Wengi wanaopiga kelele kuhusu bandari ni wapitisha mizigo kimagendo bandarini

Kwa ni usiseme serikali imeshindwa! Simple as that.
Serikali inayolea wezi, inashindwaje kuingia mkataba wa kifisadi?!


Hoja yako dhaifu.
Karibia 75% wamelishwa maneno kuhusu issue ya huo mkataba na wala sio kwamba wameusoma wenyewe na kuuelewa kisha wao wenyewe wakabaini hayo mapungufu.
 
Kumbukumbu wanaolalamika ni wapinzani, raia wa kawaida na viongoz wa dini! NB: Mbona wezi na mafisad hawalalamiki kuhusu hii kitu? Tumeona dhahiri shahiri ufisadi upo ndan ya taasis refer report ya CAG. Na sio ndan ya wapinzani, raia wa kawaida na viongoz wa dini!!
 
Karibia 75% wamelishwa maneno kuhusu issue ya huo mkataba na wala sio kwamba wameusoma wenyewe na kuuelewa kisha wao wenyewe wakabaini hayo mapungufu.
Nilikubaliana na hoja yako kuwa watanzania ni wezi, na wameshindwa kuendesha miradi miaka 60.

Swali, serikali si ndio inasimamia yote?! Kwa nini usiseme wazi kuwa serikali imeshindwa, tukodi na wazungu waje watuendeshee nchi?!

Pili, kama watanzania ni wezi. Mwizi gani anaweza kukuletea mkataba usio wa kiwizi?!
 
Ndivyo ilivyo ukiona mapovu mengi kuhusu jambo fulani ujue mara nyingi hao ndio wanufaika wakuu wanahofia kupoteza !!
 
Bandari ni mali asilli za Taifa nadhani kuna mengi ya kujifunza kwenye hili kumbuka bandari nyingi zinaunganisha nchi zingine kama lango la kuingiza na kutoa bidhaa, (logistic business),kuna mambo ya usalama hapo mimi napendekeza kuwe na ubia wa kibiashara utengenezwe muundo ambao ni rafiki lakini siyo kuwaachia wao kuendesha peke yao . In entrepreneurship we learn how to do business not about business
 
Nakubaliana na wewe nikweli kabisa serikali imeshindwa hilo wala halina ubishi wowote ule

Kuhusu mkataba inawezekana kabisa una mapungufu au una upigaji ndani yake lakini nadhani kuhusu mkataka hebu tusilishane maneno kwanza tuvute subira
 
Naungana na wewe kwenye hilo
 
Nakumbuka wakati Mwalimu yupo madarakani alipata kusema hivi-:

Kiongozi anapofanya teuzi mbalimbali katika nchi anakuwa ni sawasawa na mtu ambaye amechukua ndoo na kwenda kisimani kuchota maji,

Akifika kisimani ataiteremsha ile ndoo kwenye kisima kisha atateka maji na kuondoka nayo kwenye ndoo yake !
Ila ukumbuke kwamba hayo maji yaliyomo kwenye ndoo ndio hayo hayo kama yaliyobaki kisimani !

Hata ukiyamwaga utaenda kuyachota tena palepale kisimani ! Sijui Mwalimu alikuwa anamaanisha nini πŸ˜…πŸ˜… ! R.I.P Mwalimu πŸ™πŸ™πŸ™
 
If you do not know where you are going any road or path will take you there, (km uendako hukujui njia yoyote itakupeleka usiko kujua)
 
Ni kweli kabisa tumeshindwakwa 100% na kwanini tumeshindwa ni kutokana na serikali kuendelea kulea wezi na mafisadi kwa sababu kwanza ni ma kada wa chama tawala wenye VVIP card na niwafadhili wakubwa wa chama na serikali.

Kwaiyo tuna kubaliana kuwa ccm haitufai?
 
Sawa twende na mawazo yako Watanzania wanaibaje hapo badarini tuelimishe tuelewe

Kama mamlaka zote ziko hapo bandaruni TRA pesa zao inaingia kwenye account ya Serekali mojakwamoja ukisha lipia unapewa release order na TRA Kisha unaenda bandarini TPA wanakupa invoince unalipa pesa zao moja kwamoja kwenye account za TPA

Niambia watanzania tunaibaje hapo hapo bandarini Au tuna haki account za Serekali?
 
Hivi ni kweli Hujui kwamba ndani ya serikali wapo ambao hawajapenda kabisa bandari kupewa muwekezaji na hao ndio waathirika namba moja endapo kweli muwekezaje atawekeza na kuendesha bandari kisasa kama inavyo daiwa?

Kwa sababu hiyo itaondoa na kuua madili mengi sana pale bandarini? Unadhani wanao pitisha mizigo kwa magendo pale bandarini ni wapinzani au hao wananchi wa nanjilinji?

Unadhani waziri au kada kindaki ndaki mwenye madili yake pale bandarini anaweza kusimama kwenye media na kupinga maamuzi ya serikali inayo tokana na chama chake?

Sasa hao hao ndio wanao pitishia hoja zao kwa wapinzani na wanaharakati ili wawasemee na kulalamikia swala la kumpa muwekezaji bandari

# ifahamike kwamba swala la usahihi au mapungufu ya huo mkataba wa DP WORLD sio hoja yangu#
 
Mimi nipo nalima huku Nanjilinji na ninaupinga huo mkataba kwa nguvu zote. Hayo maslahi niliyonayo kwenye Bandari ni yepi?

Hoja yako imepoteza uhalali

Wewe ni katika wale mliodanganywa na hilo kundi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…