Wengi wanaopiga kelele kuhusu bandari ni wapitisha mizigo kimagendo bandarini

Wengi wanaopiga kelele kuhusu bandari ni wapitisha mizigo kimagendo bandarini

Karibia 75% wamelishwa maneno kuhusu issue ya huo mkataba na wala sio kwamba wameusoma wenyewe na kuuelewa kisha wao wenyewe wakabaini hayo mapungufu.
Dawa ni kuwaelekeza hao 75% kwa kuwaonyesha vifungu vya mkataba vinavyoonyesha ukweli wa mambo ili uaminike. Asante
 
Sawa twende na mawazo yako Watanzania wanaibaje hapo badarini tuelimishe tuelewe

Kama mamlaka zote ziko hapo bandaruni TRA pesa zao inaingia kwenye account ya Serekali mojakwamoja ukisha lipia unapewa lerease order na TRA Kisha unaenda bandarini TPA wanakupa invoince unalipa pesa zao moja kwamoja kwenye account za TPA

Niambia watanzania tunaibaje hapo hapo bandarini Au tuna haki account za Serekali?
Kwani inakuwaje mita za mafuta hazisomi? Na kwanini zisisome? Inakuwaje pia swala la mashine za scanning machine kila mara zishindwe kuscan kwa kile tunacho ambiwa mbovu kila mara? Halafu nini hasa kinasababisha watu kukaa bandarini karibu wiki mbili hadi mwezi mzima kwa issue za kufanya clearance! Nini tatizo

kwenye ushuru wa forodha kuna shida gani ya makadirio pale bandarini?halafu kwanini kuna kontena zingine hazipiti kwenye scanning machine zina nini ndani? Na kwanini kontena zingine zinapita mlangibwa nyuma haziingii kwenye mfumo wa ukaguzi kuna shida gani pale

Hivi inaingia akilini mtanzania aache bandari ya dar es salaam akapokelee mizingo yake mombasa kenya ninini ambacho anakikosa hapo bandari salama anakipata kenya ? Na hili sio la jana wala la leo bali ni tatizo ambalo lina couple of years.
 
Hivi ni kweli Hujui kwamba ndani ya serikali wapo ambao hawajapenda kabisa bandari kupewa muwekezaji na hao ndio waathirika namba moja endapo kweli muwekezaje atawekeza na kuendesha bandari kisasa kama inavyo daiwa ?

Kwa sababu hiyo itaondoa na kuua madili mengi sana pale bandarini? Unadhani wanao pitisha mizigo kwa magendo pale bandarini ni wapinzani au hao wananchi wa nanjilinji?

Unadhani waziri au kada kindaki ndaki mwenye madili yake pale bandarini anaweza kusimama kwenye media na kupinga maamuzi ya serikali inayo tokana na chama chake?

Sasa hao hao ndio wanao pitishia hoja zao kwa wapinzani na wanaharakati ili wawasemee na kulalamikia swala la kumpa muwekezaji bandari

# ifahamike kwamba swala la usahihi au mapungufu ya huo mkataba wa DP WORLD sio hoja yangu#
Unadhan ubinafsishaji ndio muarobaini wa ufisadi nchini?
 
Bandari ni mali asilli za Taifa nadhani kuna mengi ya kujifunza kwenye hili kumbuka bandari nyingi zinaunganisha nchi zingine kama lango la kuingiza na kutoa bidhaa, (logistic business),kuna mambo ya usalama hapo mimi napendekeza kuwe na ubia wa kibiashara utengenezwe muundo ambao ni rafiki lakini siyo kuwaachia wao kuendesha peke yao . In entrepreneurship we learn how to do business not about business
Hawa badala ya kufikiri kuigeuza kuwa free port kama ilivyo Dubai na Durbin kuongeze mapato wanawaza kuuza

Bandari ikiwa free port wafanya biashara duniani kote wataleta mizigo mingi na kuuzia hapa Kisha serekali inapata kodo kubwa ajira zinaongezeka na uchumi unakuwa, badala ya wafanya biashara kusafiru kufata mizigo nje ya mchi wanaletewa hapa bandari nchi jirani watakuja hapa kununua bidhaa nakuacha safari za kwenda Dubai na China
 
Kwa hiyo huo ndo udini, au wewe ndo unataka kuchomeka hoja zako za udini! tulia mzee watu tuendelee kupambania bandari yetu, usitutoe kwenye reli.

