Waziri Jafo: Wagombea wote walioondolewa kwa kuonewa haki itatendeka na watarejeshwa kwenye uchaguzi

Waziri Jafo: Wagombea wote walioondolewa kwa kuonewa haki itatendeka na watarejeshwa kwenye uchaguzi

Kufuatia magazeti mengi ya leo kuripoti wagombea wengi sana wa vyama mbalimbali kupita bila kupingwa ni wazi na dhahiri kuwa gharama za uchaguzi zimepungua " sana"

Je, waziri wa Tamisemi mh Jafo unaweza kutujulisha katika wakati muafaka huu uzalendo wa wagombea kupita bila kupingwa umeliokolea taifa kiasi gani cha fedha?

Ni hako kaswali tu,
Maendeleo hayana vyama!
Wagombea wengi sana wa vyama mbalimbali kupita bila kupingwa. Nimeipenda hiyo tu.
 
kila kituo cha kuandikisha ndani ya kitongoji sh 40,000 zidisha mara kama 30,000+
 
1.Hivi kweli wapinzani tu ndo hawakujui kujaza fomu za kugombea Tanzania nzima?
2.Kwanini hakuna hata mgombea 1 wa CCM aliyekosea kujaza fomu nchi nzima?
3. Kwanini hakuna mgombea hata 1 wa CCM alielalamika kunyimwa fomu na watendaji isipokua wapinzani pekee?
4.Kwann baada ya wapinzani kujitoa CCM wanawatisha wapinzani eti wana lengo na nia mbaya? Kwani si ndo wangeshangilia kushinda kwa asilimia 100? Kwann wanateseka? Kuna nn nyuma ya pazia?
Ukisikiliza utetezi wa Jafo unaweza kukufuru bora kukaa kimya tu. Ni sawa na timu iliyosajili wanasoka ghali na mishahara minono lakini inahonga waamuzi na kutumia uchawi ili kushinda mechi.Galagabaho kabsa!!
 
Siku Ya Kufanya Nyani Miti Yote Huteleza
Ccm Pekee Yake Inapiga Penati Golini Hakuna Mtu😀😁😂😃😅😅
 
Nimeamua nitaenda getini magogoni na sumu ya panya nakunya mchana kweupee kuiachia hii serikali laana. Na walele walinzi wakija kunishika faster nakunywa hiyo huku nikitema matusi ya hatarii.

TUMECHOKA liwalo na liwe tu.

Mbrrrrrrrrr!
Utakufa kwa maumivu
Sumu ya panya haikuui hapo hapo
 
Soka la bongo kikosi ni Cha milioni kadhaa mishahara ghari ,kambi ghari nje ya nchi

Halafu wanahonga refa na mganga

Sasa ndio wanafanya Nini ?

Same to siasa za bongo
 
Waziri Jafo amejishushia sana hadhi! Watanzania wa sasa siyo wajinga kihivyo. Wanatambua kinachoendelea nchini.

Bora hata ya akina sisi ambao tulisoma alama za nyakati mapema, na hivyo kutokujiandikisha kabisa kwa ajili ya huo mchakato haramu.
 
Utaumiza kichwa bure, tumeshasahau kama kuna uchaguzi tupo bize shambani kuilisha Tanzania, karibu kwenye kilimo.
 


Awali ya yote nilipenda nichukue nafasi hii kuishutumu serikali chini ya waziri Jafo kushindwa kujibu fedhea inayo tolewa na hawa wahuni wasio taka kuishi kwa amani na wananchi wenzao kwa makusudi ya kutaka kuitia dosari serikali na chama cha CCM.

Vutendo hivi vya fedhea vinavyo letwa na vyama vya upinzani dhidi ya serikali vilitakiwa vijibiwe vikali kwa njia ya kuwadhalilisha.
Nisinge sikitika kama serikali nayo inge weka bayana makosa ambayo wagombea wao wame yafanya mpaka kung'olewa au kutenguliwa ugomnea wao ili wananchi na hasa ushabiki wao waone mambo yaliyotokea.

Kitendo hiki cha serikali kukaa kimya na mda wote kuwashauri wapinzani waende kwenye halimashauri ya rufaa wakakate rufaa kama wana ona hawaja tendewa haki, hiyo mimi naona haitoshi. Hii mishetani yenye lengo la kutaka mambo kirahisi rahisi, ingekuwa busara nao kuwaumbua kama wao wanavyo jitahidi kutumia nguvu nyingi kutaka kuwa aminisha wananchi na ulimwengu kwa ujumla kuwa serikali inawanyima haka kwa kuminya demokrasia, kwa kuwaonyesha wananchi hizo formu zao walizo zijaza na makosa waliyo yatenda.

Hii mijitu ina vyombo vyao vinavyo wasaidia kuidhohofisha serikali yetu ikiwemo; BBC, VOA na DW mitandao mingine ya kijamii na online TVs. Hii mitandao ya lugha ya kiswahili imewekwa rasmi kwa lengo moja tu, nalo ni kuliangusha taifa letu. Sioni sababu na faida nyingine zaidi ya hilo. Habari zao nyingi ni zile za kusaidia wapinzani kutuaminisha sisi kuto kuwa na imani na serikali yetu.

