoka milele hadi 30 sio mbaya kabisa
Una ulivyo mpumbavu sasaHawa member wa "Rainbow society" wana shida kweli.
#TUSONGE_MBELE!
Hi
Hivi huyu Mama bado anaendelea na upuuzi wake wa kuuza Bandari kwa DP World!
Kea hiyo mkataba wa mwanzo ikisema miaka mia au milele!?.. mia na milele ni kitu kilekile!?Mimi namsikiliza mkurugenzi wa TPA na tunaamini anachokisema ni kweli kuwa wamesikiliza maoni ya watu ..sasa ni miaka 30 sio mia au milele…lakini bado tutakuwa na shauku ya kuona hayo marekebisho!
Kwenye hili TEC,Chadema,Slaa,Mdude na Mwambukusi wanastahili kupongezwa sana
Sio tumuelekeze inakouzwa sumu ya panya?Mliopo karibu na kale kabibi Maria sarungi mshikilieni anaweza kujiua leo tusipoangalia.
Na tec si loloteHiyo imeenda.
TEC wanangoja kwenye Ballot ili kuwatia adabu CCMNa tec si lolote
Fuatilia yanayojiri kutoka Ikulu kwenye Halfa ya utiaji saini wa Mikataba mahsusi 3 ya uwekezaji Bandari ya Dar es salaam, leo Oktoba 22, 2023.
View: https://www.youtube.com/live/N6izYMjIOaI?si=O_YQZdZcwAOJWWpD
MKURUGENZI MKUU WA TPA, PLASDUCE MKELI MBOSSA
Uwekezaji huu wa Serikali kupitia TPA utaongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka, kuongezeka kwa mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.
Aidha, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.
Haitegemewi kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini.
Aidha, Mkeli Mbossa amefafanua kuwa wastani wa meli kukaa nangani ikisubiri huduma ni siku 5 hadi 10 huku bandari ya Mombasa ni siku 1.25 na Bandari ya Durban ikiwa ni wastani wa siku 1.6. Hii inatokana na kukosekana kwa uwekezaji mkubwa wa muda mrefu ambao ungepelekea kuongezeka kwa namba za gati. Pia, gharama za kusafirisha makasha ni kubwa, jambo linalofanya kupanda kwa bei ya bidhaa kwa mtumiaji wa mwisho.
Mikataba inayosainiwa leo ni baina ya Nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4-7 lakini pia kutakuwa na sehemu ambayo gati 0-3 zitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TPA na kampuni ya DP World kwa shughuli za kibiashara na shughuli za kiserikali.
Mikataba hii haihusishi eneo lote la bandari wala bandari zingine za Tanzania. Upande wa gati namba 8-11, mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine umeshaanza kufanyika na akipatikana mwekezaji mwingine mwenye sifa atakabidhiwa na sio DP World.
Katika mikataba hii, Serikali itakuwa inapata ada na tozo kutoka DPW ambazo zitaongeza mapato na kupunguza gharama za uendeshaji.
Mkataba huu utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wa DPW utakuwa unapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100. Watumishi wa sasa wa TPA watakuwa na nafasi ya kuchagua kubaki TPA au kuhamia kampuni ya DPW.
Pia, mwekezaji atalipa kodi zote za Tanzania kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, sheria za Tanzania ndio zitatumika katika kutekeleza mkataba huu na serikali itakuwa na haki ya kujiondoa kwenye mkataba ikiona inafaa.
SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIARais Samia amesema haikuwa rahisi kufikia makubaliano haya lakini walisikiliza na kufuatilia maoni na hoja za kila mtu hivyo hakuna kundi au sauti ambayo imepuuzwa ambao Serikali iliunda jopo la wataalam kufuatilia maoni hayo.
Kwa ujumla na kipekee kabisa, Rais Samia ameshukuru watanzania wote waliotoa maoni kwani linapokuja jambo jipya ni lazima watu wawe na maoni tofauti.
Amewakaribisha watu wengi zaidi kuja kuwekeza Tanzania ili kuinua uchumi na kupunguza umaskini wa watu.
Mawazo ya wawekezaji wa ndani kupewa bandari ni mazuri na ya kizalendo lakini yapo mbali na uhalisia. Katika kusiani mkataba huu, maslahi mapana ya nchi yamezingatia maslahi mapana ya nchi.