LISSU; SAUTI YA HAKI ITAENDELEA KUNG’ARA

Nafsini mwaugulia, mlotaka Lisu afe,
Sirini mlivyomkalia, kula njama dhidi yake,
Mkitweta na kupania, eti Lissu aondoke,
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.

Mjengoni mlimtishia, kwa kugwaya hoja zake.
Na bila soni nje pia, kufisha maoni yake.
Mkishindana kumjazia, hata kesi ziso zake.
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.

Pamoja na kumrarua, marisasi pale kwake.
Kwa jazba kumbania, hata salamu kwake.
Yarabi hakuridhia, mauti iende kwake.
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake

Pasi na kumchulia, nainuka peke yake,
Yale mliyomnuia, yamepita mbali yake,
Leo tumeshuhudia, kwa raha kurudi kwake,
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.

Amen
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Unafikiri tz nzima ni hako ka kikundi tu?

Kumbe ndio maana huwa mnasema mnakubalika kumbe akili zenu zimeishia hapo ufipa tu
Wewe Akili yako imeishia Lumumba au imeishia gheto kwa cyprian Musiba mnaposhinda mkivuta Bangi
 
Mungu alipanga anguko la Bashite kwa lengo la kuruhusu kurejea salama kwa Rais mtarajiwa. Hasante Mungu kwa kuturejeshea Amani na furaha iliyopotea kwa miaka mitano.
Umewaza kama Mchungaji wa Wanakondoo wa Mungu. Nami nasema kweli Kila kitu hutokea kwa mapenzi ya Mungu
 
Niko mitaa fulani,jamaa kama 10 around wanafuatilia hili tukio wengi wao wakipangusa machozi!!!!!!
 

Kwa walilomfanyia lissu inabidi aconsult Mababu wa Congo au kakonko wampike na mtu yeyote atayemgusa ateketee yeye na ukoo wake wote ,ajiwekee tego la Ndizi kila ndizi ikidondoka inaodoka na mtu wa ukoo atakayemfanyia ubaya tena.
 
subira yavuta kheri
 
Kumbe zile vurugu zote hadi mtoto wa watu Akwilina akauawa ni Makonda! Mpumbavu sana. Ona leo watu tunafurahia demokrasia bila bughudha! Pamoja na Polisi kutoa jamba jamba tumeenda kwa kifua.
 
Wakuu heshima kwenu,

Kama ilivyo ada ya mwanadamu kuwa na hisia na upendo juu ya watu wengine nami moyo wangu umekuwa na upendo juu ya taifa la ubelgiji.

Nalipenda taifa hili kwa kumlinda na kumpigania mtanzania mwenzetu.
 
Bila shaka macho ya dunia yako Tanzania kuona tundu lissu atakavyowasili na namna ya kupokelewa Tanzania. Je, wanaompokea Ni wangapi na wamevaa barakoa?

Hii itasaidia Sana utalii wetu kwa wageni kujenga Imani. Tuwaache watu wengi waende kumpokea Lissu Kama kweli anakuja Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…