Huu ni zaidi ya ushauri.
Tundu Lissu hana sababu tena ya kupoteza muda mwingi wa kuzungumzia hali iliyompata. Ni nani asiyelijua hilo?
Sasa hivi atumie muda wake mwingi kuwa kama mwalimu, afundishe wananchi kuelewa haki zao za msingi ili wasiruhusu tena haki hizo zichezewe.
Ana haki, na uwezo wa kuzungumzia ulazima wa utawala bora na umhimu wake katika maendeleo ya nchi yetu.
Chaguzi zetu, afundishe watu kujua umhimu wa kuchagua viongozi wao wanaowataka wao bila ya kura zao kuharibiwa. Watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura, ili hata kutokuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi, iwe vigumu kwa tume hiyo kubadili matokeo.
Mahusiano yetu kimataifa, sio jambo la anasa, ni jambo la muhimu sana. Hatuwezi kujitenga kwa sababu uchumi wetu unategemea mahusiano hayo.
Waliopo huko ndani ya CHADEMA, ni wajibu wenu kumpa ushauri Lissu, na hasa kama ndiye atakayekuwa mpeperusha bendera wenu.
Wananchi sasa hivi hawategemei kuona nyinyi ndio mkiwa wachokozi. Mliyotendewa liwe fundisho, lakini msitafute kuchokoza kama njia ya kulipa kisasi. Mtapoteza imani ya wananchi