Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Millard Ayo bana [emoji23][emoji23][emoji23]
IMG_20200720_211323_064.JPG
 
Watoto wa kiume wa Mwalimu Julius Nyerere, Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Makongoro na Madaraka, wamekataliwa kwa kura nyumbani kwao Butiama, Mara.

Watoto hao wa Mwalimu Nyerere, walikuwa wakiomba ridhaa ya kupitishwa, kugombea ubunge na wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Bunda, kupitia chama cha CCM.

Katika mkutano huo ulifanyika leo, matokeo yanaonyesha kwamba vijana hao wa Mwalimu, wamebwangwa vibaya.

Hadi naandika hapa, matokeo yameonyesha kuwa Makongoro na Madaraka wote wameshindwa kuingia hata 10 bora.

Sasa wanasubiri kudra za Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kama atakuwa na njia ya kurejea jina la mmoja wao au wote, kati ya matatu ili kupata mmoja atakayepeperjsha benders ya chama hicho tawala kwa nafasi ya ubunge wa jimbo hilo.

Matokeo yanasomeka: Jumanne Sagini (kura 84), Frank Mahemba (80), Joseph Nyamboha (46), Manyerere Jackton (22), Makongoro Nyerere (3), Madaraka Nyerere (2).

Wagombea walikuwa 59, wapiga kura 555.

Akitangaza matokeo haya, msimamizi wa uchaguzi huo, Msafiri Mtemi amesema zoezi la kupiga kura lilifanyika kwa uwazi mkubwa na kuwataka wagombea wote kuheshimu matokeo.

Msimamizi huyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, amesema uamuzi wa nani atakuwa mgombea utatangazwa na chama chao baada ya kufanyika kwa mchakato mwingine katika mgazi za wilaya, mkoa na hatimaye halmashauri kuu.

Makongoro ambaye amewahi kuwa mbunge wa Arusha kupitia chama cha NCCR - Mageuzi na baadaye kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati Madaraka ndiyo ameingia mara ya kwanza kujaribu bahati yake.

Waulize hao Watoto wa Hayati kuwa Watoto wa Diego Maradona nao ' Wanaupiga ' kama Baba yao? Wamekurupuka mno na hawakujitathmini pia.
 
Mambo sasa hadharani. Siyo rocket science wala brain surgery. Ni hesabu rahisi tu za logic.

Ni hivi...

Kwa siasa za ndani na nje ya CCM, Makonda ni taswira ya JPM.

Huko Kigamboni, Makonda kaambulia 34.76% ya kura.
Hiyo ndiyo opinion ya wana CCM wa Kigamboni dhidi ya Makonda (mirroring JPM).

Hapana shaka kuwa huo ndiyo pia mtizamo miongoni mwa wana CCM walio wengi, wakiwamo wajumbe wa mkutano mkuu wao uliofanyika hivi karibuni kule Dodoma.... kwamba ndani ya mioyo ya wana CCM, JPM atakuwa anakubalika kwa 34.76% tu na siyo ile 100% ya maigizo.

Jee, ni nini tafsiri ya yote haya kuelekea uchaguzi mkuu October 2020?
Jibu ni rahisi.... kwamba kama uchaguzi mkuu ungekuwa unafanyika katika mazingira huru na haki, JPM asingeweza kuambulia hata 30% ya kura za Watanzania.

Makonda amekuwa ni barometer kuelekea October 2020.

Ni logic rahisi tu.
 
Mkuu usijenge daraja kabla hujauona mto,amini usiamini huu sio mwisho wa Makonda anaweza hata kuteuliwa kwa na mkuu kuwa mbunge na akawa waziri au hata kurudishwa kwenye ukiranja wa mkoa,au mumesahau ya Andengenye
Hayo yote yanawezekana. Kikubwa ujumbe umefika bila chenga.
 
Shigongo sio wa leo kwenye ulingo wa siasa za kibunge, sio mtu mdogo kabisa.

Shigongo kaanza kugombea na Amina Chifupa RIP

Na ugomvi wao mpaka anamuandama na magazeti yake ni nafasi ya kupitia UVCCM Amina alimshinda kwa kutumia kigezo cha gender.

Pia Shigongo ni mfadhili wa CCM siku nyingi mpk akadhulumiwa kontena zima la T shirts(Mama Zakia Meghji akiwa Mhazini mkuu akamwambia kunywa maji mwanangu😄😄)
 
Back
Top Bottom