Kuna fala mmoja huwa anajifanya au sijui ndio security wa Taifa kweli!!!? Nilikuwa nasikia sana tabia zake za kuwa akikutaa bar unakunywa na yeye anaagiza kama uvyokunywa wewe kisha anasema utalipa wewe,.
Bahati nzuri mimi sinywi ila nikasema hasirogwe kuingia katika anga zangu za aina yoyote hile.
Siku moja nikaenda bar na rafiki yangu mmoja alikuwa ananywa zake bia mimi nikiwa nakunywa sparletar yangu mara jamaa kaja na kama kawaida yake siku hiyo akafikia kwenye point yetu. Akatusalimia akaenda counter kaagiza na yeye bia zake kama za jamaa yangu na kumwambia counter kuwa watalipa wale pale akituonesha sisi.
Baada ya sisi kumaliza yetu tukaomba bill ilipoletwa tukaona bill imekuja mara dufu, nilipooliza tukajibiwa kuwa na pombe zile pale. Mimi nikamwambia sisi hatumfahamu alipe mwenyewe, baada ya hapo jamaa si akaja akatuuliza kwa nini hatutaki kunilipia?
Nikamuuliza tukulipie wewe una tatizo gani? Nae akatuuliza kwani nyinyi hamnifahamu, na Mimi nikamuuliza "sisi unatufahamu?" Nikamwambia ondoka kabla sijakushia dhahama, wakati huo watu wametunguka wakisilizia. Naona kaondoka uku akisema "mtanijua tu"
Juzi nimekutanae barabarani nashangaa kanisalimia bro za ziku?
Nikajifanya sikumsikia.