Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
Nampongeza sana Magufuli kwa kuzima mitandao, kuna watu wangeshinda katika mitandao badala ya kwenda kupiga kura. Huku katika mitandao hakuna vituo vya kupiga kura wote leo tukapige kura hakuna kisingizio na wale wataalam wa Twitter nadhani sindano imewachoma.

Kuna siri kubwa nyuma ya pazia kuhusu mitandao ya kijamii, narudia kumpongea mzee kwa kuweka MAKUFULI katika mitandao [emoji1319][emoji1319][emoji1319]
Ni jambo Zuri ila si kwa Dunia ya sasa.
 
Ni jambo Zuri ila si kwa Dunia ya sasa

Dunia ya sasa nayo ukiiendekeza bila kuwa na mipaka mtajikuta mmesombwa wote na mafuriko... bado tulihitaji kuwekewa mipaka speed yetu ilikuwa kubwa sana
 
Leo Ndio Leo,kwenye Jimbo lililoongozwa na upinzani Miaka 25..

Je Priscus Tarimo Atavunja Mwiko huu? Au Raymond wa CHADEMA ataendeleza desturi?

Figisu,fitna,ubabe na mengineyo yote tupia hapa na mm nitakua nikikupa updates zote
Jimbo gani hilo?
 
Ni wote. Kwa tunautumia mobile network
Kazi kwelikweli! Ili tusichat badala yake tukapige kura! Ilibidi wafanye hivyo saa za Kazi na wanafunzi wakati wa mitihani! Nqvyo muhimu
 
Jamaa hawako serious zinebaki dk 5 bado hawajafika kituoni
20201028_065408.jpg
20201028_065408.jpg
 
Nashukuru sana Mungu kwa siku hii ya leo.

Nimefika kituo cha kupiga kura tangu saa 9:15 alfajiri, hali ni shwari kabisa mahala nilipo na mvua inapiga kwa mbali.

Ile siku imewadia
 
Ni siku kuu Siku ileee, Ya kumkiri Mwokozi, Moyo Umejaaa Teleee Kunyamaza Hauwezi

Siku Kuu Siku kuu, Ya kuoshwa dhambi zangu Kuu, Hukesha na Kuomba tu🎼🎼

Ndugu watanzania, leo ndo ile siku yetu kuu, ya kuweka historia kuu, hapa Tanzania, twendeni tukapige kura kumuondoa Magufuli na Ccm madarakani ili tuweke mustakabali bora wa Tanzania yetu na vizazi vyetu vijavyo. Imetosha hakika. Tukamchague Tundu Antiphas Lissu kwa ajiri ya Tanzania mpya yenye Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.
 
Back
Top Bottom