Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiwa na mchecheto ndio akili inakuwa hivyo. Huo uchaguzi wa 2910 tutauangalia Jiwe akiwa malaika mpendwa upande ule wa pili kama atapita usaili. Kuna mtu kachanganyikiwa hapa.View attachment 1259801
Hilo tangazo wamechapisha wapinzani nini? Eti hapo ni Novemba 24, mwaka gani? Kama nimeona 2910. Naona dhambi inawatafuna sasa.
Kwa matusi haya usipopigwa ban basi moderators utakuwa ulishawaweka kiganjani!
Niliwaambia atazidi kuharibu nadhani mmeaminiKwa vyovyote vile atazidi kuharibu na kuchafua Hali ya hewa karirini maneno yangu.
Siasa za ulaghai zimefika mwisho Wananchi hatudanganyiki tena
Mimi nilijua huu ni mchezo wa upinzani kuepuka aibu ya kushindwa
Wamenusa harufu ya uchapakazi wa Magufuli anavyokubalika kwa Wananchi wakaona njia ya kuepuka aibu ni kujitoa kwenye Uchaguzi
Ila kwa kuwa Serkali inamkono mrefu ikawa imenasa huo mtego
Wengine walikosea kujaza fomu makusudi ili wasipitishwe
Ningeomba serkali iwarudishe wote hata wale wasio jua kusoma na kuandika
Mwenye masikio na asikieAman iwe nanyi wakuu
Naona vyama vya upinzani vikiwa vimeshikilia mpini wakati serikali imeshikilia makali
Polen sana ccm mlijifanya wahuni kumbe mbowe ndo mhuni zaid yenu
Msimamo wenu uendelee kuwa huo huo
Msikubali kujiingiza kwenye uchaguzi wa kijinga jinga namna hii
Usimtendee mwenzio mabaya
Shwain
LONDON BOY
Hivi hapo kati ya Mbowe na Jafoo nani kakurupuka?Mbowe amezungukwa na washauri wabaya
toka dr slaa aondoke amekuwa na maamuzi ya kukurupuka
Hahahaaaaa......!Wakati Suleimani Jafo (MB) Waziri wa nchi OR- TAMISEMI akiongea na waandishi wa habari leo Dodoma kuhusu kufuta maamuzi ya wasimamizi wenzake wa uchaguzi wa ngazi za chini, kuna jambo sioni likiongelewa na wadau hasa humu mitandaoni.
Jambo lenyewe ni hili, JAFO alikuwa akiongea kama kada wa CCM si kama msimamizi mkuu wa uchaguzi. maneno kama " wasiweke mpira kwapani, waje tuwapige, wasikimbie ulingoni waje tuwatandike" si maneno ya refarii nayetakiwa kuwa nutro hata kama ana timu yake. Piga picha Jaji Kaijage mwenyekiti wa NEC ndio anaongea hivi, tuombe asifike huko.
Maendeleo hayana vyama.
Nijambo la ajabu waziri wa Tamisemi idara yake kujichanganya hadi waziri anatoa tamko ,uchaguzi uendelee kwa wagombea kuendelea ,na mchakato wa uchaguzi
Hii ni ajabu ivi wasimamizi wa Mitihani wameisha sema baadhi ya wanafunzi wamekosa sifa za kufanya mitihani kwa vigezo husika au makosa ya hao wanafunzi
Sasa baadaye inagundulika kumbe ni fitina ya wasimamizi na kelele zimepigwa wale wanafunzi sasa warudi kufanya mitihani ,bila kujua wasimamizi wameondoa mood na ari ya kufanya mitihani hiyo
Nimuombe Jafo waswahili walisema ,akilinyingi huondoa maarifa ,jafo maarifa yametoka ,ukweli kuwaambia tena wagombea warudi tena kugombea ni kanakwamba umeisha jua kuwa ngoja waje ,tuwamalize kwa njia hii.
Jafo umetengeneza tatizo ,hill ni busara ujiuzulu ili mchakato uanze upya hapa imani haiko tena
Ukweli wapinzani kukubali kurudi wataonekana sio wajinga tu bali wapumbavu na waoga.
Jiuzuru Raisi ateue waziri mwingine aje aendeshe zoezi hili.
Jafo umeaibisha Taifa,umumuchonganisha ,Raisi na wananchi kuwa yy hapendi wananchi wake.hii ni hatari
Kumbe ni hii Incapacity ya Jafo ameshindwa.
Jafo hajawahi kuwa mwadilifuWakati Suleimani Jafo (MB) Waziri wa nchi OR- TAMISEMI akiongea na waandishi wa habari leo Dodoma kuhusu kufuta maamuzi ya wasimamizi wenzake wa uchaguzi wa ngazi za chini, kuna jambo sioni likiongelewa na wadau hasa humu mitandaoni.
Jambo lenyewe ni hili, JAFO alikuwa akiongea kama kada wa CCM si kama msimamizi mkuu wa uchaguzi. maneno kama " wasiweke mpira kwapani, waje tuwapige, wasikimbie ulingoni waje tuwatandike" si maneno ya refarii nayetakiwa kuwa nutro hata kama ana timu yake. Piga picha Jaji Kaijage mwenyekiti wa NEC ndio anaongea hivi, tuombe asifike huko.
Maendeleo hayana vyama.
Kumbe yeye ndiye atoae ruhusa!!?Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametangaza kuwaruhusu wagombea wote waliochukuwa fomu na kuzirejesha kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania Novemba 24, 2019 wanaruhusiwa kushiriki uchaguzi huo na amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi Nchini kote ya kuwaengua wagombea wa vyama mbalimbali. Waziri Jafo ametoa uamuzi huu jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wanahabari leo.
Chanzo: Ukurasa wa OR-Tamisemi Facebook
Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza wenyeviti wa vijiji 6,248, wa mitaa 1169 na vitongoji 37,505 wanaotokana na CCM wamepita bila kupingwa baada ya kutojitokeza kwa wagombea kutoka vyama vya upinzani.
“Kwa upande wa vitongoji Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika vitongoji 37,505 kati ya vitongoji 64,384 sawa na asilimia 58,”
Amesema katika wajumbe wa kundi la wanawake jumla ya wajumbe 64,085 wamepita bila kupingwa na wajumbe kundi la mchanganyiko jumla ya wajumbe 75,560 wamepita bila kupingwa.
Ukweli mtupu !!Aman iwe nanyi wakuu
Naona vyama vya upinzani vikiwa vimeshikilia mpini wakati serikali imeshikilia makali
Polen sana ccm mlijifanya wahuni kumbe mbowe ndo mhuni zaid yenu
Msimamo wenu uendelee kuwa huo huo
Msikubali kujiingiza kwenye uchaguzi wa kijinga jinga namna hii
Usimtendee mwenzio mabaya
Shwain
LONDON BOY