Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Waziri wa Fedha Dr. Mpango anakabiliana na mhe. Obama mbunge anayetetea kiti hicho jimbo la Buhigwe. Kasulu mjini ni waziri wa Elimu Prof.lJoyce Ndalichako dhidi ya Daniel Nsanzugwako mbunge anayetetea jimbo hilo. Dr Mpango anatokea eneo lililo pembeni mwa jimbo hilo na lenye wakazi wachache huku Obama akiwa mzaliwa wa Manyovu upande wenye wakazi wengi. Kwa upande wa Ndalichako huyu amekulia na kusomea Kigoma mjini japo asili
yao in Kasulu mjini. Awali alikuwa agombe Kigoma mjini lakini akakimbilia Kasulu baada ya kuona jimbo hilo uamuzi wa kuwa mbunge huamliwa na wazee wa Ujiji ambao ni waislamu.
Kwani hao wazee waislam ndio wanaopiga kura peke yao? au wao ndio wasimamizi wa uchaguzi? Nini kimepelekea hadi kuingiza udini katika hili? au ni chuki zako tu kwa waislam?
Kasome vizuri historia ya nchi hii ujue mchango wao na jinsi walsivyokuwa na uchu wa madaraka ila wanapenda haki.
 
Kigoma Mijini waislam ni wengi kwa maana hiyo wao ndiyo waamuzi wa nani awe mbunge.

Ni Kama Zanzibar. Pale Mkristo akigombea hawezi kushinda.

Kwa hiyo usitoe povu sana wakati mwenzako kasema ukweli
 
Mkuu macho na masikio yangu yapo Siha kwa sasa, natumai moleli atarudi kwao kuchunga ng'ombe na ndugu yetu Mwandri kupewa idhini ya kulitetea jimbo
Acha kujidanganya mkuu. Mbunge mstaafu na mapesa kibao ya pensheni tena ni daktari anaanzaje kuchunga ng'ombe?
 
Kigoma Mijini waislam ni wengi kwa maana hiyo wao ndiyo waamuzi wa nani awe mbunge.

Ni Kama Zanzibar. Pale Mkristo akigombea hawezi kushinda.

Kwa hiyo usitoe povu sana wakati mwenzako kasema ukweli
Kwani wao ndio wasimamizi wa uchaguzi mkuu? maana kasema wazee wa kiislam, ni kwa vipi wao ndio waamue? mbona moshi na mbeya wakristo ni wengi so kwanini isiwe wazee wa kikristo ndio waamuzi maeneo hayo na sio tume?
Tatizo ni kuwa waislam wanaandamwa sana hasa sababu ya dini yao hata kama waislam hao sio wenye kutekeleza huo islam.
So, sehemu zenye wakristo wengi, wakimchagua mkristo, nao ni udini?
 
Inaonekana huna exposure ya kutosha kujua desturi za sehemu husika.

Mfano Moshi ni Wakristo. Ila kinachoamua ni nani awe Mbunge ni mgombea kuwa mzawa wa asili wa eneo husika.

Akiwa muislamu hawezi kushinda labda awe na msimamo wa wastani na pia eneo husika kuwe na waislamu wengi na wasabato mfano same na mwanga
 
Huu mchakato wa CCM una kasoro yaani uchukuwe fomu halafu hakuna campaign; huo ushawishi wa kupigiwa kura unatokana na nini.

Uchaguzi wa namna hii unapendelea incumbencies na watu almaarufu; wengine ni wasindikizaji tu.
 
Moshi vijijini Kuna Ester Mmassy na Victor Tesha ambao watachuana vikali. Wengine hawana nguvu.

Ubungo yupo Emmanuel Maluli huyu ni Katibu wa Hamasa kata ya Makuburi.

Mwingine ni Cypirian Mrema ambaye Ni mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ubungo.

Pia yupo Kitila Mkumbo. Wengine siwajui
Ubungo Prof Kitila hakubaliki?!
 
Back
Top Bottom