Wazungu/West wako mbali sana, wamefikia hadi kwenye supu ya box/kopo!

Wazungu/West wako mbali sana, wamefikia hadi kwenye supu ya box/kopo!

Nani kakuambia vyakula vya kopo vina sumu?? Mbona huko wanakoishi kwa hivyo vyakula vya makopo ndio wana life expectancy kubwa zaidi? Kama ni sumu kwa nini wastani wao wa maisha ni mkubwa sana kutuzidi sisi??
Life expectancy yao inasogezwa na maendeleo ya nyanja ya matibabu, lakini sio afya, watu wanapigwa maboost ya kuedelea kuishi, serikali zao zinahaha kuwaomba wajaribu kula lishe bora, ambayo ni gharama ya kununua, na kupika mwenyewe, watu huko wanakalukuleti mpaka kupika nyama au mboga za majani inakula umeme au gesi kiasi gani
Na vyakula vya lishe bora, huko wanaita organic, vinakuwa bei mbaya
Narudia ni mpaka mfike huko na kuishi nao, ndio mtajua,
 
Vyakula vya Makopo vina sumu
Upo sahii 1000%
Chumvi peke yake-ni sumu.
Na mkimuuliza mleta Uzi huu ageuze haya makopo, utaona lishe iliyokuwa na asilimia kubwa, ni Chumvi-Sodium.

Kutumia Chumvi nyingi kwenye chakula husababisha mishipa ya damu kukauka yani inakuwa 'brittle' (for lack of a better word) na hivyo kusababisha mishipa hiyo kupasuka na madhara yakr ni ulemavu ama kifo. Hatahivyo haijalishi hapa.
na huko wanakula maskini, vyakula vya asili wanakula wenye uwezo....
Ni kweli kabisa kuhusu 'masikini', kula vyakula vya makopo na ni kweli ni wenye uwezo ndio wanaokula vyakula Fresh(asili?)

Usisahahu

Mazao yetu ndio inayowalisha Mabilionea Duniani na hata wale wenye Ufunuo na elimu juu ya kula Vyakula vyenye virutubisho ambavyo havijachakachuliwa na makemikali.

Vilevile... vilivyochakachuliwa...
Kuanzia vyakula vitokanavyo na mbegu za GMO seed, kusindikwa na vyakula vinavyo mwagiliwa mavi ya watu(wanatumia mavi ya watu kama mbolea)-sasa hivi. New Technology ati...🤔

By the way, Sasa hivi hata nyama za makopo zinatoka kwenye mahabara. Nyama inaota kwenye maabara! Kuku hana kichwa wala miguu na Ng'ombe vilevile!

Anyways

Vile wanavyozalisha kwa mbegu za GMO wenyewe, ndio hivi wanaviweka kwenye makopo kwa sababu mazao yao yanayotokana na mbegu za GMO huharibika haraka.

Hivi sasa, Marekani wana kampeni kubwa sana ya kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kula vyakula Fresh-yaani "Unprocessed foods" Kwa sababu gani?

Ni kwa sababu wameshagundua vyakula vilivyochakachuliwa vinapoteza lishe(natural Nutrients) na hayo makemikali wanayotumia hueza sababisha cancer..... hata Flavor pia duh.

Na ndio maana kwenye hayo makopo unaeza ona...Vitamin Added Added Flavor etc....itoshe hata hiyo Flavor ya chakula sio Natural(Asili) inatengenezwa kwenye Mahabara🙌🏾Sumu tupu.

Nitakula matembele yangu, kha

====================

Huyu mleta mada hatutakii Watanzania afya njema wala hayo maendeleo. Yeye nikutukuza Wazungu tyu.
 
Magharibi wana supu zilizofungashwa kwenye box na makopo kama juice! Yani unanunua supu unaenda kupasha tu unakunywa, hakuna haja ya kupoteza muda kuchemsha nyama masaa ukitafuta supu.
Ki[pofu aliyeona punda.

Unaloliona kwa mara ya kwanza unafikiri ndiyo kwanza limeanza.

Hayo mammbo yapo zamani, miaka mingi sana nyuma, kinachobadilika ni ubunifu na vifunganishi tu.s,

Tanzania tulikuwa ytuna kiwanda kinatengenezz beef ya kopo, unaifunguwa unakula tu au ukipenda kuiongezea fundi, kazi kwako. Hiyo ilikuwa 60. Kiwanda kilikuwa pale Kawe, kinaitwa Taganyika Packers, kikataifishwa na nyerere. kikashindwa kuendeshwa, kikafa, mpala leo hii tunaona badala ya kiwanda kimekuwa uwanja wa wajinga ndiyo waliwao.
 
Life expectancy yao inasogezwa na maendeleo ya nyanja ya matibabu, lakini sio afya, watu wanapigwa maboost ya kuedelea kuishi, serikali zao zinahaha kuwaomba wajaribu kula lishe bora, ambayo ni gharama ya kununua, na kupika mwenyewe, watu huko wanakalukuleti mpaka kupika nyama au mboga za majani inakula umeme au gesi kiasi gani
Na vyakula vya lishe bora, huko wanaita organic, vinakuwa bei mbaya
Narudia ni mpaka mfike huko na kuishi nao, ndio mtajua,
Waambie.
 
Hii mnayoita supu kibongo ndio broth sasa. Soup/supu halisi kizungu inawekwa mazagazaga kama yote(karoti, vitunguu, hoho, njegere, french beans n.k)
Wewe hujui supu ya bongo; ni mchuzi pamoja na nyama iliyoungwa chumvi, limao na pilipili. Nyama hiyo inaweza kuwa ni utumbo, makongoro, nofu la kawaida, mbavu au hata maharage. Lakini broth ni mchuzi ambao haujaungwa chochote, hivyo hiyo siyo supu ya kibongo kabisa. Inatengezwa kwa kuchemsha nyama na maji ndani ya sufuria halafu huo mchuzi unaopatikana ndiyo broth yenyewe. Wanaufungwa kwenye vacuum kusudi usiharibike.
 
