Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Karibu tena Lissu tujenge nchi.
Huku Corona inasemekana hakuna na ilikwisha isha nadhani umejionea hata wafuasi wamekuthibitishia hilo kwa vitendo. Imekwishaje mimi sijui.
Bila shaka kesho utamsindikiza Mzee wetu Mkapa japo aliwaiteni wapumbavu mwaka 2015 mkalalama kuwa mmetukanwa.
 
Hii ni siku kubwa na kwa msingi huo nimeamua kuwapa uhuru wote niliowaweka kwenye ignore list yangu na sasa nimeweza tena kuzisoma posts zenu lakini duh! Hakika Mungu ni mkubwa, Mungu ni taa na penye mwanga giza ni marufuku...asante Mungu kwa kuangaza kwa mwanga mkali ndani ya taifa letu na kusababisha shetani na wafuasi wake kuumbuka na kuanza kutafuta pa kuficha nyuso zao.
 
Leo CHADEMA walijua watatikisa jiji kwa umati lakini hawaamini kilicho tokea, kati ya wakazi zaidi ya milioni 6 waishio jijini, wameambulia watu chini ya 1000 na wengi wao wakiwa ni viongozi toka mikoa mbalimbali.

Walijipanga sana huku wakisindikizwa na kelele za vyombo vya mabepari na chombo chao hiki cha JF (maana sikuhizi JF imekuwa sehemu yao) ila Watanzania wameonesha kuwa hawana mpango nao.

Nimeshuhudia Lissu akishangaa jengo lakisasa Terminal 3, ilibaki kidogo aseme CCM hoye, namsihi baada ya kukatwa na CHADEMA atembelee miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali hii kisha aende kisutu akiwa na dereva wake bila shuruti kujibu mashtaka yanayo mkabili.
cc
jingalao mng'ato na wazalendo wengine
Walitakiwa 30 tuu mbona wamekuja wengi sana
 
Hii ni siku kubwa na kwa msingi huo nimeamua kuwapa uhuru wote niliowaweka kwenye ignore list yangu na sasa nimeweza tena kuzisoma posts zenu lakini duh! Hakika Mungu ni mkubwa, Mungu ni taa na penye mwanga giza ni marufuku...asante Mungu kwa kuangaza kwa mwanga mkali ndani ya taifa letu na kusababisha shetani na wafuasi wake kuumbuka na kuanza kutafuta pa kuficha nyuso zao.
IMG-20200727-WA0042.jpg


Jr[emoji769]
 
Huu ni ujumbe kama tuna tume huru Mwamba anachapa mapema tu saa 4 asubuhi

What are the actual numbers ya watu kwenye hiyo nyomi?

Kuiacha hisia na kutumia uhalisia, hugo nyomi yote ipige kura, halafu zidisha mara kumi, Kira milioni 6 zitafika? Kama zitazidi milioni 6 zitatoboa ushindi?

Upinzani bado utasubiri sana kuchukua dola. Amsha amsha iendeleetu.

Tundu karibu nyumbani kumenoga.
 
[emoji3577][emoji3577][emoji3577][emoji3577][emoji3590][emoji1665][emoji170][emoji1665][emoji3590][emoji1665][emoji170][emoji1665][emoji170][emoji3590][emoji1665]
 
Nabii Lissu ana maono ambayo wengine wote hawaoni... aliona viashiria vyote vya udikteta akasema huyu jamaa ni dikteta uchwara......

Bahati mbaya sn anarudi huku jamaa akiwa dikteta kamili kuanzia kwenye chama chake mpaka kwenye mihimili yote ya dola imewekwa kiganjani mwake......

TUNDU Lissu ndiye pekee wa kurejesha misingi imara ya taifa. Aanze na kufumgua kesi ya kikatiba kufutwa kwa maamuzi ya kuruhusu baadhi ya watz kupewa ruhusa kisheria kuvunja katiba ya nchi bila kushitakiwa....
Tundu Lissu anapendwa na vyombo vyote vya Dola ni vile tu hawajiweki wazi. Vyombo vya dola vinajua maamuzi ya Jpm hayana tija kwa taifa.
 
Nyie watu embu acheni masihara, mtu uliyemmiminia risasi 38 za kuulia nyati na kudhani umemuuwa halafu siku unakutana nae ni mzima wa afya , inahitaji ujasiri wa ziada kupanga tukio kama hilo kumdhuru

Hata aliyefyatua zile risasi sidhani kama bado tupo nae duniani
Hata nyati hapigwi Risasi 30. Mbili au Tatu tu chali. Ni upotevu wa risasi kuua nyati mmoja kwa risasi 30.
 
Back
Top Bottom