Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Halima amefanya vyema, si vibaya chama kikatoa shukran rasmi kwa jeshi la polisi, hata kama ni kwa kinafiki. Pia nashauri sana Tundu Lisu ashauriwe kutokwenda kesho msibani. Kwangu bado Lisu ana hasira na lile shambulio, kwa vyovyote atataka kuionyesha serikali na hasa rais Magufuli kuwa amepona. Na mashabiki wake wanaweza kuonyesha furaha iliyopitiliza ambayo itaipa serekali kuchukua maamuzi hasi.

Kwakuwa wamemstahi leo, ni vyema angeachana na huo msiba, kuna nafasi kubwa ya kushindana na ccm. Na kama itawezekana kuanzia sasa Lisu pia ashauriwe asitumie lugha kali za kupandisha hamasa za chuki, bali apambane na ccm kwa sera. Kuna sehemu nyingi sana za kuwazidi ccm, mfano huu rushwa ya juzi kwenye chaguzi zao, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk. Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi binafsi.
Msiba ni wa waTZ wote bila kujali hitikadi za vyama vyao, hivyo ni haki yake kwenda kumuaga kiongozi wake wa kitaifa. Hasa ukizingatia kwamba hakuna uhakika bado kwamba Lissu ataweza kwenda kwenye mazishi. Muacheni akatoe heshima zake za mwisho kama raia wengine. Hata waziri mkuu amekaribisha kila mtu mwenye kuweza kutoka kila kona ya nchi aende akaage mwili.

"rushwa, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk."
Ndio anayo simamia Lissu siku zote, na ni mambo ambayo hayatakiwi kuchekewa. Ni lazima yazungumzwe kwa ukali kwa sababu ndio misingi mikuu ya taifa.

"Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi binafsi."
Hapa kwenye shambulizi binafsi sijakuelewa vizuri. Kwa sababu (a) Lissu wakati anashambuliwa alikuwa mbunge wa bunge la JMT. Na bunge ndilo linalotunga/pitisha sheria ambazo viongozi wanazitumia kuiongoza nchi. Kumshambulia mmoja kati ya wabunge kwa namna alivyoshambuliwa Lissu ndio umeligusa bunge zima na serikali kwa ujumla. (b) Shambulio lile kuna kila dalili kwamba halikuwa la uporaji. (c) Mpaka sasa hivi vyombo vyenye mamlaka havija toa taarifa ya tukio lile.
 
Asanteni sana @tanpol !!! Tunawapenda SANA!! SISI ni watu wema!!! Tanzania ni YETU SOTE. Tusiruhusu maslahi ya WATU wachache watuvurugie UPENDO wa ASILI wa TAIFA LETU-Halima Mdee
Mara nyingi wanao chafua hali ya hewa ni polisi kwa kulazimisha yasiyo kubalika ili wapate kisingizio. Mfano mdogo ni pale airport makamanda walianzisha wimbo pale "kamanda tuvushe" lakini viongozi walipokataza mara moja watu walinyamaza na amani imekuwepo adi mwisho. Mdee yuko sahihi katika hili. Na hata wanao watuma hao polisi pia wamefanya busara sana maana dunia inafuatilia matukio mawili makubwa ndani ya nchi moja na kwa wakati mmoja. Watu kufanya wanayoyafanya sio kwamba hawana akili ama busara, la hasha, wanaamua tu kujitoa ufahamu kwa maslahi flani.
 
Sasa mnalialia nini??chuma kishatua subirini Oct tuwafundishe kucheza kiwazenza
 
Leo Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe wameonesha usaliti kwa mara nyingine. Awali walijiweka kama wanajali wananchi ila leo wamekuwa tayari kuangamiza watanzania kisa Lissu.

Walijivika joho la WHO huku wakihubiri Sera za kubaki ndani maarufu kama Karantini kumbe ni unafiki mkubwa.
Tuwapime, tuwashangae, tuwakatae.
Ungejiuliza kwanza walijiweka karantini wakati gani? Na kwa nini walijiweka karantini ? Serikali ilikuwa ikizungumza nini kuhusu covid-19? Na sasa serikali inazungumza nini? Mapokezi ya Mwinyi kule ZNZ uliyaonaje? Ama pale uhuru ambapo watu wanaaga mwili wa mstaafu umeona mazingira yake? Ama tatizo lako ni chadema tu?
 
Kama Kuna Mambo mema lazima tushukuru. Tazameni vyesi vyote chanzo chake Ni uonevu na usimamizi mbaya wa Sheria toka jeshi la polisi
 
Leo Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe wameonesha usaliti kwa mara nyingine. Awali walijiweka kama wanajali wananchi ila leo wamekuwa tayari kuangamiza watanzania kisa Lissu.

Walijivika joho la WHO huku wakihubiri Sera za kubaki ndani maarufu kama Karantini kumbe ni unafiki mkubwa.
Tuwapime, tuwashangae, tuwakatae.
Nguruwe wa Lumumba hamuishi viroja
JamiiForums-1364449287~2.jpg
 
Leo Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe wameonesha usaliti kwa mara nyingine. Awali walijiweka kama wanajali wananchi ila leo wamekuwa tayari kuangamiza watanzania kisa Lissu.

Walijivika joho la WHO huku wakihubiri Sera za kubaki ndani maarufu kama Karantini kumbe ni unafiki mkubwa.
Tuwapime, tuwashangae, tuwakatae.
Nimejifunza kuwa Wasukuma wengi sio watu wazuri.
Mshana Jr
 
Nimeshangaa wabunge kumnanga Mwenyekiti kuhusu ule mguu lkn bado anatembelea magongo.kumbe haigizi?
 
Mh tundu lisu dunia imeona ulichofanyiwa na ujio wako umewatia aibu watesi wako.

Mapokezi yako yawape heshima waliokuja kukulaki. Ili waiandike historia Yao ya mapenzi na amani kupitia wewe.

Tal the great
Hajawahi kuhubiri /ku-instigate watu wavunje amani! He has never done so! Labda useme awe mnafiki kumpamba Jiwe
 
Pumbavu huna la kuandika hapo Bora ukavae Dera tujue unaserebuka tuwahi kuleee
 
Back
Top Bottom