Hili nalo nendeni mkalitizame
 

Attachments

  • AE8E6D33-FE18-4EE1-BD44-687325AAE656.jpeg
    55 KB · Views: 2
 

Attachments

  • 81B73FD1-D58C-4BA5-AC76-1E1A537AFE74.jpeg
    134.4 KB · Views: 2
Watanzania tukilalamika kuwa hili dili la mkataba wa bandari lina kila aina ya ukakasi muelewe.

Taarifa za uhakika na za kweli kabisa ni kuwa kampuni ya DP World tayari ipo bandarini, kitengo cha makontena na wanafanya kazi kwa siku nyingi tu kabla hata ya Mkataba wa Msingi haujapelekwa bungeni.

Mfumo wanaotumia ni single window service na sherehe za uzinduzi wa shughuli zao haps nchini ilifanyika Hyatt Hotel(Kilimanjaro hotel ya zamani) miezi kadhaa iliyopita.

Maswali tunayoiuliza serikali ni haya yafuatayo:

1. Mosi kwa nini serikali mpaka leo imetuficha kuwa kampuni ya DP world tayari imeshaanza kazi hapo bandari ya Dar es salaam kabla ya hiyo mikataba ya HGA haijasainiwa?

2. Au je tayari mikataba ya HGA imeshasainiwa kimyakimya ila haijatueleza au inatudanganya?

3. Je hao DP World watafanya kazi hapo kitengo cha makontena kwa miaka mingapi?

Inaelekea serikali inapata kigugumizi kushughulikia mkataba huu wa KUUZA NCHI kwa sababu tayari DP World tayari wameshaestablish fact on the ground.

Serikali ilete majibu.
 
Ni kweli, kwasababu ile MoU inaonekana wazi kabla haijapelekwa bungeni kupitishwa, tayari hao waarabu walishaanza shughuli zao tangu October 2022 kama ilivyoandikwa kwenye ule mkataba, hiyo kwa maana nyingine ni kwamba, bunge lilipitisha ule mkataba huku waarabu tayari wakiwa field.

Zaidi, hata sishangai kwanini waarabu wanajiamini kiasi hicho, wanafanya hivyo makusudi wakijua fika ndani ya ule mkataba, tumewapa uhuru wakufanya wanavyotaka, au niseme tumewapa mamlaka kamili ya kujitawala wakiwa ndani ya Tanganyika yetu, kwenye zile "Exclusive Rights" tulizowapa ndani ya ule mkataba, ndio maana hata siwashangai wakizipiga teke sheria na taratibu zetu.

Hapo ndio tayari tumeshageuzwa watumwa ndani ya Tanganyika yetu, Samia ametudhalilisha sana watanganyika, ametudharaulisha, ameutweza utu wetu mbele ya wajomba zake wa uarabuni kwa vizazi vyote vijavyo vya hili taifa, haaminiki tena.
 
Amini nawambia CCM watafika mahali hawataweza tena kutumia ubabe ktka level ya URAIS bali itawabidi wakubali wananchi wamchague wamtakae halafu wao watajua namna ya kubanana huko na rais wao.
 
Hii serikali ni ongo
Kassim Majaliwa ni muongo
Spika ni Muongo
Na Samia ndiye kubwa la waongo

Mnatuambia kuwa tusubiri mikataba ya HGA wakati mwarabu tayari yuko bandarini anafanya kazi?

Hivi nyie mnatuchukuliaje?
 
Hii serikali inafanya kazi kwa manufaa ya nani? Mbona wanadharau wananchi sana!
 
Mazuzu yanashangilia eti anaupiga mwingi huku akiwaibia wanyonge
 
Kuna vinara hapo ccm wakifa, Ngoma zitachezwa na sherehe kubwa zitafanywa kwa sababu tu kafa adui wa wananchi na Tanganyika yetu

Kuna sababu gani ya wananchi kutofanya sherehe hizo wakati wanaona kabisa mateso wanayosababishiwa na viongozi wa ccm?

Tanzania imepewa mtihani mkubwa sana, kuwepo dude linaitwa CCM!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…