ostrichegg
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 12,050
- 6,199
Tundu Karibu Nyumbani.
Karibu nchini mwako,huku ulipozaliwa
Hili ni taifa lako,tena ulilolelwa
Wapo humu ndugu zako,wa damu wakuzaliwa
Rafiki na jamaa zako,kwa hamu wasubiriwa
Tundu karibu nyumbani,kilipo kitovu chako.
Karibu rafiki yetu,karibu tena nyumbani
Wewe bado ndugu yetu,asiejua ni nani
Karibu nyumbani kwetu,Tanzania ndo nyumbani
Karibu ule vya kwetu,na siyo vya ugenini
Tundu Karibu nyumbani,Ilipo asili yako.
BY: Idd Ninga.
LISSU; SAUTI YA HAKI ITAENDELEA KUNG’ARA
Nafsini mwaugulia, mlotaka Lisu afe,
Sirini mlivyomkalia, kula njama dhidi yake,
Mkitweta na kupania, eti Lissu aondoke,
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.
Mjengoni mlimtishia, kwa kugwaya hoja zake.
Na bila soni nje pia, kufisha maoni yake.
Mkishindana kumjazia, hata kesi ziso zake.
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.
Pamoja na kumrarua, marisasi pale kwake.
Kwa jazba kumbania, hata salamu kwake.
Yarabi hakuridhia, mauti iende kwake.
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake
Pasi na kumchulia, nainuka peke yake,
Yale mliyomnuia, yamepita mbali yake,
Leo tumeshuhudia, kwa raha kurudi kwake,
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.
Amen