Uchaguzi 2020 Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
Achana na mtoa povu huyo, hajui historia ya Ujiji. Kulikuwa na Mkuu wa Mkoa akiitwa Mzindakaya anaelewa nguvu ya wazee wa Ujiji. Walimwambia Serukamba nenda jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini na Zitto aje huku Kigoma mjini na wote mtakuwa wabunge na ikawa japo vyama tofauti. Amtafute Serukamba ilikuwaje.
Akapigwa chini
 
Huu mchakato wa CCM una kasoro yaani uchukuwe fomu halafu hakuna campaign; huo ushawishi wa kupigiwa kura unatokana na nini.

Uchaguzi wa namna hii unapendelea incumbencies na watu almaarufu; wengine ni wasindikizaji tu.
Ukichukua fomu unapita kwa wajumbe kila kata wapiga kura wakuone huku ukisubiri siku ya kujinadi kwa mara nyingine mbele yao
 
Salamu wandugu, shauku ni kubwa ya kupata matokeo ya watia nia wa nafasi ya ubunge CCM sehemu mbalimbali. Muda huu mchakato ukiendelea kwenye majimbo mbalimbali mwenye latest update anaweza kutumwagia hapa.
 
1 Kwanini Mkristo akigombea Zanzibar iwe hawezi kushinda ?
2.Kwani wazee wa kiislamu pale Ujiji wanamtishia kitu gani Profesa Ndalichako kama sifa anazo ?
[/QUOTE

Peter Serukamba ni mkristo Mbona alishinda Jimbo hilo kabla ya kuhamia Kigoma Kasikazini?
 
Haya kumeshakucha tena La mgambo likilia ujue kuna jambo.


Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, leo na kesho ni siku ya Mikutano Mikuu ya CCM ya Majimbo/Wilaya kupiga kura za maoni za wagombea wa ubunge na ujumbe wa baraza la wawakilishi

Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Magufuli waliochukua kugombea nafasi za Ubunge na uwakilishi ni 10,367. Waliokamilisha kujaza fomu na kurejesha ni 10,321.

Watanzania wataelekeza zaidi macho na masikio yao maeneo yenye upinzani mkali kama Kigamboni, Arusha mjini, Simanjiro, Kyela, Mbeya mjini, Mwibara, Misungwi, Same Mashariki, Tunduma, Tarime Vijijini na Ubungo ni baadhi ya maeneo yanayoangaliwa kwa jicho la tatu.

Ngoja tuone.

Up dates:

Maendeleo hayana vyama!
Misungwi kuna wagombea nani na nani jmn
 
HILI N KWA WALE WANAOGOMBEA NAOMBA NOWAJULISHE CHAMA CHA MAPINDUZI KINA MAMBO MENGI SANA KUKUCHAGUA KYWA MGOMBEA MWAKA HUU


Kukumbushaaa tu UNAPOONA JINA LAKO LIKO TATU BORA MPENDWA USICHINJE MBUZI KUSHANGILIA

MWAKA HUU MWAKA WA FURAHAAA ANASEMA KAKAYANGU MWAMPOSA DK

KAMA UMECHAGUKIWA SUBIRI MPAKA MAJINA YA MWISHO KULE YANAPOTOLEWA UKONA UPO FANYA SHUKRN

NASEMA HAYA KUWAANDAA WENZANGU KISAIKOLOJIA TUSIJE WAPOTEZA MANGULI WA SIASA KWA PRESURE KISA MATARAJIO AYAJAKUWA WANAVYOTARAJIA

KILA LA KHERI

CCM TANO TENA
DKJPM TANO TENA
 
Back
Top Bottom