CCM nawashauri mlireserve comments zenu maana hii league ndo kwanza imeanza....uhakika wa kutangazwa unaweza kuwepo ila uhakika wa kuongoza bado ni fumbo....
 
Kwahali hii sidhani kama vyama pinzani watashinda
Never never never.
 
Haya sasa, Mwenyekiti Mbowe chali.
Unapofika mahali hadi Mwenyekiti unakosa nafasi bungeni, ujue chama hicho kwisha habari yake.
Rejea hali ya vyama kama nccr, tlp, udp, cuf, tadea nk
Kuingiza watu barabarani sio option, watanzania sisi ni waoga kwelikweli, ujinga na umaskini tulio nao ni mwingi hasa.
Mwenyekiti huu si muda wa kufikiria ufanye nini, njoo na solution ulioiandaa na ifanyiwe execution. Kama unafikiria kuingiza watu barabarani, sahau.
 
Trend ipi mataga ya kuwatoa mawakala kwa nguvu?
Mkuu "MbeyaIlembo" zoezi la kupora Uchaguzi huu liliratibiwa kibabe na Tume ya Uchaguzi kwa kuwezeshwa na vyombo vyetu vya Ulinzi. Mfano ni pale Halima Mdee wa Kawe alipokamata mabegi ya kura ambazo tayari Tume ya Uchaguzi iliwapigia wagombea wa CCM kwa niaba ya wananchi.

Ajabu ni kwamba Vyombo vyetu vya Ulinzi havikuchua hatua yoyote kuhusu kura hizo haramu zilizokuwa kwenye mabegi hayo. Unaweza kuamini kuwa Halima Mdee alikamatwa na Polisi kimkakati ili kutakatisha kura Haramu katika vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Kawe.

Kwa uchache nimepiwa simu kuwa kwenye vituo vingi vya kupigia kura mawakala wa CHADEMA na ACT walikuwa kwa muda wanatolewa nje kibabe kwa visingizio mbalimbali. Na kwa sababu Jimbo la Kawe imeonekana Tume ya Uchaguzi ndo mmiliki wa kura zilizokuwa zimepigwa kwa niaba ya wananchi, unaweza kuamini kuwa mawakala wa CHADEMA na ACT walitolewa nje kibabe ili kulahisisha utakatishaji wa kura Haramu walizopigiwa wagombea wa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…