Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Waliokuwa wanasema hakuna wanaChadema waje tena.

IMG_20200727_140345.jpg


IMG_20200727_135551.jpg
 
Kumekuwa na watu wakijifanya wana huruma eti wanawaonya watu wasiende kumpokea Lissu kwasababu watapigwa na askari. Wengine wanatumia msiba wa mzee Mkapa kama kisingizio.

Binafsi namuheshimu sana mzee Mkapa, mungu amlaze pema. Lakini haya mapokezi hayataathiri msiba kwa aina yeyote. Pia ieleweke Lissu ni mtu maarufu aliyenusurika kuuawa, wananchi na wafuasi wake wana shauku ya kumuona.

Msiba utafanyika Mtwara ambako mwili wa marehemu umeshafikishwa ilhali mapokezi yanafanyikia Dar.

Mimi binafsi na familia yangu tunaomboleza msiba wa mzee Mkapa lakini tunafanya hivi bila kushurutishwa bali kwa upendo tuliokuwa nao kwake. Isitoshe mambo ya msiba na mapokezi hayaingiliani kabisa. Kitu ninachoomba tu kuwe na utulivu.
 
Back
Top Bottom