Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Wakuu nimekuwa nikifatilia matamko mbalimbali kuanzia kwa Wakuu wa mikoa Mawaziri na watawala wa Ccm wote maelezo yao niyaubabe lakini majibu ya Kangi Lugola Bungeni yalinitoa machozi. "Chama cha upinzani kilichojitoa kwenye kinyang'anyiro ndio kinachochea vitendo vya vurugu zinazoendelea nchini, tutawashughlikia".

Leo Jafo kaitimisha kwa kuwarejesha watia nia wa upinzani wote walioenguliwa na vichaa (watendaji) kwa maelekezo ya boss wao.

Nchi mkaipeleka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ikichanganya msikimbie msubiri mpaka mwisho. View attachment 1259806
Eti walienguliwa na vichaa kwa maelezo ya boss wao. Inamaana boss wa vichaa bila shaka na yeye atakuwa sawa nao au kawazidi kidogo?
 
Nimecheka sana anavuja jasho mara mpira kwapani, anahangaika sana
Anaongea kwa kubabaika sana,hakutulia kabisa kitini...utadhani sio Yule chiriku tuliyemzoea..hahahahh
 
chadema wakishiriki , watakuwa wameumia .lakini ni wakati sasa ya kudai tume huru ya uchaguzi .... Mungu amesikia kilio cha chadema . wameonewa sana . Mungu akasema ngoja mpinzani wako ajichanganye hapo hapo ndiyo pa kukamatia ....tume huru ya uchaguzi ndiyo mpango mzima .Mchakato wa Uchaguzi uanze upya .

david cameron aliwahi kusema........Elections aren't about records, they're about plans and choices.
 
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametangaza kuwaruhusu wagombea wote waliochukuwa fomu na kuzirejesha kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania Novemba 24, 2019 wanaruhusiwa kushiriki uchaguzi huo na amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi Nchini kote ya kuwaengua wagombea wa vyama mbalimbali. Waziri Jafo ametoa uamuzi huu jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wanahabari leo.

Chanzo: Ukurasa wa OR-Tamisemi Facebook


Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza wenyeviti wa vijiji 6,248, wa mitaa 1169 na vitongoji 37,505 wanaotokana na CCM wamepita bila kupingwa baada ya kutojitokeza kwa wagombea kutoka vyama vya upinzani.


“Kwa upande wa vitongoji Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika vitongoji 37,505 kati ya vitongoji 64,384 sawa na asilimia 58,”

Amesema katika wajumbe wa kundi la wanawake jumla ya wajumbe 64,085 wamepita bila kupingwa na wajumbe kundi la mchanganyiko jumla ya wajumbe 75,560 wamepita bila kupingwa.

Maskini ya rabi wanahangaika kama vifaranga vilivyonyonyolewa manyoya ya mkiani. Jiwe anaharisha tu baada kuona janja ya nyani imeshitukiwa. Hakuna namna Mbowe, zitto, Lipumba, mbatia hakuna kurudi nyuma tena watajamba wakati huu. Ushenzi mtupu halafu wakirudi wakasimamiwe na wale waliowaengue Go to hell idiots Kuweni wenyewe mukwibe vizuri sasa hivi agiza train ya maji stupid
 
Wakati mwingine lazima tujiulize ,unapomfanyia ubaya mwenzako moyoni mwako unajisikiaje ,nilimsikiliza professor Lipumba ikisema haikuwa na maana yeyote kuandaa uchaguzi huu kama wahusika walijua kuwa haikuwa wa haki na huru
 
John Shibuda akiiasa CCM nanukuu " Nyama ya kitimoto hata uibadilishe jina au uitie viungo kibao vya kunukia na kuongeza ladha, bado itabaki kuwa haramu kwa wanaoamini" mwisho wa kumnukuu Mzee Shibuda.

CCM baada ya kunajisi katiba ya nchi na utaratibu wa vyama vingi kuelekea uchaguzi huu wa serikali za mitaa na vijiji, hata mje na kubadilisha gia za aina zote bado ni uchaguzi haramu.
 
Nilisoma mahali flani kuwa wale wote waliokatwa wanaruhusiwa kurejea kwenye kinyang'anyiro, hii itakuwa siyo kutoka kwa jafo direct but vigogo wa ccm wamekaa na kutafakari kwa undani (akiwepo head secretary dr. bashiru ambaye namuona hakubaliani na uamuzi ule) so wameona HAIBU.

Hakuna atakayeshitakiwa hapo, ndani ya chama au popote.
 
Siasa za ulaghai zimefika mwisho Wananchi hatudanganyiki tena

Mimi nilijua huu ni mchezo wa upinzani kuepuka aibu ya kushindwa

Wamenusa harufu ya uchapakazi wa Magufuli anavyokubalika kwa Wananchi wakaona njia ya kuepuka aibu ni kujitoa kwenye Uchaguzi

Ila kwa kuwa Serkali inamkono mrefu ikawa imenasa huo mtego

Wengine walikosea kujaza fomu makusudi ili wasipitishwe

Ningeomba serkali iwarudishe wote hata wale wasio jua kusoma na kuandika
Hili unalisema leo,muda woote ulikuwa wapi hivi ni kwann mtu ukiwa mfuasi wa chama cha kijani unakuwa na shida ya kufikiri?
 
Kumlaumu Jafo ni kumwonea yeye yupo kama TV tu.!
Aisee, hakuna dharau kubwa kuliko hii!

Umemtukana tusi baya sana; lakini ndio hivyo tena, mradi watoto wanaenda chooni, hakuna tusi lisiloweza vumilika kwa baadhi ya watu.
 
Back
Top Bottom