Uchaguzi 2020 Yaliyojiri sehemu mbalimbali Tanzania katika zoezi la upigaji kura za Rais - Oktoba 28, 2020
Haya mnayo yaona leo ni matokeo ya mtu mmoja Mbowe ya kumleta Lowassa Ukawa, hili lilikuwa bonge la kosa ambalo kwa mtu makini kabisa kwa kosa lile alitakiwa ajihuzuru, ila Mbowe anadunda, untouchable, ukimkosoa humu watu wanakushambulia.
images (23).jpeg


Nilikuwa mwanasiasa kindakindaki wa CHADEMA chuo kuanzia 2009 ila baada ya Lowassa kuingia nilikaa pembeni, nikabezwa,nikapondwa baada ya UKAWA kupata viti vyingi bungeni ila baada ya wabunge kuanza kurudi CCM, kuna watu niliwaambia 2020 hali itakuwa mbaya sana na leo tuna yaona.

CHADEMA mlivyo mleta Lowassa UKAWA na kujiamini kwamba mpo imara kumbe mliacha nyumba yenu mliyokuwa mnaijenga kidogo kidogo kwenye mwamba na kwenda kujenga kwenye mchanga kisa tu kuna urahisi. Sasa angalieni leo mnayoyapata ni haki yenu hamjaibiwa hata kura moja.

CHADEMA mkitaka kusimama tena mnabidi muanze upya mfumue chama chote na mkijenge CHAMA kupitia vijana wenu na watu wenu mlio waandaa nyinyi na si kunyakua wanasiasa kutoka CCM na mnatakiwa kuwaamini watu wenu.

MMEVUNA MLICHO KIPANDA.
 
MALIPO YA DHULUMA NI LAANA NA KIFO

LAANA YA MUNGU IWAPATE WOTE WALIOSHINDA KWA DHULMA NA WIZI

BARAKA ZA MUNGU ZIAMBATANE NA WALIOSHINDA KIHALALI NA WALIO TAYARI KUWATUMIKIA WANANCHI
 
Lissu awe mstaarabu akubali matokeo maana hii ya kuanza kupitapita kabla matokeo hayajatangazwa ni dalili ya kutokubali kuyapokea matokeo.

Je wabunge wake (endapo watashinda) watatoka Bungeni siku ya kulizindua?

Amen
 
Watumishi wa umma tuna jambo letu.
Wamachinga tunajambo letu.
mara sijui,,,bodaboda tuna jambo letu.

"minikajiuliza jambo gani hilo la tarehe 28"
kumbe ni ushindi wa kishindo wa JPM zaidi ya 90%.
Viva JPM.
Viva wananchi watanzania.
 
Back
Top Bottom