Hakyamungu Chuma kimetua, jamani MUNGU yupo, muuaji anajisikia vibaya sana saa hii, analia machozi na mda wowote mshtuko wa moyo unaweza mpata.

Acheni Mungu aitwe Mungu, loh, kuanzia leo naanza kusadiki Mungu yupo, anaishi!
Amina
 
Kumekuwa na watu wakijifanya wana huruma eti wanawaonya watu wasiende kumpokea Lissu kwasababu watapigwa na askari. Wengine wanatumia msiba wa mzee Mkapa kama kisingizio.

Binafsi namuheshimu sana mzee Mkapa, mungu amlaze pema. Lakini haya mapokezi hayataathiri msiba kwa aina yeyote. Pia ieleweke Lissu ni mtu maarufu aliyenusurika kuuawa, wananchi na wafuasi wake wana shauku ya kumuona.

Msiba utafanyika Mtwara ambako mwili wa marehemu umeshafikishwa ilhali mapokezi yanafanyikia Dar.

Mimi binafsi na familia yangu tunaomboleza msiba wa mzee Mkapa lakini tunafanya hivi bila kushurutishwa bali kwa upendo tuliokuwa nao kwake. Isitoshe mambo ya msiba na mapokezi hayaingiliani kabisa. Kitu ninachoomba tu kuwe na utulivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…