Mambo mazuri yanayo fanywa na serikali kwa ajili ya maendeleo yetu, hii mitandao haiipi kipao mbele katika kuitangaza. Kama kuna kitu ambacho wazungu wanakitumia kutumia sana katika mikutano yao inayo husu maendeleo ya uchumi wa bara la Afrika basi ni neno RUSHWA. Hata hivyo naona ajabu sana hii mitandao wala haiwaabarishi chochote wana ulimwengu kuhusu jitihada ambazo zime fanywa na serikali hii ya kupunguza kwa kiasi kikubwa sana rushwa na pia matumizi ya madawa ya kulevya.

Kwa hali hiyo naomba serikali iwe makini sana na hawa watu. Hawa watu wanaonekana walikuwa wamesha jiandaa na kujipanga kwa makusudi kufanya hivyo na ndiyo maana hawa kujishughulisha na mchakato mzima wa kuwafundisha wagombea wao jinsi ya kujaza hizo formu kulingana na maelezo yaliyo tolewa na serikali kama CCM ilivyo fanya.

Zaidi ya hayo mimi siamini kuwa wao ni wajinga kiasi hicho mpaka wagombea wao wengi wakashindwa kuzijaza hizo formu kisahihi. Naona hiyo ilikuwa mpango wao kususia huo uchaguzi na kujaribu kuwahiniza wananchi kuto toa ushirikiano kwa serikali yao.

Hiyo inaonyesha dhahiri kuwa lengo lao ni kuwapa wasiwasi wananchi kuto kuwa na imani na serikali yao kwa malengo ya kuidhohofisha Serikali.

Wapinzani wanajua uwezo ambao Rais Magufuli ameuonyesha kwa wananchi wake na wanajua dhahiri kuwa hawana uwezo wa kui beat CCM, ndiyo maana wana fanya kila hila kuidhoofisha serikali ili ipoteze imani kwa wananchi wake.

Waziri Jafo na Naibu waziri Mwaitara na nyie chukueni hatua kubwa kwa miaka ya serikali za kuwaanika hayo majingili hadharani, kama inawezekana, kama mlivyo fanya kwa akina Kinana, Nape, Ngeleja, Membe na Makamba senior na junior, vinginevyo hawatawaelewa hao.

Watu wengi wamesha sema sana kuwa mambo ambayo hawa wahuni wanayafanya dhidi ya serikali yetu na bunge letu tukufu na pia Taifa letu sio matendo ya kiupinzani wa vyama bali ni hujuma dhidi ya Taifa letu. Haya majangili yamekuwa militant na wako tayari kutumia kila njia kuliangamiza Taifa letu kwa maslahi yao na mabeberu wao.
 
Dah, ndugu yangu nimekuelewa sana, lakini naomba utafakari kwa umakini sana na ufanye utafiti wa kina then urejee huku uandike. Binafsi baada ya kusikia hii taarifa ilibidi nizunguke karibia kwenye vituo vyote ndani ya tarafa tu mbili yalikotundikwa majina ya wagombea wenye sifa na wasiyo na sifa, kilicho nishangaza ni kwamba.

Wagombea wote kutoka vyama Pinzani wote wameenguliwa kwa kuwa hawana sifa na hawakukidhi vigezo.....wagombea wote kutoka chama Tawala wameteuliwa kwa kuwa wamekidhi vigezo.

Mungu ndiye shaihidi wa haya Mambo naamini hiki kitu HAKIWEZEKANI kabisa, lakini nikukumbushe kuwa Watendaji wa Vijiji/kata nk hawa ndiyo wahusika wakuu.

Unapaswa utambue kuwa hawa viongozi tunaishi nao, tunapanga nao, ni wenza wetu, ni marafiki zetu, ni washkaji zetu,nk si wote watakuwa watiifu wenye utashi kwa serikali bali ni watiifu kwa kulinda vibarua vyao.

Yanayotokea ni miongoni mwa maelekezo waliyopewa na wakubwa wao. Siwezi kuingia jukwaani kuongopa mimi ni mtu mzima, sina u CCM wala u CHADEMA, japo namkubali sana Rais Magufuli na timu yake. Lakini nakumbuka sana kipindi cha kuandikisha wapiga kura sote tulijionea yaliyotoke.

Nilishuhudia Afisa Utumishi wa Halmashauri moja anaomba magari ya halmashauri ili yasaidie kusomba wanafunzi kutoka shuleni kwenda kujiandikisha.

HAPA MTU MWENYE AKILI TIMAMU lazima ahoji hili jambo...Pia baadhi ya watumishi walitumiwa SMS za vitisho kutoka kwa wasimamizi wao kuwa endapo hawataenda kujiandikisha basi watachukuliwa hatua za kinidhamu.

HAPA MWENYE AKILI TIMAMU lazima ahoji hili jambo hivyo mleta uzi huu siwezi kukubaliana na wewe kuwa wapinzani wote ni mbumbumbu na CCM wote wanauledi kuliko wengine

HAPA MWENYE AKILI TIMAMU lazima apatwe na wasiwasi.
 
