Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Tundu Karibu Nyumbani.

Karibu nchini mwako,huku ulipozaliwa
Hili ni taifa lako,tena ulilolelwa
Wapo humu ndugu zako,wa damu wakuzaliwa
Rafiki na jamaa zako,kwa hamu wasubiriwa
Tundu karibu nyumbani,kilipo kitovu chako.

Karibu rafiki yetu,karibu tena nyumbani
Wewe bado ndugu yetu,asiejua ni nani
Karibu nyumbani kwetu,Tanzania ndo nyumbani
Karibu ule vya kwetu,na siyo vya ugenini
Tundu Karibu nyumbani,Ilipo asili yako.

BY: Idd Ninga.

LISSU; SAUTI YA HAKI ITAENDELEA KUNG’ARA

Nafsini mwaugulia, mlotaka Lisu afe,
Sirini mlivyomkalia, kula njama dhidi yake,
Mkitweta na kupania, eti Lissu aondoke,
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.

Mjengoni mlimtishia, kwa kugwaya hoja zake.
Na bila soni nje pia, kufisha maoni yake.
Mkishindana kumjazia, hata kesi ziso zake.
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.

Pamoja na kumrarua, marisasi pale kwake.
Kwa jazba kumbania, hata salamu kwake.
Yarabi hakuridhia, mauti iende kwake.
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake

Pasi na kumchulia, nainuka peke yake,
Yale mliyomnuia, yamepita mbali yake,
Leo tumeshuhudia, kwa raha kurudi kwake,
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.

Amen
 
Mungu alipanga anguko la Bashite kwa lengo la kuruhusu kurejea salama kwa Rais mtarajiwa. Hasante Mungu kwa kuturejeshea Amani na furaha iliyopotea kwa miaka mitano.
Umewaza kama Mchungaji wa Wanakondoo wa Mungu. Nami nasema kweli Kila kitu hutokea kwa mapenzi ya Mungu
 
Mkuu hapa uwanja wa ndege watu wanabubujikwa na machozi.

1:Kumuona mtu aliye pigwa risasi zaidi ya 16 kama tembo mharibifu wa mazao akirudi anatembea kwa miguu yake mwenyewe.

2:Jinsi wana nchi walivyo amua kujitokeza kwenda kumpokea kiongozi wao bila ya kuogopa mikwara ya polis hapo jana.

3: Hata baada ya miaka 5 ya kupigwa stop ya kutokutana kwa shughuli za kisiasa lkn bado watu wapo na mapenzi makubwa sana na cdm.

Hili jambo limewaliza sana watanzania.
Niko mitaa fulani,jamaa kama 10 around wanafuatilia hili tukio wengi wao wakipangusa machozi!!!!!!
 
Kama lisu angelikuwa Muislamu, Siku hizi tatu Muhimu sana kwa ibada na Maombi, Ningemshauri kufunga akeshe na kuomba,
Alitakalo atapewa ,
Lakini wacha nimuombee mimi ikiwa Mungu hili la Lisu likatika mapenzi yake na Kunikubali mimi kwa Udhaifu nilionao

Kwa walilomfanyia lissu inabidi aconsult Mababu wa Congo au kakonko wampike na mtu yeyote atayemgusa ateketee yeye na ukoo wake wote ,ajiwekee tego la Ndizi kila ndizi ikidondoka inaodoka na mtu wa ukoo atakayemfanyia ubaya tena.
 
nawasalimu katika jina la Ed Kawiche

sijawahi kushuhudia kundi la watu wanafki km hawa ma'ccm! hivi inakuaje mikwara inakuwa mingi mpaka sasa tunawaona mmekuwa paka watu?

kelele za kusema mh Tundu akifika tu mnamkamata na ataisoma namba ziko wapi sasa?
mara mh Tundu ni msaliti wa taifa na haina budi kufa... mbona mmekuwa kimya hv?

leo nimeamini ni kundi la watu wachache (ccm) ndyo mnaotisha wananchi wa nchi takatifu na yenye amani Tanzania.

utaifa kwanza acheni kutuchimba mikwara watanzania tunaolitakia mema taifa letu teule Tanzania.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
subira yavuta kheri
 
Kumbe zile vurugu zote hadi mtoto wa watu Akwilina akauawa ni Makonda! Mpumbavu sana. Ona leo watu tunafurahia demokrasia bila bughudha! Pamoja na Polisi kutoa jamba jamba tumeenda kwa kifua.
 
Wakuu heshima kwenu,

Kama ilivyo ada ya mwanadamu kuwa na hisia na upendo juu ya watu wengine nami moyo wangu umekuwa na upendo juu ya taifa la ubelgiji.

Nalipenda taifa hili kwa kumlinda na kumpigania mtanzania mwenzetu.
 
Bila shaka macho ya dunia yako Tanzania kuona tundu lissu atakavyowasili na namna ya kupokelewa Tanzania. Je, wanaompokea Ni wangapi na wamevaa barakoa?

Hii itasaidia Sana utalii wetu kwa wageni kujenga Imani. Tuwaache watu wengi waende kumpokea Lissu Kama kweli anakuja Tanzania
 
Back
Top Bottom