Utiaji saini Mkataba wa Tanzania na DP World: Mkataba utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wake utapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100
Pamoja na kelele zote za watanganyika kuhusu bandari yao kuuziwa mwarabu, bado serikali inayoongozws na rais Samia imepuuza na kuwapa bandari warabu wa DP World.

View attachment 2789020

Leo mikataba 3 ya DP World inasainiwa rasmi.
Hii Haina tofauti na kelele za chanjo ya uviko kuwafanya mazombie 😁😁
 
Fuatilia yanayojiri kutoka Ikulu kwenye Halfa ya utiaji saini wa Mikataba mahsusi 3 ya uwekezaji Bandari ya Dar es salaam, leo Oktoba 22, 2023.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa amesema uwekezaji huu wa Serikali kupitia TPA utaongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka, kuongezeka kwa mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.

Aidha, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.

Haitegemewi kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini.

Aidha, Mkeli Mbossa amefafanua kuwa wastani wa meli kukaa nangani ikisubiri huduma ni siku 5 hadi 10 huku bandari ya Mombasa ni siku 1.25 na Bandari ya Durban ikiwa ni wastani wa siku 1.6. Hii inatokana na kukosekana kwa uwekezaji mkubwa wa muda mrefu ambao ungepelekea kuongezeka kwa namba za gati. Pia, gharama za kusafirisha makasha ni kubwa, jambo linalofanya kupanda kwa bei ya bidhaa kwa mtumiaji wa mwisho.

Mikataba inayosainiwa leo ni baina ya Nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4-7 lakini pia kutakuwa na sehemu ambayo gati 0-3 zitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TPA na kampuni ya DP World kwa shughuli za kibiashara na shughuli za kiserikali.

Mikataba hii haihusishi eneo lote la bandari wala bandari zingine za Tanzania. Upande wa gati namba 8-11, mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine umeshaanza kufanyika na akipatikana mwekezaji mwingine mwenye sifa atakabidhiwa na sio DP World.

Waarabu ni watu wema sana, juzi El Shanawary alipoumia na kupatiwa matibabu pale uwanjani, , Chama aliomba maji na juisi na kuonyeshwa upendo mkubwa sana na Waarabu:
Nawashangaa watanzania wanao shobokea Wazungu badala ya waarabu: Kuna watu nawapenda mpaka wanavyo ongea ni kama kiarabu flani, wanavaa na kaznu na vikofia ilimradi tu wafananie uarabu.
 
Fuatilia yanayojiri kutoka Ikulu kwenye Halfa ya utiaji saini wa Mikataba mahsusi 3 ya uwekezaji Bandari ya Dar es salaam, leo Oktoba 22, 2023.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa amesema uwekezaji huu wa Serikali kupitia TPA utaongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka, kuongezeka kwa mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.

Aidha, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.

Haitegemewi kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini.

Aidha, Mkeli Mbossa amefafanua kuwa wastani wa meli kukaa nangani ikisubiri huduma ni siku 5 hadi 10 huku bandari ya Mombasa ni siku 1.25 na Bandari ya Durban ikiwa ni wastani wa siku 1.6. Hii inatokana na kukosekana kwa uwekezaji mkubwa wa muda mrefu ambao ungepelekea kuongezeka kwa namba za gati. Pia, gharama za kusafirisha makasha ni kubwa, jambo linalofanya kupanda kwa bei ya bidhaa kwa mtumiaji wa mwisho.

Mikataba inayosainiwa leo ni baina ya Nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4-7 lakini pia kutakuwa na sehemu ambayo gati 0-3 zitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TPA na kampuni ya DP World kwa shughuli za kibiashara na shughuli za kiserikali.

Mikataba hii haihusishi eneo lote la bandari wala bandari zingine za Tanzania. Upande wa gati namba 8-11, mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine umeshaanza kufanyika na akipatikana mwekezaji mwingine mwenye sifa atakabidhiwa na sio DP World.

Katika mikataba hii, Serikali itakuwa inapata ada na tozo kutoka DPW ambazo zitaongeza mapato na kupunguza gharama za uendeshaji.

Mkataba huu utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wa DPW utakuwa unapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100.

Mbona Miaka michache sana?
 
Tanzania inaelekewa kuwa ni "logistics solution" ya Afrika.

Nna uhakai huko mbeleni tutakuwa kitovu cha biashara kikubwa katika Afrika, lakini kwa leo tutazame tunayoyakabili sasa hivi.

Tunataka kujenga banadari kavu katika mipaka yote ya Tanzania.

Mazao yote ya Tanzania sasa yatakuwa kwenye soko la dunia kwa jina la Tanzania.

Hayo ni maneno ya Mwenyekiti wa DP World.

Sisi siyo bandari tu, sisi ni kituo cha UStawi wa Tanzania.
Mwenye upeo anaelewa hayo maneno yanamaanisha kitu gani, asiye na upeo atakuita chawa.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema kuwa mkataba wa DP World wa uendelezaji na uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam ni wa miaka 30 na utendaji kazi wa DP World utakuwa ukipimwa kila baada ya miaka mitano.✍️
 
Back
Top Bottom