Kuna meneja mmoja wa KFC alitoa siri bila kujijua kwa kiherere chake
Kawaida wale kuku wanachanganya na unga wenye viungo mbali mball wanaita spices, halafu wanaokwa kwenye jiko, katika kuoka huo unga ukiwa na mchanganyiko wa damu na mafuta ya kuku huwa unapukutika, wenyewe wanaita "crumbs"
Sasa akajichanganya na kusema haya ma scrumbs huwa wana ya chemsha na kuyakoroga kutengeneza mchuzi unaiitwa "GRAVY",
Duuuhhhh,!!!
Nchi nzima ikawa breaking nyuuuuzi!
Hawakupenda kabisa......

Wewe hujui supu ya bongo; ni mchuzi pamoja na nyama iliyoungwa chumvi, limao na pilipili. Nyama hiyo inaweza kuwa ni utumbo, makongoro, nofu la kawaida, mbavu au hata maharage. Lakini broth ni mchuzi ambao haujaungwa chochote, hivyo hiyo siyo supu ya kibongo kabisa. Inatengezwa kwa kuchemsha nyama na maji ndani ya sufuria halafu huo mchuzi unaopatikana ndiyo broth yenyewe. Wanaufungwa kwenye vacuum kusudi usiharibike.
Kuna wabongo wengi tu wanachemsha nyama hawaungi na chochote, hawaweki chumvi, limao au pilipili. Mnachoita mchemsho ndio soup kwa wazungu, mnachoita supu nyie ni broth, hata mzungu akinunua broth anaweka chumi, limao na pilipili akipenda.
 
Ki[pofu aliyeona punda.

Unaloliona kwa mara ya kwanza unafikiri ndiyo kwanza limeanza.

Hayo mammbo yapo zamani, miaka mingi sana nyuma, kinachobadilika ni ubunifu na vifunganishi tu.s,

Tanzania tulikuwa ytuna kiwanda kinatengenezz beef ya kopo, unaifunguwa unakula tu au ukipenda kuiongezea fundi, kazi kwako. Hiyo ilikuwa 60. Kiwanda kilikuwa pale Kawe, kinaitwa Taganyika Packers, kikataifishwa na nyerere. kikashindwa kuendeshwa, kikafa, mpala leo hii tunaona badala ya kiwanda kimekuwa uwanja wa wajinga ndiyo waliwao.
Wewe mujahideen hakuna chochote cha maana ulichoandikia hapa, sijazungumzia nyama ya kopo, shida yako ilikuwa kuwashwawashwa kumtaja Nyerere tu ndio usikie raha.
 
Mbona hizo "supu" za kopo zipo kwenye supermarket nyingi za bongo tena kwa miaka mingi ? Au mimi ndio sielewi
 
Life expectancy yao inasogezwa na maendeleo ya nyanja ya matibabu, lakini sio afya, watu wanapigwa maboost ya kuedelea kuishi, serikali zao zinahaha kuwaomba wajaribu kula lishe bora, ambayo ni gharama ya kununua, na kupika mwenyewe, watu huko wanakalukuleti mpaka kupika nyama au mboga za majani inakula umeme au gesi kiasi gani
Na vyakula vya lishe bora, huko wanaita organic, vinakuwa bei mbaya
Narudia ni mpaka mfike huko na kuishi nao, ndio mtajua,
Wewe acha porojo zako, hata Tanzania hamli organic foods na sio kila mtu ana huo muda wa kununua na kupika mwenyewe kila mlo. Supermarkets za West zimejaa vyakula vya kila aina kutoka mashambani, vingine hata wewe hujawahi kuviona dunia hii na watu wanapika kuliko hata wewe mbantu.
 
Kuna wabongo wengi tu wanachemsha nyama hawaungi na chochote, hawaweki chumvi, limao au pilipili. Mnachoita mchemsho ndio soup kwa wazungu, mnachoita supu nyie ni broth, hata mzungu akinunua broth anaweka chumi, limao na pilipili akipenda.
Hujawahi kula supu la kitanzania bali unalisikia tu. Ningali kijana tulikuwa tukiamka na hangover tunakwenda kwa mangi wa supu; bakuli moja tu linakutoa kijasho chembamba na hangover yote inakatika. Broth haiwezi kufanya hivyo; in fact mimi hupikia sana broth kama kiungo kimojawapo kwenye nyama nikitaka kula ugali. Borth ni majimaji tu!
 
Fika Ulaya au Marekani agiza supu ndio utajua hujui.
 
Wapo mbali kwenye kula sumu na vyakula vya Makopo?

Mtazamo wako unashangaa kwakweli
Wanakula sumu? Vyakula vyao vina viwango vya hali ya juu, viko regulated sana. Na wanaishi kwa muda mrefu sana. Ukifa na 70 unaonekana umekufa mapema.
 
Fika Ulaya au Marekani agiza supu ndio utajua hujui.
Mimi naishi Marekani kwa miaka 30 sasa; kwa hiyo najua ninachosema. Broth inatunzwa kwenye friji (refrigerator), wakati soup inatunza kabatini (pantry) tu. Nikijadili kwa kiswahili kizuri hapa usidhani niko Igalula; hapana, ndiko ndani ya USA. JF hunipa nafasi nzuri sana ya kutumia kiswahili changu kwani nikishatoka JF huwa situmii kiswahili tena.
 
Back
Top Bottom