Kauze kahawa ..acha porojo
 
Tunaomba materials na Methods au Methodology uliotukua kufanya utafiti wako Mdogo
Na ndio hapo hapo ambapo watanzania mnafeli kujifanya mnahitaji takwimu za kisomi na kuachana na ku deal na tatizo

Utatuzi na ubainifu wa matatizo ni vitu viilivyo kuwepo kabla hata ya hizo porojo za methods na methodology unazo taka ? Ina maana matatizo yalikuwa hayatatuliwi? Acha kujifanya msomi wakati umekalili.
 
Serikali iliyoshindwa kusimamia bandari ndio ing'atuke waingie watu wenye uwezo.

Nchi haiwezi kuendelea kwa akili za kuwaza kuuza uza kila kitu

Serikali ngapi zimepita na ufisadi bdo hauishi kwenye bandari
 
Unaachanaje na Watanzania kusimamia miradi?!

Sasa kwa nini tusikodishe serikali kuendesha nchi!

Huwezi kusema watanzania ni wezi, unakataa kwamba mkataba walioingia hao wezi sio wa kifisadi .

Mwizi anawezaje kukuletea jambo jema?!

Mradi gani tumesimamia vizur?Hakuna nchi ambayo inaendesha kila kitu wao wenyewe tuh...
 
Hawa badala ya kufikiri kuigeuza kuwa free port kama ilivyo Dubai na Durbin kuongeze mapato wanawaza kuuza

Bandari ikiwa free port wafanya biashara duniani kote wataleta mizigo mingi na kuuzia hapa Kisha serekali inapata kodo kubwa ajira zinaongezeka na uchumi unakuwa, badara ya wafanya biashara kusafiru kufata mizigo nje ya mchi wanaletewa hapa bandari
Wazo zuri pia lakini tatizo kubwa tanzania ni management kukiwa na kuwajibishana bila kuangaliana usoni wala hakuna haja ya kumpa muwekezaji kotu chochote kile na hata mtandao wa TTCL ungekuwa ndio mtandao wenye coverage kubwa kuliko mitandao yote nchi hii

Tatizo kubwa hapa ni watu walewale wenye mawazo yaleyale fikra zilezile na wizi uleule ndio wapo kwenye uongozi tangu tupate uhuru hadi sasa ndio maana aina ya wizi ni ile ile miaka yote.

Angalau mzee magufuli alianza kubadilisha kizazi cha uongozi nchini ila ndo hivyo tena
 
Kwani inakuwaje mita za mafuta hazisomi? Na kwanini zisisome? Inakuwaje pia swala la mashine za scanning machine kila mara zishindwe kuscan kwa kile tunacho ambiwa mbovu kila mara? Halafu nini hasa kinasababisha watu kukaa bandarini karibu wiki mbili hadi mwezi mzima kwa issue za kufanya clearance! Nini tatizo

kwenye ushuru wa forodha kuna shida gani ya makadirio pale bandarini?halafu kwanini kuna kontena zingine hazipiti kwenye scanning machine zina nini ndani? Na kwanini kontena zingine zinapita mlangibwa nyuma haziingii kwenye mfumo wa ukaguzi kuna shida gani pale

Hivi inaingia akilini mtanzania aache bandari ya dar es salaam akapokelee mizingo yake mombasa kenya ninini ambacho anakikosa hapo bandari salama anakipata kenya ? Na hili sio la jana wala la leo bali ni tatizo ambalo lina couple of years.
Yote unazungumza mambo ya mitter kutokusoma scanner yote yako chini ya TRA sio TPA mkuu mbona unarudia makosa kila ukiandika hapo bandari au TPA inahusikaje au watanzania tunahusikaje hapo? Dp unayotetea itasaidiaje majukumu ya TRA?
 
