brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Unyanyasaji huu wa vyombo vya dola haukubaliki.

Your browser is not able to display this video.


Kwanini sheria za nchi zilizopo hazifuatwi?

Kwa hakika tuungane kuukataa ubazazi wa namna hii.

---------------------
Ikumbukwe:

 
Hii Tabia ya kuonea raia kisa tu ofisa wa usalama wa Taifa kakwaruzana na waendesha magari barabarani inatoka wapi?
Hii inaonyesha kuwa tuna Usalama wa Taifa incompentent, wasiojua kazi zao, ambao wanatumia nafasi zao kuonea watu.

Ni wapi katika majukumu ya usalama wa Taifa, Usalama wa Taifa unafanya kazi za Trafiki barabarani?

Leo hii ofisi na premise za usalama wa Taifa zinaenda kutumika kama parking ya kukamatia raia eti kisa raia kakwaruzana na ofisa mmoja huko barabarani ni ushamba wa hali ya juu na ni kuipaka Idara matope.

Tunataka Idara ya Usalama wa Taifa TISS imchukulie hatua za kinidhamu huyo ofisa anayeonekana kuleta kiburi kwa kutumia kazi yake kuonea watu.

Kibaya zaidi anaamrisha raia anyang'anywe simu yake bila search warrant au bila kufuata sheria za kipolisi, huu kama siyo ujambazi ni nini.

Huu utovu wa nidhamu ukomeshwe mara moja, hatutaki usalama wa Taifa unaoendeshwa kihuni.

Your browser is not able to display this video.
 
Pole sana kwa kukwangua gari la watu. Yatakwisha tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…