Wazazi wenye wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Darasa la Saba 2022 tukutane hapa tutiane moyo

Sasa mtashauriana vipi wahanga kwa wahanga.

Pole ila ruhusu na ambao si wahanga wakushauri.
 
Hakuna kitu unachoelewa mkuu jitahidi uulizie kwa watu wanaojua,angalia matokeo ya 2021 ndiyo utaelewa ninachozungumzia
Mwanafunzi ufutiwa matokeo tu endapo yeye kashiriki kwenye udanganyifu yaan amekamatwa na kitu ambacho kinaashiria wizi wa mtihan mfno kushikwa na nondo, kuwa na picha tofauti...

Matokeo hayo yameshikiliwa sioo kufutwa ndo maaan yameandikwaa W*

Fatilia baraza la mitihan pale BAMAGA utapata matokeo ya mwanao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeishia kulaumu bila kutoa kwa ufasaha nini anatakiwa afanye. Ukiishia kulaumu na kuponda bila kutoa way forward unakuwa huna tofauti na unayemlaumu.
 
Umeeleza vizuri sana... Nina swali je kwa sasa hivi ule utaratibu wa mwanafunzi kurudia darasa upo? Yaani kama amefeli au kutofanya mtihani anaweza mwakani akarudia darasa la 7 na mwisho wa mwaka akafanya mitihani?
 
Inaruhusiwa kurudia darasa la 7 mkuu? Utaratibu ukoje?
 
Hakuna uchawi hapo, anaenda sekondari kama kawaida, ishu ingrkuwa sisi ambao tunategemea mtoto afaulu tuuze kuku kumpatia pesa asome sekondari ya serikali
Umewahi kuona mtu yeyote kwa miaka hii miwili hakumaliza la saba na kaenda sekondari? Nijuavyo kwa Sasa ili apande kwenye prems lazima uweke no ya psle.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Poleni sana wakuu

Mimi nashauri ufuate taratibu zitakazotolewa na wizara husika usichukulie poa kabisa. Kabla ya kupiga hatua consult watu wa wizara watakupa muongozo kwa faida ya mwanao baadae.

Pili, nawashauri muifungulie shule mashtaka ya madai, haiwezekani wakawapoteza hivi, tafuteni wakili au mnaweza nipa hii kazi mimi pia, kuna uzembe wa taasisi umewagharimu ninyi na watoto wenu pia. Ipo nafuu Mahakamani ni nyie tu muamue.

Poleni sana. Haya mambo yanafadhaisha,, yana uzi na kukasirisha sana.
 
Umewahi kuona mtu yeyote kwa miaka hii miwili hakumaliza la saba na kaenda sekondari? Nijuavyo kwa Sasa ili apande kwenye prems lazima uweke no ya psle.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Watu wanachukulia poa cheti/namba ya elimu ya msingi ila hii kitu ina cost sana maana kuna wakati vinatumika kwenye uraia au kujua mtu alipokulia, in short kina mambo mengi nyeti yasiyohusu elimu hata.
 
Wasimamizi hawajui lolote kivipi mkuu!?
wizi wa mitihani wa kutumia wasimamizi ni wakizamani sana na huo sio wizi ni udanganyifu na mara nyingi unatokea ndani ya chumba cha mitihani (lazima ujue tofauti ya wizi na udanganyifu)

udanganyifu hifanywa na vishule vyetu hivi.... wizi wanafanya giants na wana hadi mawakala wa hizo kazi kuanzia mwanzo (maandalizi) ya mtihani hadi mwisho wanajua....

baadhi ya shule ziliyumba baada ya mawakala wao kukamatwa fuatilia utazijua
 
Kama B ndo jibu sahihi wafanyaje?
 
NECTA mwaka huu hawajarank shule,nadhani Ili kupunguza udanganyifu,Yale mabango kuwa shule imekuwa ya kwanza yatapungua
 
udanganyifu hifanywa na vishule vyetu hivi.... wizi wanafanya giants na wana hadi mawakala wa hizo kazi kuanzia mwanzo (maandalizi) ya mtihani hadi mwisho wanajua....
Duh!!
Kwahiyo unataka kuniambia walipata mitihani kabla wakawapa majibu watoto...
Hili haliwezekani mkuu
 
Duh!!
Kwahiyo unataka kuniambia walipata mitihani kabla wakawapa majibu watoto...
Hili haliwezekani mkuu
hahahhhahaha shauri ako mkuuu ningekupa mifano ya shule chache ila ntazichafua zaidi mana hii nayo ni biashara.
 
Hili tatizo pia linasababishwa na baraza la mitihani. Haiwezekani kabisa utunge mtihani wote maswali yawe ni multiple choices... Ilitakiwa mtihani kama una sections 3 basi multiple choice iwe ni only one section na sections nyingine ziwe ni za kujaza majibu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…