Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametangaza kuwaruhusu wagombea wote waliochukuwa fomu na kuzirejesha kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania Novemba 24, 2019 wanaruhusiwa kushiriki uchaguzi huo na amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi Nchini kote ya kuwaengua wagombea wa vyama mbalimbali. Waziri Jafo ametoa uamuzi huu jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wanahabari leo.
Chanzo: Ukurasa wa OR-Tamisemi Facebook
Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza wenyeviti wa vijiji 6,248, wa mitaa 1169 na vitongoji 37,505 wanaotokana na CCM wamepita bila kupingwa baada ya kutojitokeza kwa wagombea kutoka vyama vya upinzani.
“Kwa upande wa vitongoji Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika vitongoji 37,505 kati ya vitongoji 64,384 sawa na asilimia 58,”
Amesema katika wajumbe wa kundi la wanawake jumla ya wajumbe 64,085 wamepita bila kupingwa na wajumbe kundi la mchanganyiko jumla ya wajumbe 75,560 wamepita bila kupingwa.