Mimi tayari Niko kituoni. SAA 9:45.
SAA ya Ukombozi ni sasa, majuto ni Mjukuu, usifanye makosa
Kweli hapo umenipiku, yaani saa 9:45 upo kituoni! Mimi nilikuwa kituoni toka saa 11.00 Alfajiri nimetoka saa 2:47 asubuhi. Tumeanza kupiga kura kuanzia saa 1:35 asubuhi. Wasimamizi wametupanga upande mmoja akina mama (wanawake) upande mwingine akina baba (wanaume). Msaidizi anaita kutoka kila upande. Mambo yanaenda vizuri.
Jambo moja tu la kurekebisha kwa usimamizi wa uchaguzi kwa siku zijazo ni hili. Tunapenda sana wenzetu ambao wana matatizo ya Afya, wazee, akina mama wanaonyonyesha, wajawazito na walemavu wapewe kipaumbele cha kuwahi kupiga kura ili wakapumuzike na wasikae kwenye foleni muda mrefu. Lakini kwa kuwa kuna wengine wamewahi sana pale kituoni ili wakapige kura hasa kwa upande wa akina mama lakini mpaka naondoka walikuwa bado hawajuruhusiwa kuingia kupiga kura.
Hii ni kwa sababu kuna mama wanaonyonyesha walikuja baadaye na walikuwa wengi na wao ndiyo sasa wakawa wanaruhusiwa kupiga kura. Hii imekera wale wa mama waliowahi pale kituoni. Na nimeacha kuna dalili baadhi watalazimika kuondoka bila kupiga kura leo.
Nimejaribu kuwashauri wasimamizi waangalie namna bora ya kutokuwakera wapiga kura hawa; wasimamizi hawakutaka kabisa kunisikiliza wakasema wao wanafuata masharti tu yaliyobandikwa pale nje kwa ajili ya mpigakura . Na mimi sikutaka kulazimisha maana sina mamlaka hayo.
Nilitaka kuwashauri kuwa wale wenzetu waliopewa kipaumbele kupiga kura kwanza iwe ivyo waendelee kupewa kipaumbe hicho. Lakini iwe hivi, wakipiga kura wawili wale ambao hawana kipaumbele basi ndiyo aingie mmoja mwenye kipaumbele cha kupiga kura kabla ya wengine. Binafsi nadhini hili lingepunguza manung'uniko na kukereka kwa wapigakura hawa.
Kwa hiyo, ushauri niliyotaka kuwapa wasimamizi wa kituo hicho nilipokwenda kupiga kura leo, ni maoni yangu kuwa uchaguzi ujao, basi ushauri huu ufuatwe. Nadhani hili litarekebeshwa kwa kufuata sheria na taratibu za nchi yetu ili sheria za Uchaguzi za nchi ziakisi utatuzi wa kero hii.
Nawatakia uchaguzi mwema.