Haya matumizi ya lugha iliyosheheni maneno makali na yasiyokuwa na staha ni yenye lengo gani hasa? Maneno kama mijitu, mashetani, wahuni n.k hivi yanapaswa kutumika ktk jukwaa kwa hili ili kufikisha maudhui?

Hata kama upinzani umesusia uchaguzi, lkn si ndiyo faraja kwa wakereketwa wa chama tawala? Sasa hili povu lenye lugha zenye kujaa mihemuko ni la nini sasa?
 
Mtoa mada huyu maneno meier amejidhihirisha alivyo punguani, mhuni, mpumbavu na mbumbumbu. Angetoa hoja kiungwana angeeleweka lakini lugha alizoweka ndo zinamchora alivyo.
 
Dah, ndugu yangu nimekuelewa sana, lakini naomba utafakari kwa umakini sana na ufanye utafiti wa kina then urejee huku uandike. Binafsi baada ya kusikia hii taarifa ilibidi nizunguke karibia kwenye vituo vyote ndani ya tarafa tu mbili yalikotundikwa majina ya wagombea wenye sifa na wasiyo na sifa, kilicho nishangaza ni kwamba...Wagombea wote kutoka vyama Pinzani wote wameenguliwa kwa kuwa hawana sifa na hawakukidhi vigezo.....wagombea wote kutoka chama Tawala wameteuliwa kwa kuwa wamekidhi vigezo......Mungu ndiye shaihidi wa haya Mambo naamini hiki kitu HAKIWEZEKANI kabisa, lakini nikukumbushe kuwa Watendaji wa Vijiji/kata nk hawa ndiyo wahusika wakuu. Unapaswa utambue kuwa hawa viongozi tunaishi nao, tunapanga nao, ni wenza wetu, ni marafiki zetu, ni washkaji zetu,nk si wote watakuwa watiifu wenye utashi kwa serikali bali ni watiifu kwa kulinda vibarua vyao...yanayotokea ni miongoni mwa maelekezo waliyopewa na wakubwa wao. Siwezi kuingia jukwaani kuongopa mimi ni mtu mzima, sina u CCM wala u CHADEMA, japo namkubali sana Rais Magufuli na timu yake. Lakini nakumbuka sana kipindi cha kuandikisha wapiga kura sote tulijionea yaliyotoke.....nilishuhudia Afisa Utumishi wa Halmashauri moja anaomba magari ya halmashauri ili yasaidie kusomba wanafunzi kutoka shuleni kwenda kujiandikisha.....HAPA MTU MWENYE AKILI TIMAMU lazima ahoji hili jambo...Pia baadhi ya watumishi walitumiwa SMS za vitisho kutoka kwa wasimamizi wao kuwa endapo hawataenda kujiandikisha basi watachukuliwa hatua za kinidhamu....HAPA MWENYE AKILI TIMAMU lazima ahoji hili jambo...hivyo mleta uzi huu siwezi kukubaliana na wewe kuwa wapinzani wote ni mbumbumbu na CCM wote wanauledi kuliko wengine...HAPA MWENYE AKILI TIMAMU lazima apatwe na wasiwasi.
Na ndiyo maana ukisoma paragraphs zangu hizi utaelewa nini nimemaanisha. Hata mimi sitaki kuamini kuwa wapinzani wamekuwa wajinga ki hivyo, kiasi kwamba wagombea wao wote wakatenguliwa!

Hapa nadhani kulikuwa na nia fulani mbovu ambayo wahusika wa maswala haya wanaweza kutupa majibu sahihi.

Siamini siamini kama hiki kitu ki.ekuwa hivyo!

Kwa hali hiyo naomba serikali iwe makini sana na hawa watu. Hawa watu wanaonekana walikuwa wamesha jiandaa na kujipanga kwa makusudi kufanya hivyo na ndiyo maana hawa kujishughulisha na mchakato mzima wa kuwafundisha wagombea wao jinsi ya kujaza hizo formu kulingana na maelezo yaliyo tolewa na serikali kama CCM ilivyo fanya.

Zaidi ya hayo mimi siamini kuwa wao ni wajinga kiasi hicho mpaka wagombea wao wengi wakashindwa kuzijaza hizo formu kisahihi. Naona hiyo ilikuwa mpango wao kususia huo uchaguzi na kujaribu kuwahiniza wananchi kuto toa ushirikiano kwa serikali yao.

Hiyo inaonyesha dhahiri kuwa lengo lao ni kuwapa wasiwasi wananchi kuto kuwa na imani na serikali yao kwa malengo ya kuidhohofisha serikali.

Wapinzani wanajua uwezo ambao Rais Magufuli ameuonyesha kwa wananchi wake na wanajua dhahiri kuwa hawana uwezo wa kui beat CCM, ndiyo maana wana fanya kila hila kuidhoofisha serikali ili ipoteze imani kwa wananchi wake.
 
Back
Top Bottom