Wanabodi, Hakika ule usemi usemao akili sio ukubwa wa kichwa umetimia kwa huyu waziri Seleman Jafo,
Leo unaitisha vyombo vya habari kuomba wale ulioshiriki kuwafuta warudishwe kugombea, Tulishauri bandikeni majina ya wanaccm tu kwenye mbao hapa JF na umetekeleza ushauri wetu hapa JF, Tunakupongeza kwa hilo, Sasa tu nakushauri tena endelea na sera za kifashisti na kibaguzi ili wewe na kundi lako mje mvune mnachokipanda
Jafo alichagua kuwa wa moto kufuata sheria za kifashisti na kibaguzi, Jafo uliamua kuigawa jamii makundi mawili ili lengo lako la watu kupigana na kuchomeana mali lipate kutimia na umeshalitimiza baadhi ya maeneo, Uliamua kukaa kimya ulipoambiwa watendaji wanafunga ofisi hawataki kupokea fomu za vyama vingine
Jafo Leo umegeuka vuguvugu hujawa moto wala baridi, Hujui la kufanya, Mamlaka iliyokuteua imekuzidi akili, Kwa elimu yako ungeandika barua kwa mamlaka ya uteuzi upumzike, Umegeuka kituko mbele ya Jamii
Wewe ni mmoja ya wacheza ngoma wa Pwani uliepata elimu kidogo hivyo tulitegemea utaijenga jamii yako kwa fikra na mawazo, Sasa umegeuka katuni mbele ya jamii
Unaongea huku Facial impression au muonekano wake usoni ni dhahiri una mawazo mengi Sana lakini hujui hatima ya uwaziri wako
Seleman Jafo wewe ni sadaka inayosubiriwa na maamuzi ya wananchi, Bosi wako anasubiri reaction ya wananchi Halafu wewe utatolewa sadaka kuwa hujasikiliza wananchi
Maelezo uliyoyatoa Leo yanapingana na ndugu yako Humprey pole pole aliyesema CCM na watendaji wa kata na vijiji walichofanya kuwafuta wagombea wengine ni sahihi,
Jafo unasikiliza chama au unasikiliza aliyekuteua, Kwa ufupi ulipaswa kusimamia ukatili uliouonyesha toka mwanzo na kufa na tai shingoni
Ulisahau kuwa asilimia 90 ya watanzania hawana vyama ni Raia tu wa kawaida, Wewe na kundi lako mlifikiri wale viongozi wa mitaa na watendaji wanaongoza ccm, Act na Chadema
Kumbuka kuna maelfu ya watanzania wamekua maskini, hawana ajira, Hawa hawana vyama bali uchaguzi ni sehemu ya kupunguza hasira na mawazo
Pambana na maisha ya wananchi, CCM na Chadema hamfiki hata asilimia 11 ya watanzania
Sasa waziri Jafo jamii inakutazama kama kituko ambae hujui hatma ya maisha ya siasa zako za moto