Watoto ni matokeo ya ngono, Si zawadi wala baraka kutoka kwa Mungu!

Watoto ni matokeo ya ngono, Si zawadi wala baraka kutoka kwa Mungu!

Sawa tuachane na huyo Mungu kwanza, je unaamini au kukubali kwamba, ulimwengu una creator?
Swali zuri mkuu. Maana at one point lazima tukubali kuwa kuna kitu sijui nguvu ilikuwepo tu bila kuumbwa halafu ndo tutoke hapo tuamie kwengine.
 
  • Thanks
Reactions: ---
Kitu ambacho nadhani hawa watu wanachanganya ni kutaka kuthibitisha mambo ya kiroho kwa mbinu kisayansi , ukifanya hivi tayari umeingia mkenge. Kama Physics na Math zenyewe pia zina limits na hazitoshi kuelezea kila kitu kwenye huu ulimwengu.
True. Halafu Mzungu akija na Unidentified Anomalous Phenomena sisi sisi wazee wa logic tunakuja na reasoning uchwara kujadili kuwa ina weza kuwa ni nini? Au alien?

Mlokole, muislamu sijui wazee wa kimila wakija na amekutana na jini au malaika sijui mzimu huyo kwetu ni kichaa ana illusions hamna kitu kama hicho n.k n.k
 
Sawa tuachane na huyo Mungu kwanza, je unaamini au kukubali kwamba, ulimwengu una creator?
Hapana.

Kwa nini unataka ulimwengu uwe na creator?

Kwa nini unataka ulimwengu uwe created?

If complex systems require a creator then creator requires a more complex creator that imply an infinite chain of creators that get more and more complex.

Ikiwa mifumo tata inahitaji muumbaji, basi muumbaji naye anahitaji muumbaji aliye tata zaidi. Hilo linapelekea msururu usio na mwisho wa waumbaji, ambapo kila mmoja anakuwa tata zaidi kuliko aliyemtangulia.
 
Imani bila matendo ni Bure.

Mtu anayeamini kuwa anaweza kwenda ulaya bila Passport akashindwa kuigeuza imani yake kuwa tendo linalowezekana katikati ya wanaoona haiwezekani huyo ameshindwa kuileta imani aliyo nayo ifanye kazi katika ulimwengu wa logic so inabakI kuwa Bure.

Mfano binadamu walioamini kuwa tunaweza kupaa wakaunda ndege wasingezigeuza imani zao zikafanya kazi kwenye logic, wangekuwa na tofauti gani na huyu anayeamini wanaweza kwenda ulaya bila Passport?

Wale wasabato badala ya kwenda airpot na imani bure pekee wangejiuliza ili imani ya kwenda ulaya bila Passport ifanikiwe kwenye ulimwengu wa logic nini kinatakiwa? Huwezi jua kwa kujiuliza hili swali na kupata majibu sahihi labda baada ya miaka kadhaa vizazi vijavyo wangeweza kwenda ulaya bila Passport. Sasa sijajua ingekua ni kwa jina la YESU au ingekuaje.
Kama imani bila matendo ni bure, then imani peke yake pia ni bure.

If faith without work is nothing, then faith itself is nothing.

Kwa hiyo imani si chochote na wala haiwezi kufanya lolote.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Imani bila matendo ni Bure.

Mtu anayeamini kuwa anaweza kwenda ulaya bila Passport akashindwa kuigeuza imani yake kuwa tendo linalowezekana katikati ya wanaoona haiwezekani huyo ameshindwa kuileta imani aliyo nayo ifanye kazi katika ulimwengu wa logic so inabakI kuwa Bure.

Mfano binadamu walioamini kuwa tunaweza kupaa wakaunda ndege wasingezigeuza imani zao zikafanya kazi kwenye logic, wangekuwa na tofauti gani na huyu anayeamini wanaweza kwenda ulaya bila Passport?

Wale wasabato badala ya kwenda airpot na imani bure pekee wangejiuliza ili imani ya kwenda ulaya bila Passport ifanikiwe kwenye ulimwengu wa logic nini kinatakiwa? Huwezi jua kwa kujiuliza hili swali na kupata majibu sahihi labda baada ya miaka kadhaa vizazi vijavyo wangeweza kwenda ulaya bila Passport. Sasa sijajua ingekua ni kwa jina la YESU au ingekuaje.
Wright brothers hawakuwa na imani kama hiyo yenu watu wa dini. Wao walikuwa wanatazama ndege mnyama anavyopaa na tiara zinavyorushwa na watoto wakajenga imaginations au dhana kwamba inawezekana wakatengeneza chombo kama ndege mnyama. Mchakato wao ulikuwa ni wa Sayansi kabisa ukiwa na rejea halisi za kuanzia.
 
