Waziri Jafo: Wagombea wote walioondolewa kwa kuonewa haki itatendeka na watarejeshwa kwenye uchaguzi

Waziri Jafo: Wagombea wote walioondolewa kwa kuonewa haki itatendeka na watarejeshwa kwenye uchaguzi

Wasalaam, wengi tulitegemea hizi sarakasi kuelekea uchaguzi serikali za mitaa hawa watendaji waliitwa nyumba nyeupe na kuelekezwa wafanye wanayofanya kukimbia ofisi, kufunga ofisi na kukata majina ya wagombea wa upinzani ili ccm wapite bila kupigwa.

Kauli ya waziri jaffo kwamba mabaraza ya rufaa yasikilize rufaa na ikibidi yawarejeshe wagombea wa upinzani ni mtego na propaganda za kitoto kwani hakuna haki itakayopatikani zaidi ya kupotezeana muda kwani ccm ilishazamiria kupora vijiji na vitongoji vyote vilivyo chini ya upinzani baada ya uchaguzi huo. Wote mnakumbuka kauli ya jaffo hapo juzi kwamba figisu ktk chaguzi ni kawaida dunia nzima.

Wito wangu kwa vyama vya upinzani msihangaike kukuta rufaa mnapoteza muda na pesa zenu kwani hakuna mpinzani ataeshinda uchaguzi huo wa Nov 24 watashinda ccm kwa ubabe, dawa pekee ni kususia uchaguzi huo na chaguzi zote zijazo mpaka itapoundwa tume huru ya uchaguzi.
Ova.
 
Rais magufuli naomba ujue kuwa nchi ikitawaliwa na chama kimoja na serikali yako ikisaidia kuua upinzani jua kuwa unaenda kutengeneza upinzani mkubwa ambao unaitwa UMA WA WATANZANIA(tembo) kwa kuua vyama vya siasa pinzani(sisimizi)
.
Wananchi wenyewe ndio wanaua upinzani kwa sababu wameona kuwa Rais wetu amemaliza yote.
 
Waziri wa Tamisemi mh Jaffo amesema wagombea wote wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao wameondolewa lakini wamekata rufaa malalamiko yao yatasikilizwa na haki kutendeka na kama wameonewa basi watarejeshwa uchaguzini.

Chanzo: ITV habari

Hizi ni habari njema kwa wapinzani ukizingatia ukweli kuwa waziri Jaffo ni muumini mzuri wa dini ya Haki.

Maendeleo hayana vyama!
CCM hakuna muumini mzuri wa dini ya haki, wote ni walewale wanatengeneza tatizo kisha wanajitokeza eti kutatua tatizo.
 
Usizugike na hao wanaompigia promo kwa sababu wana acces na media ila waliowengi ni wana jelous na jamaa ndo wamefungwa mdomo.
Wananchi wenyewe ndio wanaua upinzani kwa sababu wameona kuwa Rais wetu amemaliza yote.
 
Ccm wanafanya udhalimu hadi wanajishitukia! Washenzi kweli hawa.
 
Hili suala halina afya kwa Taifa wala CCM yenyewe. Mara mia mngesubiri mkaiba kura kama utaratibu wenu ulivyo ( nyie ni majizi kwa asili) kuliko mlichokifanya.
Kupandikiza chuki katika level ya mtaa ambapo watu ni wachache, wanajuana, wengine ni ndugu n.k, hamjatafakari vya kutosha. Mnaleta utengano wa hatari.
Mjitafakari.
 
Kufuatia magazeti mengi ya leo kuripoti wagombea wengi sana wa vyama mbalimbali kupita bila kupingwa ni wazi na dhahiri kuwa gharama za uchaguzi zimepungua " sana"

Je, waziri wa Tamisemi mh Jafo unaweza kutujulisha katika wakati muafaka huu uzalendo wa wagombea kupita bila kupingwa umeliokolea taifa kiasi gani cha fedha?

Ni hako kaswali tu,
Maendeleo hayana vyama!
 
Pesa itafanya matumizi mengine. Sio jukumu lako kujua
 
1573115432990.jpeg
 
Kwa hiyo wale waandishi wa wapiga kura watarudisha hela kwa zile sehemu ambazo CCM wamepita bila kupingwa?
Kufuatia magazeti mengi ya leo kuripoti wagombea wengi sana wa vyama mbalimbali kupita bila kupingwa ni wazi na dhahiri kuwa gharama za uchaguzi zimepungua " sana"

Je, waziri wa Tamisemi mh Jafo unaweza kutujulisha katika wakati muafaka huu uzalendo wa wagombea kupita bila kupingwa umeliokolea taifa kiasi gani cha fedha?

Ni hako kaswali tu,
Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom