Wanajeshi kwa waliohusika na tukio hili wawajibishwe
Hii Tabia ya kuonea raia kisa tu ofisa wa usalama wa Taifa kakwaruzana na waendesha magari barabarani inatoka wapi?
Hii inaonyesha kuwa tuna Usalama wa Taifa incompentent, wasiojua kazi zao, ambao wanatumia nafasi zao kuonea watu.

Ni wapi katika majukumu ya usalama wa Taifa, Usalama wa Taifa unafanya kazi za Trafiki barabarani?

Leo hii ofisi na premise za usalama wa Taifa zinaenda kutumika kama parking ya kukamatia raia eti kisa raia kakwaruzana na ofisa mmoja huko barabarani ni ushamba wa hali ya juu na ni kuipaka Idara matope.

Tunataka Idara ya Usalama wa Taifa TISS imchukulie hatua za kinidhamu huyo ofisa anayeonekana kuleta kiburi kwa kutumia kazi yake kuonea watu.

Kibaya zaidi anaamrisha raia anyang'anywe simu yake bila search warrant au bila kufuata sheria za kipolisi, huu kama siyo ujambazi ni nini.

Huu utovu wa nidhamu ukomeshwe mara moja, hatutaki usalama wa Taifa unaoendeshwa kihuni.

 
Back
Top Bottom