If complex systems require a creator then creator requires a more complex creator that imply an infinite chain of creators that get more and more complex.
Well, I argue that the creator is a necessary being one that exists by its own nature and does not require a cause or creator. This necessary being is the foundation that stops the infinite regress problem which is where this is leading. Without such a necessary being, we are left with no ultimate explanation for existence or complexity.

Additional ly, while natural processes explain some complexity, they do not explain the origin of the fundamental laws and conditions that allow such processes to occur. The existence of these laws and the fine-tuning of the universe point to an intelligent source beyond naturalistic explanations.

Therefore, the belief in a creator is not just about complexity but about the necessity of an uncaused cause that grounds all existence
 
Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Creator Kabla ya kusema ni necessary being.

Kusema tu kuna necessary being bila kuthibitisha uwepo wake, ni kufosi bila uthibitisho.

Kwanza thibitisha kama huyo creator yupo.
 
Mkuu kabla ya kuendelea naomba nikuulize kitu hiki; ukiachana na mambo ya kiimani unafikiri kwamba kila kitu kinawezekana kwa logic tu?
 
Wright brothers hawakuwa na imani kama hiyo yenu watu wa dini.

Wao walikuwa wanatazama ndege mnyama anavyopaa na tiara zinavyorushwa na watoto wakajenga imaginations au dhana kwamba inawezekana wakatengeneza chombo kama ndege mnyama. Mchakato wao ulikuwa ni wa Sayansi kabisa ukiwa na rejea halisi za kuanzia.
Ndo imani yenyewe. Mchakato wa kisayansi umekuja baada ya kulink imani na logic na facts. Imagination ni imani. Yaani unaangalia kitu kisichokuwepo katika wakati husika halafu unaamini kinawezekana kuwepo.

Step ya kinachofata either ni muujiza au sayansi ni step baada ya kuamini kuwa lisilokuwepo linaweza kuwepo.
 
Watoto ni matokeo ya ngono, Na wala sio baraka wala zawadi kutoka kwa Mungu yeyote.

Ndiyo maana “slay queens ” wanatafuta pesa ili kutoa mimba, wakati mke mgumba wa mchungaji anatafuta mtoto kwa muda mrefu. Na mimba haishiki.

I'm out.

Kusema watoto ni “matokeo ya ngono tu” ni kupunguza jambo kubwa la uumbaji kuwa tendo moja la kimwili. Uislamu unafundisha kwamba ngono ni sababu, lakini Allah ndiye Muumba na Mpangaji wa watoto.

Qur’an inasema:

“Yeye huumba anachokitaka. Humruzuku amtakaye watoto wa kike, na humruzuku amtakaye watoto wa kiume; au huwapa wote wawili... na humfanya amtakaye kuwa tasa.”
(Qur’an 42:49–50)

Hivyo yule anayepata mtoto na yule anayekosa mtoto wote wako chini ya uwezo na hikma ya Allah. Na mtoto si “zawadi” kwa maana kwamba kila mtu lazima apewe mtoto; ni neema na amana pale Allah anapomjaalia.

Na usiwadhihaki wanawake wanaotamani watoto wala wale wanaopata mimba. Qur’an inatufundisha kusema: “Mola wangu! Usiniache peke yangu, nawe ndiye Mbora wa warithi.” (Qur’an 21:89)

Kwa hiyo, mtoto anaweza kuja kupitia sababu ya kimwili, lakini kusema hakuna Mungu anayehusika katika uumbaji wake ni dai linalohitaji ushahidi na si ukweli unaothibitishwa kwa kusema tu “watoto ni matokeo ya ngono.”
 
Ndo imani yenyewe. Mchakato wa kisayansi umekuja baada ya kulink imani na logic na facts. Imagination ni imani. Yaani unaangalia kitu kisichokuwepo katika wakati husika halafu unaamini kinawezekana kuwepo.

Step ya kinachofata either ni kwa muujiza au kwa sayansi ni step baada ya kuamini kuwa lisilokuwepo linaweza kuwepo.
Imaginations sio Imani.
Walio imagine bunduki, risasi na canons wakazitengeneza sio sawa na kina Kinjekitile waliokuwa wanaamini maji yatabadilisha risasi kuwa maji.
 
