Yule ni mwanae sana tena saana,sidhani kama atamuacha hivi hivi tu mikono mitupu.
Sawa kiongozi nimekuelewa sana kwamba Mnyeti mtu wa familia ila Kitwanga kwa kuwa ni rafiki wa Jiwe na kwamba Ubunge ameukosa imani yangu ni kwamba baada ya uchaguzi wa 2020 atapewa uteuzi wowote ule hatamwacha hivi huvi
 
CCM imetengeneza 1,036,100,000 kupitia ada za fomu za ubunge na uwakilishi. kweli mwenye nacho huongezewa.
bado nasikia kuna michango mbalimbali isiyo rasmi wanatakiwa kulipia mbali na hiyo ada
Natumai panapimajaliwa mwaka 2025 hii ada lazima ipande..hata mwaka huu ingepanda sema hawajashtukia mchezo mapema kama watu watakua wengi kiasi hiki
 
Kama watanzania wa vyama vyote tungekuwa na Nia njema ya kuleta maendeleo ya nchi yetu Hawa wabunge ambao wamekaa bungeni zaidi ya miaka kumi tungewakataa katika uchaguzi huu. Haiwezekani mtu anakuwa Mbunge Hadi miaka ishirini na bado tu anautaka ubunge Tena utadhani Jimbo Hilo ni yeye tu mwenye sifa za kuwa mbunge.

Hii ingesaidia watu na hawa viongozi kutambua umuhimu wa katiba mpya na kuacha mawazo ya kudhani kuwa wao ni raia wa faraja la juu kuliko wengine, kwanza Hawa wabunge wa aina hii hawana jipya zaidi ya kujipendekeza na kupiga majungu kwa wenye mamlaka tu.

Wanayo majina yao eti maseneta wapishe wengine hao hata Kama watapishwa na upinzani wasichaguliwe, wakipitishwa na CCM wananchi tusiwachague.
 
Uwe unapandisha matokeo juu ,nimeona Jimbo la mwigulu tayari matokeo lakini kwenye update hakuna...Hatuna muda wa kusoma comments zote unless tagged.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…