Hawa badala ya kufikiri kuigeuza kuwa free port kama ilivyo Dubai na Durbin kuongeze mapato wanawaza kuuza

Bandari ikiwa free port wafanya biashara duniani kote wataleta mizigo mingi na kuuzia hapa Kisha serekali inapata kodo kubwa ajira zinaongezeka na uchumi unakuwa, badara ya wafanya biashara kusafiru kufata mizigo nje ya mchi wanaletewa hapa bandari
Not free port but run a competitive business comparing to other ports in Africa the challenge will be taxi and rate settings which is not friendly, there should be a well organized coordination and positioning the business to global network and customers
 
Unadhan ubinafsishaji ndio muarobaini wa ufisadi nchini?
Tatizo terms za mikataba tu ila kwa hali ilivyo nchi hii angalau hiyo njia itasaidia kidogo kuongeza hata 15% ya pato hadi hapo tutakapo weza kuamza kuwajibishana bila kuangaliana usoni bora chongo kuliko kukosa kabisa, kuliko hii hali iluvyo sasa watu wachache wanapiga pesa halafu wanatuambia taasisi zinajiendesha kwa hasara.
 
Yote unazungumza mambo ya mitter kutokusoma scanner yote yako chini ya TRA sio TPA mkuu mbona unarudia makosa kila ukiandika hapo bandari au TPA inahusikaje au watanzania tunahusikaje hapo? Dp unayotetea itasaidiaje majukumu ya TRA?
Hakuna kitu TRA wanaweza kufanya pasi na ushirika na TPA kwa sababu mifumo yao inawasiliana kwa maana hiyo hapa si TPA si TRA wote ni wachafu
 
Wazo zuri pia lakini tatizo kubwa tanzania ni management kukiwa na kuwajibishana bila kuangaliana usoni wala hakuna haja ya kumpa muwekezaji kotu chochote kile na hata mtandao wa TTCL ungekuwa ndio mtandao wenye coverage kubwa kuliko mitandao yote nchi hii

Tatizo kubwa hapa ni watu walewale wenye mawazo yaleyale fikra zilezile na wizi uleule ndio wapo kwenye uongozi tangu tupate uhuru hadi sasa ndio maana aina ya wizi ni ile ile miaka yote.

Angalau mzee magufuli alianza kubadilisha kizazi cha uongozi nchini ila ndo hivyo tena

Mkuu wa tz wengi hawana msimamo wao kila kitu wakiambiwa na mwanasiasa wanakieka kichwani na kuanza kubwabwaja..
Kampuni kibao tunaendesha wenyewe zinafanya utumbo tuh
.1.ttcl
2.atcl
3.Tanesco
4 bandari nk
Zote izo tuko nazo wenyewe na kila cku zinapata hati chafu na ufisadi ulikithir.afu bdo jitu linajidai kwan hatuezi jiendesha wenyewe 🥸
 
Not free port but run a competitive business comparing to other ports in Africa the challenge will be taxi and rate settings which is not friendly, there should be a well organized coordination and positioning the business to global network and customers
English is not our national language ulimbukeni sio lazima kujua kingereza andika kiswahili nitakujubu
 
Yote unazungumza mambo ya mitter kutokusoma scanner yote yako chini ya TRA sio TPA mkuu mbona unarudia makosa kila ukiandika hapo bandari au TPA inahusikaje au watanzania tunahusikaje hapo? Dp unayotetea itasaidiaje majukumu ya TRA?

Kwa hio wataka kusema tpa haina makosa ila tra ndio inafanya wizi
 
Hakuna kitu TRA wanaweza kufanya pasi na ushirika na TPA kwa sababu mifumo yao inawasiliana kwa maana hiyo hapa si TPA si TRA wote ni wachafu
Sio kweli TRA na TPA ni mamlaka mbili tofauti mkuu kila mamlaka inajitegema
 
Back
Top Bottom