Imaginations sio Imani.
Walio imagine bunduki wakazitengeneza sio sawa na kina Kinjekitile waliokuwa wanaamini maji yatabadilisha risasi kuwa maji.
Wote wameanini. Mmoja akageuza imani kuileta kwenye logic mwingine akategemea itokee tu bila matendo. Imani bila matendo ni bure.

Kinjekitile aliamini risasi zinaweza geuka kuwa maji ila hakugeuza imani yake kuwa facts, angeweza kufikiri namna gani risasi ziwe maji na akafanikiwa hiyo tayari ingekuwa ni technology ambayo sasa hivi unaikataa sababu haipo.
 
Upo sahihi.

Haupo sahihi. Ongezea hapo Imani bila matendo ndo utakuwa sahihi.
Kama imani haiwezi kusimama yenyewe, then imani si kitu na haiwezi kitu.

Kwa sababu matendo na imani ni vitu viwili tofauti.

Matendo yanaweza kusimama yenyewe na yakaleta matokeo.

Imani haiwezi kusimama yenyewe, then it has nothing to do na matendo.

Matendo yatabaki matendo na wala haya hitaji imani.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Wote wameanini. Mmoja akageuza imani kuileta kwenye logic mwingine akategemea itokee tu bila matendo. Imani bila matendo ni bure.

Kinjekitile aliamini risasi zinaweza geuka kuwa maji ila hakugeuza imani yake kuwa facts, angeweza kufikiri namna gani risasi ziwe maji na akafanikiwa hiyo tayari ingekuwa ni technology ambayo sasa hivi unaikataa sababu haipo.
Hakuna muamini dini aliyewahi kugeuza imani yake ya superstitions kuwa facts, sio Kinjekitile sio Mwamposa wala yeyote yule.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kama imani haiwezi kusimama yenyewe, then imani si kitu na haiwezi kitu.
Imani inasimama yenyewe kama imani. Ila unapotaka ilete matokeo ndo matendo sahihi yanahitajika kuilink hiyo imani na matokeo unayoyataka.
Kwa sababu matendo na imani ni vitu viwili tofauti.
Yes. Kama ambavyo maji, cement na mchanga ni vitu tofauti ila ukitaka litokee tofali unavichanganya kwa ratio sahihi.
Matendo yanaweza kusimama yenyewe na yakaleta matokeo.
Matendo hayawezi simama pekeyake yakaleta matokeo. Matokeo ni hitimisho la muunganiko wa matendo na imagination ya unachotaka kitokee. Kuimagine kuwa kitu kinaweza kutokea pasipo kutokea ndo imani hiyo.
 
Hakuna muamini dini aliyewahi kugeuza imani yake ya superstitions kuwa facts, sio Kinjekitile sio Mwamposa wala yeyote yule.
Sawa. Lakini umeonganisha vitu viwili, imani na dini. Je dini ni matendo sahihi ya kuchanganya na imani ili ilete matokeo ya kinachoaminiwa?

Hivi unajua dini inaweza kuwa ni weapon ya kulimit uwezo wa binadamu kufanya anachoamini kitokee? Ukichanganya dini na elimu ya mtindo fulani uchwara kama hizi tulizo nazo unapata taifa la watu wa aina mbili.

1. Watu ambao wakiamini hawatendi sababu ya dini inachoelekeza.
2. Watu ambao wakiamini wanategemea logic iliyofungwa na elimu waliyokwisha ipata kutenda.
 
Imani inasimama yenyewe kama imani. Ila unapotaka ilete matokeo ndo matendo sahihi yanahitajika kuilink hiyo imani na matokeo unayoyataka.

Yes. Kama ambavyo maji, cement na mchanga ni vitu tofauti ila ukitaka litokee tofali unavichanganya kwa ratio sahihi.

Matendo hayawezi simama pekeyake yakaleta matokeo. Matokeo ni hitimisho la muunganiko wa matendo na imagination ya unachotaka kitokee. Kuimagine kuwa kitu kinaweza kutokea pasipo kutokea ndo imani hiyo.
Hapa ume introduce tena neno imagination naku link na imani.

Kama imani inasimama yenyewe kama imani, Imagination inatoka wapi kwenye imani?

Wewe sentensi yako ya kwanza si umesema mwenyewe kwamba, imani inasimama yenyewe kama imani?

Kwa nini una link imagination na imani?

Imagination ni imani?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom